Spika Ndugai ana jukumu la kumuita mbunge wa Gairo, Shabiby kwenye kamati ya maadili kwa kumtumia sms zisizofaa DC wa Gairo!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
44,323
2,000
Rais Magufuli amesema atalishangaa bunge kama halitamuita mbunge wa Gairo mh Shabiby na kumhoji kwa vitendo vyake vya kumtumia message zisizofaa Mkuu wa wilaya ya Gairo. DC huyo ambaye ni Mrs wa mtu amekuwa haelewani na mbunge kiasi cha mbunge kuanza kumtumia message za hovyo hata nyakati za usiku.

Je, Shabiby na Assad watagongana kamatini.

Ni hayo machache
Maendeleo hayana vyama!
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,920
2,000
Spika kaamriwa amwite Shabiby amhoji kuhusu sms Za Hovyo anazimtumia DC ambae Ni Mke wa Mtu!

Mzee Baba Siku hizi anapitia sms Za wenzie Kama zake vile

Hoja ya Prof inazidi kupata reference kwa Kuwa sasa Spika anapokea Maelekezo rasmi Na hadharani

Kasema live anaweza kumwambia Katibu Mkuu wa Chama amvue Uanachama apoteze ubunge Mara Moja
 

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,367
2,000
Dah.
Magufuli naye bana...

Ameshaanza kuingilia mpaka mambo binafsi kabisa ya maisha ya watu.
Sms mbovu mana yake nini??

Ni za vitisho??
Kwa nini DC asiende mahakamani??

Kama ni za mtongozo yeye zinamhusu nini??
Si awaache wamalizane wenyewe hata kama huyo mwanamke ni mke wa mtu??
Spika ataita wangapi wanaotongozana??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom