Spika Ndugai alitaka Bunge kubadili Sheria ya HESLB ili wanafunzi wa VETA na NACTE wapate mikopo pia

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,477
Nimependa mapendekezo ya Spika leo.

Anataka kuona sheria inayowapa mikopo wanafunzi wa TCU, VETA, NACTE.

Anataka 70% ya fedha za HESLB ziende ktk sayansi na teknolojia.

Ameyasema haya kwenye kilele cha mashindano ya sayansi, teknolojia na ubunifu.

Kila la kheri wabunge wetu. Tumieni hati ya dharula kutekeleza jambo hili

Lakini msisahau kuwa ufanisi wa mawazo haya utahitaji Bodi hii kupewa uwezo wa kufanya harambee duniani kote ili kutunisha mfuko wake.
 
Hiyo anatafutatu kusifiwa. Waliopo vyuoni ambao ni maskini,yatima na ombaomba hawana mikopo.
Bodi haina uwezo wa kusaidia maskini inaongezewa tena mzigo!!

Aibu kwako kimbunga jobo
 
Wazo zuri ila anavyotaka 70% iende kwenye science na teknolojia maana yake anataka kuziua hizi course nyingine, ni sawa na kuhamisha tatizo lililopo science waanze kufurahia then arts waanze kulalamika.
 
Huyu Jobo amekula nini??? Sheria zote zinazo tumika zime pita hapo bungeni. Yeye akiwa kinara. Anapo zitoa makosa tuna muona kama kaazi mbatata yeye na wabunge wake wasio na vision.
Maji Kongwa debe 1000/
Jimbo la spika..
Screenshot_20210511-110253.jpg
 
Linaweza kuwa ushauri mzuri lakini huu unakidhi kwa kiwango kipi kwa wanufaika walipo? Pia wazo mbona kama limewahi kufikishwa bungeni moja mabunge yaliyopita ilishindikana vipi kucanyiwa kazi Hadi wazo litolewe leo.
 
Wazo zuri ila anavyotaka 70% iende kwenye science na teknolojia maana yake anataka kuziua hizi course nyingine, ni sawa na kuhamisha tatizo lililopo science waanze kufurahia then arts waanze kulalamika.
Kusomea manunuzi
 
Kozi za arts haziitajiki,mtu kama anataka mkopo aende VETA kule hawabagui hata kama ni arts unapokelewa.
 
Back
Top Bottom