johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,897
- 141,829
Spika wa bunge mh Ndugai amesema anakerwa sana na kitendo cha Serikali kuchukua fedha za halmashauri bila taarifa na kwenda kuzitumia huku miradi ikidorora.
Ndugai amesema haoni mantiki ya Serikali kuchukua fedha ambazo hazijatumika kila ifikapo June 10 bila kujali kwamba kuna miradi inakuwa bado haijakamilika.
Spika Ndugai amekumbusha kuwa nchi za wenzetu wakati wa kampeni huwa wanaahidu kuendesha " less government" tofauti na sisi ambapo serikali imebana kila mahali kiasi cha kuwafanya wananchi wakose hata nafasi ya kupumua.
" Yaani kila upande unaogeuka unakutana na serikali watu wanashindwa hata kujiachia achia" amesisitiza Ndugai.
Chanzo: ITV habari