Spika Ndugai akerwa na tabia ya Serikali kuchukua fedha za halmashauri bila taarifa, ataka mfumo wa " less government" utumike nchini!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,571
Spika wa bunge mh Ndugai amesema anakerwa sana na kitendo cha Serikali kuchukua fedha za halmashauri bila taarifa na kwenda kuzitumia huku miradi ikidorora.

Ndugai amesema haoni mantiki ya Serikali kuchukua fedha ambazo hazijatumika kila ifikapo June 10 bila kujali kwamba kuna miradi inakuwa bado haijakamilika.

Spika Ndugai amekumbusha kuwa nchi za wenzetu wakati wa kampeni huwa wanaahidu kuendesha " less government" tofauti na sisi ambapo serikali imebana kila mahali kiasi cha kuwafanya wananchi wakose hata nafasi ya kupumua.

" Yaani kila upande unaogeuka unakutana na serikali watu wanashindwa hata kujiachia achia" amesisitiza Ndugai.

Chanzo: ITV habari
 
Spika wa bunge mh Ndugai amesema anakerwa sana na kitendo cha serikali kuchukua fedha za halmashauri bila taarifa na kwenda kuzitumia huku miradi ikidorora...
Kuwa jali wananchi kunahitaji moyo wa ujasiri sawa na chuma, kwani wengi wameshindwa hata kutokuwajali kiasi cha kuwageuza wanyonge.
 
Safi Job kuambiwa unademka ilikua dharau asee. Sasa waombe poo wao. Hasira za mgogo sio mchezo
 
Mpinzani wa kweli kwa sasa amebaki ndugai tu, Chadema wanachekelea zile biashara zao haramu kwa sasa zinakwenda poa tu,
 
Bwashe sasa ni wazi Ndugai ameamua kuziba ombwe la kukosekana kwa wabunge wa upinzani bungeni, amekuwa mpinzani wa waziwazi wa Serikali ya Rais SSH. Ilikuwaje akawa mtiifu full kwa meko na sasa mpinzani underground wa SSH? Full utapeli.
 
Kuhusu bwawa la Bagamoyo mjomba amemsaliti baba, mama awe muangalifu ma kaka yake.
 
Tangu mwendazake aondoke job anaweweseka hovyo hovyo

Yeye anawalipa covic-19 kutoka Taratibu, katiba na sheria ipi?

Huo upuuzi si yeye ndio alikuwa anakubaliana na mwendazake kwa madudu yote.

Job atakuwa na matatizo makubwa.
Ila Jiwe sijui alikuwa ana akili kichwani ama matope
 
Bwashe sasa ni wazi Ndugai ameamua kuziba ombwe la kukosekana kwa wabunge wa upinzani bungeni, amekuwa mpinzani wa waziwazi wa Serikali ya Rais SSH. Ilikuwaje akawa mtiifu full kwa meko na sasa mpinzani underground wa SSH? Full utapeli.
Anakuaga na mtindo wa kuitisha serikali toka kitambo enzi za Mwendazake Kisha anaitwa na kueka Mambo sawa. Maza Hana iyo mimambo ye anadili nae mdogo mdogo ashamuondolea Yule katibu wa bunge Kigaigai kamueka wake. Anamnyoosha tu
 
Kumbe! Ukute ndo maana amekuwa bitter sana baada ya Katibu wake aliyepewa na meko kuondolewa
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom