Spika Ndugai ahoji shughuli za Serikali kurudi Dar, ataka kujua ni nani anayedhibiti matumizi ya Serikali kwa sasa

Jaminati

Senior Member
Feb 18, 2021
178
250
Spika wa bunge mh Job Ndugai leo wakati wa kuahirisha shughuli za Bunge, amewahoji mawaziri ni kwa nini kwa sasa wameamua kufanyia makongamano, warsha na semina nyingi Dar es Salaam na kuacha kufanyia Dodoma ambayo ni makao makuu ya nchi.

Ndugai ametaka kujua ni nani anayecontrol expanditure za serikali kwa sasa kwani kila mawaziri wanapofanya hizo safari za Dar wanalipana posho za kutisha pamoja na wasaidizi wao huku wakiwaacha wananchi masikini wakiwa hoi hoe hae bila huduma muhimu za jamii.

View attachment 1932327
Na yy atuambie ni sheria gan inayowatambua wale wabunge 19 wanaondelea kutafuna kodi zetu wakati walishatimuliwa kwenye chama chao
 
init

Member
Mar 22, 2021
23
45
Magu alikurupuka kuhamia Dodoma
😂 kwamba unachojaribu kusema ni kwamba Mh Dr Magufuli aliamka na kuamua kuhusu kuanza kuamia Dodoma sio😁? . FYI Mpango huo ulikuwepo tangu enzi ya Mwalimu, inaoneka hata hilo hufahamu na Marais wengi waliofuata walitakiwa kulifanyia utekelezaji na hawakufanya hivyo ikawa maandiko kwamba serikali ina nia ya kuhamia Dodoma pasipo utekelezaji wowote licha ya swala hilo kuwa na maslahi kiuchumi ambayo mojawapo ilikuwa kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali kwani wabunge na mawaziri ofisi na baadhi ya maswala Dar bunge Dodoma na usafiri ni wa serikali , Mtekelezaji hakukubali kulaza zege kwani hata baadhi ya tasisi Dar zmepanga na nadhani unafahamu au hata kama ufahamu umewahi sikia gharama za kupanga jengo kwaajili ya Ofisi katika jiji hilo na pia yeye kama alivyojitanabaisha wazi kwetu watanzania hakupenda matumizi yasiyo ya lazima kwa serikali.
 
citizensindevelopment18

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
963
500
Spika wa bunge mh Job Ndugai leo wakati wa kuahirisha shughuli za Bunge, amewahoji mawaziri ni kwa nini kwa sasa wameamua kufanyia makongamano, warsha na semina nyingi Dar es Salaam na kuacha kufanyia Dodoma ambayo ni makao makuu ya nchi.

Ndugai ametaka kujua ni nani anayecontrol expanditure za serikali kwa sasa kwani kila mawaziri wanapofanya hizo safari za Dar wanalipana posho za kutisha pamoja na wasaidizi wao huku wakiwaacha wananchi masikini wakiwa hoi hoe hae bila huduma muhimu za jamii.

View attachment 1932327
Inasikitisha sana. Lakini naona mawaziri wanaiga kichwa. Kama mkuu anafanya nusu ya kazi Dar basi na mawziri wanafuata. Hivi Ikulu ya Dodoma haina ubora? Hali hiyo inatia simanzi sana kwani matumizi yanazidi mapato. Ndugai endelea kutafuta majibu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom