Spika Ndugai afunguliwa kesi ya kikatiba kwa kumtambua Mwambe kuwa Mbunge halali licha ya kujivua uanachama Chadema

Mwambe mwenyewe alijua kwamba alishajivua ubunge baada ya kuhama chama kilichomdhamini ndiyo maana hakurudi bungeni,mpaka alipoitwa na Ndungai.
Chadema walimwandikia spika wakimjulisha kuwa Mwambe sio mwanachama wao kwa vile amejiunga na CCM,lakini Ndungai akasema haitambui kwa vile haina viambatanisho ilihali alitambua barua kama hizo alizoandikiwa kuhusu wabunge wa Chadema waliounga mkono juhudi za mkulu.

Sent using Jamii Forums mobile app
... umeeleza vizuri! Na hapo ndipo tatizo la msingi lilipo; uamuzi wa mwisho kwamba fulani ubunge wake umefikia tamati kwa evidence hizi na hizi ni nani? Those powers are vested in the Speaker ambaye tayari alishakataa viambatisho kama ulivyoeleza na kauli yake ni ya mwisho kwenye hilo.

Kwa mtazamo wangu kwa kuzingatia maelzo yako ni kwamba Spika alitakiwa ashtakiwe kwa "double standards" na sio kuvunja Katiba; kavunja vipi katiba wakati hakuwahi (kwa mamlaka aliyo nayo na ndiye peke yake mwenye mamlaka hayo) kutangaza kwamba fulani sio mbunge?
 
Wasomi wa Tz ni kama nyani tu,ila hawana mkia.

Mtu na akili zake anajua wazi kwamba mtu kujivua uanachama wa chama cha siasa anakosa sifa ya kuwa mbunge,unalazimishaje aendelee kuwa mbunge ili hali hana chama kilichomdhamini.
Tulikuta msomi uchwara itakuwa ni tusi kwako?

Watu wanaumwa corona,wewe unapima wanyama na matunda,tukupe jina gani linalolingana na sifa yako?

Tukikosea kupewa uhuru mapema,ilikuwa tupate uhuru mwaka 2030

Sent using Jamii Forums mobile app
... hivi "kujivua uanachama" maana yake ni nini hasa? Ni kusimama jukwaani na kuwatangazia wasikilizaji "jamaniiii; nimejivua uanachama"? Siwezi kutamka hivyo na bado kadi yangu nikawa nayo tena kadi hai? Siwezi kutamka hivyo halafu mahali pengine nikasema "jamaniii mimi ni mwanachama bado"? Kauli ipi izingatiwe?

Bahati mbaya Katiba haielezi process nzima ya "kujivua uanachama" (sio ubunge) ili ikamilike nini kifanyike! Ila ili ubunge wa mbunge ufikie mwisho ni lazima Spika narudia tena Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atoe tangazo rasmi na hapo narudia tena hapo ndipo mtihani wa hii kesi ulipo! white wizard.
 
Ina maana wewe unajua sana sheria za bunge kuliko spika wa bunge?
Kuwa spika wa Bunge haina maana una akili kuliko watu wote! Au hujui huwa anapatikanaje?

Kwa akili hiyo ya mihemko ni kweli bora ufie huko huko kwa mabeberu.
Huku tunahitaji watu makini wasio na mihemko.
Nyinyi mlio makini mbona mnahangaika na Sukari mwaka 2020! mtafikia kweli azma yenu ya Uchumi wa viwanda kama tu vya sukari vimewashinda?

Mimi akili zangu za mihemko sawa wewe akili zako ni tepetepe tena za kurudi nyuma kwa sababu unafikiri Spika wa Bunge ana akili kukuzidi na watu wengine wote.
 
Maamuzi ya spika kumuita mwambe ni pale alipoona udhaifu wa vyama kutofata sheria na kanuni, hapo anawakumbusha wasome katiba zao vizuri wazielewe wasiwe wanasubiri huruma,
Naimani wewe ni mtu mzima na unajitambua vizuri tu huna ujinga mkubwa kichwani mwako.
.
Madiwani wa Chadema wanaohama chama kwa kuita Camera za TBC kila kukicha huwa Chama kinaandika Barua kwenye Halmashauri zao kuwa wao si wanachama wa chama kilichowapa dhamana ya uongozi au chama huwa kinafanya nini?
.
Au spika huwa ni msimamizi wa vyama vya siasa na anawataka wafanye moja mbili tatu wasipofanya anachukua maamuuzi yake?
.
Nikupe mfano mimi ni mwanachama wa Chadema na ni mwenyekiti wa kijiji kilichopo Wilaya ya Maswa, leo hii nihame niende CCM bila kuandika barua CHADEMA wala kokote niitishe tu press nitangaze kuhama, kisha nichukue kadi ya ccm.

Alafu niendelee kuhudhuria ofisini na kutekeleza majukumu mengine ya wadhifa nilioupata kwa dhamana ya CHADEMA kumbuka CCM ndio wamenipa ruhusa ya kurudi ofisini wewe utafanya nini? Au utaenda mahakamani ambako Jaji anaifanyia kazi CCM? au utaenda kwa msajili?

linapotokea jambo wawe wanachukua hatua mapema, kumbuka Pf Ripumba na CUF.
Ukiwa upo upande wa chama tawala kwenye nchi za kimasikini kama Tanzania hata uibe mabilioni, uuze unga, ua watu hufanywi lolote.

Msajili wa vyama vya siasa anatafutwa na kuteuliwa na Rais, Jaji anatafutwa na kuteuliwa na Rais, IGP anatafutwa na kuteuliwa na Rais, CDF, CGP wotee, RC, DC kote Rais anatafuta na kuteua yeye.

Haya kaamua Mwambe arudi bungeni wewe utafanya nini?
Kaamua ukae ndani hadi unyooke we utafanya nini?
Kaamua Lipumba arudi chamani wewe utafanya nini?
.
Kenya Rais kazi yake ni ku-point alafu Bunge linaweza kukubali au likamkataa!

Mathalani CDF Samson Mwathethe amestaafu akam-point CDF mpya Bunge limempitisha!
 
Aisee wewe jamaa unanichosha, tumieni katiba zenu na ya nchi na za vyama vya siasa, vingimevyo mtaendelea kushindwa tu.
Chukuweni hatua kwa wakati,

hayo ya madiwani ndo nasema msizoee kuishi kwa mazoea dunia inabadilika.
 
Siyo aibu tu na hasira pia. Je angekuwa ni Mbunge wa ccm Ndugai angefanya huu upuuzi??

Sent using Jamii Forums mobile app

Yote haya yanafanyika kwa kutumia ubabe na Jeuri ya Magufuli tu. Hivi mtu akiua mchana kweupe kwa KUMPIGA mtu gongo kichwani au risasi kama alivofanya Ndugai kwa mwana CCM mwenzake Mahakama itasema haina document za ushahidi?

Nimesikia Ayubu akidai hatambui nyaraka za Cecilia Mwambe kujiuzulu Uanachama wa CHADEMA na kujiunga CCM.

Sasa Kama yeye ni MWAMBA hayo maneno akayasemee Mahakamani. Ushahidi usiotiliwa Shaka na dunia nzima ni huu:
  1. Picha za video, mnato na sauti Mwambe akijitoa Uanachama CHADEMA.
  2. Picha za video, mnato na sauti Cecil Mwambe akikabidhiwa Kadi ya Mwanachama wa CCM.

Kama Mahakama Kuu itakataa ushahidi kama huo usiotiliwa Shaka basi Tanzania kama Taifa mfumo wa Judiciary utakuwa umeoza isivo kawaida.
 
Yote haya yanafanyike kwa kutumia ubabe tu. Hivi mtu akiua mchana kweupe kwa KUMPIGA mtu gongo kichwani au risasi kama alivofanya Ndugai kwa mwana CCM mwenzake Mahakama itasema haina document za ushahidi?

Nimesikia Ayubu akidai hatambui nyaraka za Cecilia Mwambe kujiuzulu Uanachama wa CHADEMA.

Sasa Kama yeye ni MWAMBA hayo maneno akayasemee Mahakamani. Ushahidi usiotiliwa Shaka na dunia nzima ni huu:
  1. Picha za video, mnato na sauti Mwambe akijitoa Uanachama CHADEMA.
  2. Picha za video, mnato na sauti Cecil Mwambe akikabidhiwa Kadi ya Mwanachama wa CCM.

Kama Mahakama Kuu itakataa ushahidi kama huo usiotiliwa Shaka basi Tanzania kama Taifa mfumo wa Judiciary utakuwa umeoza isivo kawaida.
Kama tujuavyo Mahakama zetu pamoja na Bunge letu yako mfukoni kwa Mmiliki wa ule Mhimili uliojichimbia chini zaidi ya mingine. Hivyo shauri lile litapigwa dana dana hadi Bunge litakapovunjwa hivi karibuni.

Nchi imeoza kila kona harufu. Na aliyetufikisha hapa tulipo ni mtu mmoja tuu asiye na haya usoni. Lakini siku yake yaja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yote haya yanafanyika kwa kutumia ubabe na Jeuri ya Magufuli tu. Hivi mtu akiua mchana kweupe kwa KUMPIGA mtu gongo kichwani au risasi kama alivofanya Ndugai kwa mwana CCM mwenzake Mahakama itasema haina document za ushahidi?

Nimesikia Ayubu akidai hatambui nyaraka za Cecilia Mwambe kujiuzulu Uanachama wa CHADEMA na kujiunga CCM.

Sasa Kama yeye ni MWAMBA hayo maneno akayasemee Mahakamani. Ushahidi usiotiliwa Shaka na dunia nzima ni huu:
  1. Picha za video, mnato na sauti Mwambe akijitoa Uanachama CHADEMA.
  2. Picha za video, mnato na sauti Cecil Mwambe akikabidhiwa Kadi ya Mwanachama wa CCM.

Kama Mahakama Kuu itakataa ushahidi kama huo usiotiliwa Shaka basi Tanzania kama Taifa mfumo wa Judiciary utakuwa umeoza isivo kawaida.

Hii kesi itakuwa tamu sana kuifutilia tokea mwanzo hadi kuhitimishwa kwake!
Huu utakuwa mtego mkali sana kwa Katiba ya Tanzania lakini pia mfumo wa Mahakama zetu Kama zinafanya kazi kwa weledi na Haki.
 
Hii sio kesi ni upuuzi mtupu kusumbua Mahakama Kwa takataka kama hii, inapaswa itupiliwe mbali kabisa!!
 
... hivi "kujivua uanachama" maana yake ni nini hasa? Ni kusimama jukwaani na kuwatangazia wasikilizaji "jamaniiii; nimejivua uanachama"? Siwezi kutamka hivyo na bado kadi yangu nikawa nayo tena kadi hai? Siwezi kutamka hivyo halafu mahali pengine nikasema "jamaniii mimi ni mwanachama bado"? Kauli ipi izingatiwe?

Bahati mbaya Katiba haielezi process nzima ya "kujivua uanachama" (sio ubunge) ili ikamilike nini kifanyike! Ila ili ubunge wa mbunge ufikie mwisho ni lazima Spika narudia tena Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atoe tangazo rasmi na hapo narudia tena hapo ndipo mtihani wa hii kesi ulipo! white wizard.

Acha propaganda za kijinga halo!
Kumbe kujiunga na kujiuzulu Uanachama Katiba iko kimya?

Kama Katiba iko kimya kuhusu Wanachama wanaoingia Bungeni kwa tiketi ya vyama vyao wakiwa Wabunge basi kuna mapungufu makubwa Sana kwenye Katiba yetu.

Kwa lugha nyingine kuanzia LEO WABUNGE WOTE SIYO WANACHAMA WA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA NA KATIBA IFUMULIWE NA KUFANYIWA MAREKEBISHO YA KUWA NA WAGOMBEA BINAFSI.
 
... kugombea kupitia chama fulani kuna documents zinazothibitisha udhamini wa chama and those are recognized officially. Labda utuambie wewe kama mtu anapojivua uanachama kuna fomu au nyaraka nyingine anazotakiwa kujaza kuthibitisha hilo! Kama zipo na mhusika alitimiza utaratibu huo well and good, ushindi upo kwa wafungua kesi kinyume cha hapo ni kujilisha matumaini hewa.
 
Nawapongeza sana walioamua kufungua kesi hii! ....Hata kama mahakama itatoa yale maamuzi ya kimazoea kama tulioyashuhudia kwenye kesi za CUF dhidi ya Prof. Lipumba, Lakini bado upinzani watakuwa wameudhirishia umma namna walivyo makini katika kuhoji na kupambana na uvunjaji wa katiba yetu! Eidha ushindi wao utasaidia kuweka adabu kwenye kiti cha Spika ambacho kinaonekana wazi kuwa kinahitaji mwekezaji kutoka nje , lakini sio spika wa sasa!
 
Back
Top Bottom