Spika Ndugai akiambatana na Wabunge 10 wafika Bandarini Dar mapema leo kugagua Kontena zilizozuiliwa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Spika Ndugai akiwa na wabunge 10, amefuatana na waandishi hadi Bandari ya Dar, bado haijajulikana ziara hiyo inalenga nini.

fr.png

UPDATES: Spika wa Bunge, Job Ndugai akipokea maelezo kutoka kwa watendaji wa bandari kwenye kontena.

Spika Ndugai: Ndugu waandishi mnavyoona hadi Spika nimekuja hapa, jua kuna sintofahamu nyingi.

Spika Ndugai: Baada ya kuona suala hili la makontena nikaona nije ili kujua ukweli. Hili si jambo dogo.Tutaona jinsi gani kuishauri Serikali

Spika Ndugai: Namshukuru Rais Magufuli kuja huku bandarini na ya kuyang'amua makontena 20 ya mchanga.

Spika Ndugai: Kama Bunge, tutaunda timu ya kuja kutathimini biashara hii ya mchanga na madini kwa ujumla.

Spika Ndugai: Timu hii pia itaangazia hatua za awali toka uchimbaji wa madini hapa nchini hadi huko nje tunapoenda kuyauza.

Spika Ndugai: Tutapenda kujua biashara ya madini kama taifa tunafaidikaje?

cds.png
 
View attachment 487108
Hakuna jipya, wanataka kututoa koromije kwa bashite
 
Natamani timu zinazoundwa wangepewa hii kazi wanajeshi(wavae kiraia) au usalama ili wabunge wawe na majukumu ya kitaifa tu.(just thinking loud)
 
Kelele zote zile kumbe kick ilikuwa ni bandarini.....

Ladha ya bia ya 1 hadi ya 6..

Kwa wanywaji wazuri wa bia,

chupa ya kwanza huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza koo... Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.

Chupa ya pili kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihi....

Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wachezaji wa Yanga bila kukosea.. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.

Chupa ya tatu huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sana.... Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokeza.....
ya nne huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikia..... bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.

Bia ya tano ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipu......na kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; ‘Mi sipendwi mpaka leo sijaolewa’ au ‘ Mume wangu sijui yukoje hanijali’

Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.

Kuanzia bia ya sita na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana. ....... ...Kuna watu husema ukilewa ndipo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamueleza ukweli jinsi alivyo fala na hajui kuendesha kampuni.

Au unasema ukweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Kimsingi uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao pia uchumba unaweza kuvunjika.......

Imetolewa na
*BALOZIWA VIROBA NCHINI
 
Natamani timu zinazoundwa wangepewa hii kazi wanajeshi(wavae kiraia) au usalama ili wabunge wawe na majukumu ya kitaifa tu.(just thinking loud)

Wanajeshi kazi yao ni kulinda mipaka ya Nchi.Bunge ndio lina kazi za namna hiyo.
 
Hii Ni Kiki Tu ya mjomba magu ILA front page ya kesho Ni nay WA mitego atiwa akamatwa Na polisi Moro kisa nyimbo yake ya wapo
Huwezi kuzuia biashara binafsi zisiuzwe and waliona Kiki ya airport haitauza
 
Tuliaminishwa miaka ya nyuma kwamba ni sawa mchanga kusafirishwa tena kwa ulinzi mkali pamoja na watu kupinga. Kuna jipya?
 
Back
Top Bottom