Spika Ndugai akitimiza azma yake ya kumvua Tundu Lissu ubunge wake kwa ubabe ndiyo atakuwa amejiharibia kabisa!

Masikini

'Masikini aonewe lakini ni lazima haki apewe'
Kwenye hili, mimi ninadhani tunamuonea spika na kwenye hili jamvi hili inabidi ilijadili jambo hili bila jazba.
1. Ndugu Tundu Lissu ni kweli alikuwa anaumwa na wote tunafahamu kuwa yuko nje ya nchi kwa matibabu.
Lakini hizi ziara zake huko nje ni za kitabibu[ ninaona alichokuwa anakifanya mbowe kinajirudia]
2. Jee kanuni za bunge zinasema nini kuhusu hili?
3. Jee hizo safari ambazo ndugu TL anazifanya zimeidhinishwa na nani?
4. Jee ni namna gani mbunge anaweza kupoteza ubunge?
Mbona haki yake ambayo iipo kwa mujibu wa sheria za Bunge, kupatiwa matibabu ndani ya nchi na nje ya nchi, hamjampa??

Hizo zote ni ishara ya namna mnavyomchukia Mbunge Tundu Lissu

Lakini yeye mwenyewe amesema kuwa mmejaribu kumpiga risasi zaidi ya 30 kwa lengo la kumuua, IMESHINDIKANA

Mnajaribu kumvua ubunge kwa hila nayo ITASHINDIKANA

Mungu yupo na Tundu Lissu na ataendelea kumlinda na watesi wake
 
Tatizo la makamada wa Ufipa ni uwezo ndogo wa kufikiri na kuelewa mambo kwa marefu na mapana badala ya kujiaminisha hata kisichokuwepo [hewa]. Eti BBC HardTalk imetoa mwaliko kwa JPM kufanya interview, this is ridiculous! BBC haiendeshwi hivyo, lest ingekuwa imepoteza integrity kitambo sana. Eti watazamaji wa Hardtalk wanaokadiriwa kufikia milioni 350 duniani kote ni wafuasi wa Lissu [sick]. Who cares mambo ya mtaa wa Ufipa? Pengine tujue kuwa kati ya watazamaji hao, ni 0.0001% tu ndio wanaojua na kufuatilia siasa za Tanzania, achilia mbali kushabikia siasa za Ufipa! Climax ya Siasa ni uchaguzi, sasa ni wangapi kati ya hao watazamaji milioni 350 ni potential voters kwenye chaguzi za Tanzania [2020]? Au niulize kwa njia nyingine, ni Watanzania wangapi, wapiga kura, mashabiki wa Ufipa wanaojua Kiingereza waliotazama HardTalk na kisha wakatoa approval rating ya juu kwa Tundu Lissu? Men think correctly!

Secondly, makamanda hata hawajui kuwa Lissu is nothing before a state president whose policy decisions change entire business, social and economic landscape of not only Tanzanian but also global entities with connections in Tanzania. Ukitaka ku-deal na ku-vanquish serikali iliyopo madarakani unatakiwa kuwa makini sana. Siyo reckless actions au janja-janja kama za akina Mbowe. Hutakiwi kutoa na kuwapa kisingizio chochote cha kisheria kwa serikali unayopambana nayo. Bunge halijasema halitambui Tundu Lissu kupigwa risasi, kuumizwa na kupelekwa hospitalini - Dodoma NH, Nairobi NH na hatimaye Brussels. Bunge linasema kuna viashiria kuonesha kuwa Tundu Lissu amepona na kwamba muda huu anatakiwa kuwa hapa nchini, isipokuwa kwa taarifa za kitabibu. Hili ni suala la kisheria kwamba madakatari wake waoneshe kuwa Tundu Lissu anastahili kuendelea kuwa hospitalini nje ya nchi kwa matibabu. Na iwapo Tundu Lissu bado anaumwa basi hatatarajiwa kwenda excursions kama alivyofanya juzi BBC. Kwa common sense tu ni kuwa mgonjwa hatarajiwi kwenye excursions isipokuwa akiwa amepona. Lest Lissu will be considered as having absconded the parliament!

Waswahli husema ndege mjanja hunaswa na tundu bovu Mbowe tayari anajua maana na methali hii Tundu Lissu asirudie kosa hili atajuta na kusaga meno.
Yaani kwa sababu ya yeye kuwa London kuongea na BBC basi ni medically fit kurejea kazini Tz. Mbona Kenya aliongea na waandishi wa habari hamkusema he is fit to come back home.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani unitukane hadharani na majanga uniletee katika serikali yangu, watu wanaopenda uongozi wangu wakubomoe, haya hata utaratibu Wa rufaa hufuati ety unataka nikusaidie matibabu yako... What a shame???? Ukiona umeshika makali na bado ni kiburi kiasi cha kuona Wazungu unaowatetea watakusaidia its fine ila kama muungwana AJITATHMINI KABLA HAJAROPOKA HUKO INTERNATIONALI

Sent using Jamii Forums mobile app
Mmeshavimbiwa madaraka mpaka mnaita 'serikali yangu'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ningelikua lissu ningeacha tu Ndugai anifute kama Mbunge wa Jimbo lango. Ubunge sio bora sana kama Uhai wangu ambao ukienda haurudi!

Ndugai anaagizwa toka juu na ni criticism

Sent from my SM-J530F using Tapatalk
 
Shida mnaendeshwa na mihemko. Rais wa nchi akamjibu lisu huko London hahahahahahah. Hivi unafikir Rais ni kiongoz wa kijiwe cha kahawa?

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
Zile ni tuhuma nzito zinahitaji kujibiwa, kidiplomasia ile ni damage kubwa sana. Ni zaidi ya kufungua tawi la CRDB wilayani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona haki yake ambayo iipo kwa mujibu wa sheria za Bunge, kupatiwa matibabu ndani ya nchi na nje ya nchi, hamjampa??

Hizo zote ni ishara ya namna mnavyomchukia Mbunge Tundu Lissu

Lakini yeye mwenyewe amesema kuwa mmejaribu kumpiga risasi zaidi ya 30 kwa lengo la kumuua, IMESHINDIKANA

Mnajaribu kumvua ubunge kwa hila nayo ITASHINDIKANA

Mungu yupo na Tundu Lissu na ataendelea kumlinda na watesi wake
Hakuna kitu kibaya kama kupenda maana hata matumizi ya logic yanakuwa hayafai.
Nijuavyo mimi hakuna kitu kibaya kama kufanya maamuzi kwa kutumia 'emotions' na hilo ndilo tatizo linalotukwamisha kuzungumzia malipo ya gharama za matibabu ya mh. TL.
Nijuavyo mimi[layman] and i stand corrected.
Ni kwamba mara baada ya tukio la shambulio hilo, mheshimiwa alipelekwa kwenye hospitali ya Dodoma[Rufaa] ambako alipatiwa matibabu ya dharura kabla ya kupelekwa Muhimbili [hili lilishauriwa na jopo la madaktari hapo dodoma].
Kwa bahati mbaya, sura ya suala hili lilibadilishwa na kuwa la kisiasa pale ambapo wanasiasa walipoingilia na kuamua kuwa watakodi ndege kumpeleka Nairobi ambako waliamini kuwa huko angepata matibabu mazuri na ya usalama zaidi na kwamba wangegharimia matibabu hayo.
Kwa upande mwingine, serikali ina utaratibu wake ambapo hospitali yenye uwezo wa kupendekeza na kupeleka wagonjwa kwenye hospitali nje ya nchi ni muhimbili hospital pekee.
Nionavyo mimi, taratibu za malipo ya serikali kwa matibabu ya mheshimiwa nje ya nchi yanakuwa magumu kwani muidhinishaji wa kwanza anapaswa kuwa muhimbili kabla ya wizara ya afya, bunge na hazina kuhusika.
Matumizi yoyote yale nje ya taratibu zilizowekwa zingezua Query ambapo mwisho wa siku CAG angehusika
 
Back
Top Bottom