Spika Ndugai amvaa Zitto Kabwe kuhusu ripoti ya CAG

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
Spika wa Bunge Job Ndugai,amesema Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) anawadanganya wananchi. Spika Ndugai ameyaasema hayo bungeni leo mchana muda mfupi kabla hajaahirisha Bunge.

Ndugai amesema uchambuzi wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), unaofanywa na Zitto unalenga kuwaaminisha wananchi kwamba kila kilichomo kwenye ripoti hiyo ni cha kweli.

Amesema kwa upande wake humuungi mkono kwa kuwa ukweli wa ripoti hiyo hudhihirishwa na kamati mbili za Bunge ambazo ni kamati ya PAC na LAAC.

"Zitto Kabwe amekuwa mwepesi sana kwenye kutoa taarifa hasa zinazotoka ofisi ya CAG na wengi mnamtafsiri kama shujaa flani hivi, lakini kwa utaratibu wake zitaenda kwenye kamati, zile ni hoja tu. Watu wanawaaminisha watu kuwa kila kilichoandikwa kule ni ukweli 100%, sio hivyo, yapo mambo kule si kweli hata kidogo," amesema Spika Ndugai.

Pamoja na hayo Spika alisema Zitto anatumia muda wake mwingi kuichambua ripoti hiyo kwa kuwa anataka awe Mwenyekiti wa Kamati ya PAC kinyemela.
 
Huyu nae kwakujitekenya mwenyewe Kama hizo kamati hazijamchambulia au hazijapitia nakugundua yapi nikweli nayapi sikweli anasemaje aliosema zito niuongo apunguze midadi
 
Sasa yeye amejuaje kuwa yaliyomo ndani siyo kweli wakati hizo kamati zake anazozisema hazijaichambua hiyo ripoti?

Katika hili Ndugai hawezi kuaminika kwa sababu ameshaonyesha chuki ya wazi dhidi ya CAG, kwa hiyo sitoshangaa akifanya juhudi zote kuandermine kazi ya CAG ili yeye aonekane mzuri na CAG mbabaishaji
 
Hivi kuna lugha ambazo speaker na mawaziri ni ruksa kuwatolea watu wengine lakini ni marufuku wengine kuwaambia wao maneno kama hayo? Nauliza tu maana kumwambia Mbunge anadanyanya au waziri kumuita CAG "MUONGO" tena kutokana na findings zilizopo kwenye ripoti rasmi za ukaguzi naona ni maneno makali sana kuliko neno "DHAIFU" ambalo wanadai limewadhalilisha
 
Spika wa Bunge Job Ndugai,amesema Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) anawadanganya wananchi. Spika Ndugai ameyaasema hayo bungeni leo mchana muda mfupi kabla hajaahirisha Bunge.

Ndugai amesema uchambuzi wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), unaofanywa na Zitto unalenga kuwaaminisha wananchi kwamba kila kilichomo kwenye ripoti hiyo ni cha kweli.

Amesema kwa upande wake humuungi mkono kwa kuwa ukweli wa ripoti hiyo hudhihirishwa na kamati mbili za Bunge ambazo ni kamati ya PAC na LAAC.

"Zitto Kabwe amekuwa mwepesi sana kwenye kutoa taarifa hasa zinazotoka ofisi ya CAG na wengi mnamtafsiri kama shujaa flani hivi, lakini kwa utaratibu wake zitaenda kwenye kamati, zile ni hoja tu. Watu wanawaaminisha watu kuwa kila kilichoandikwa kule ni ukweli 100%, sio hivyo, yapo mambo kule si kweli hata kidogo," amesema Spika Ndugai.

Pamoja na hayo Spika alisema Zitto anatumia muda wake mwingi kuichambua ripoti hiyo kwa kuwa anataka awe Mwenyekiti wa Kamati ya PAC kinyemela.
Hata yeye kama Spika hatakiwi kuwa upande wowote kwenye mjadala wa ripoti, sio kazi yake.
Kauli yake kwamba ripoti ya IMF ina uongo nayo inapotosha wananchi.
 
Spika wa Bunge Job Ndugai,amesema Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) anawadanganya wananchi. Spika Ndugai ameyaasema hayo bungeni leo mchana muda mfupi kabla hajaahirisha Bunge.

Ndugai amesema uchambuzi wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), unaofanywa na Zitto unalenga kuwaaminisha wananchi kwamba kila kilichomo kwenye ripoti hiyo ni cha kweli.

Amesema kwa upande wake humuungi mkono kwa kuwa ukweli wa ripoti hiyo hudhihirishwa na kamati mbili za Bunge ambazo ni kamati ya PAC na LAAC.

"Zitto Kabwe amekuwa mwepesi sana kwenye kutoa taarifa hasa zinazotoka ofisi ya CAG na wengi mnamtafsiri kama shujaa flani hivi, lakini kwa utaratibu wake zitaenda kwenye kamati, zile ni hoja tu. Watu wanawaaminisha watu kuwa kila kilichoandikwa kule ni ukweli 100%, sio hivyo, yapo mambo kule si kweli hata kidogo," amesema Spika Ndugai.

Pamoja na hayo Spika alisema Zitto anatumia muda wake mwingi kuichambua ripoti hiyo kwa kuwa anataka awe Mwenyekiti wa Kamati ya PAC kinyemela.

Kwa hiyo. inamaana SPIKA kaona kwenye ripoti ya CAG kuna vya uongo?

Najaribu kuunganisha DOTS....
1. KANGI KASEMA CAG MUONGO
2. Spika anasema siyo kila kilichomo kwenye ripoti ya CAG ni kweli… kwa maneno mengine CAG ni muongo..!!!!

Spika atueleze kwenye ripoti nzima UONGO NI UPI NA UKWELI NI UPI..

Kwa mtazamo wangu, Sakata la CAG, lazima lina mkono mzito unaowalinda akina Kangi na Spika…. huwezi toa kauli ya hivyo BILA USHAHIDI halafu ubaki salama...
 
Back
Top Bottom