Spika Ndugai akerwa na tabia ya Serikali kuchukua fedha za halmashauri bila taarifa, ataka mfumo wa " less government" utumike nchini!

Anakuaga na mtindo wa kuitisha serikali toka kitambo enzi za Mwendazake Kisha anaitwa na kueka Mambo sawa. Maza Hana iyo mimambo ye anadili nae mdogo mdogo ashamuondolea Yule katibu wa bunge Kigaigai kamueka wake. Anamnyoosha tu
Si kweli.
Lini aliwahi kuitisha serikali ya JIWE?
 
Spika wa bunge mh Ndugai amesema anakerwa sana na kitendo cha serikali kuchukua fedha za halmashauri bila taarifa na kwenda kuzitumia huku miradi ikidorora.

Ndugai amesema haoni mantiki ya serikali kuchukua fedha ambazo hazijatumika kila ifikapo June 10 bila kujali kwamba kuna miradi inakuwa bado haijakamilika.

Spika Ndugai amekumbusha kuwa nchi za wenzetu wakati wa kampeni huwa wanaahidu kuendesha " less government" tofauti na sisi ambapo serikali imebana kila mahali kiasi cha kuwafanya wananchi wakose hata nafasi ya kupumua.

" Yaani kila upande unaogeuka unakutana na serikali watu wanashindwa hata kujiachia achia" amesisitiza Ndugai.

Source: ITV habari!
Kama nilimuelewa vizuri alikuwa anaunga mkono hoja iliyoletwa na mbunge mmoja kuhusu mchezo wa serikali kupelekea halmashauri mapesa kibao ya mradi muda mfupi kabla ya mwaka wa fedha kuisha, halafu kuzichukua tena kwa kisingizio kuwa halmashauri imeshindwa kutumia!
Kwa mfano, halmashauri imeomba bilioni 1 kwa ajili ya kujenga kituo cha afya. Wanazunguka mwaka mzima bila mafanikio lakini mwishoni mwa mwezi wa tano wana dumbukiziwa bilioni 1 kwa ajili ya mradi. Kwa maana nyingine wanatakiwa wampate mkandarasi ambae atakamilisha ujenzi ndani ya mwezi mmoja kwa sababu hamna malipo yatakayoidhinishwa baada ya tarehe 30 saa sita usiku. Amesema hiyo sio haki maana mtoaji alipaswa kujua kuwa mradi hauwezi kukamilika katika muda huo.

Amandla...
 
Back
Top Bottom