Lituye
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 1,862
- 5,679
Yaani ukistaajabu ya Kihiyo utayaona ya bwana Ngugai. Jioni hii nimewasha TV yangu nakutana na tangazo ITV likisema Usikose kuangalia kipindi maalumu siku ya Alhamisi saa tatu usiku cha mafanikio ya Bunge la AWAMU ya Tano.
Nilicho baini kama huyu jamaa kuwa kweli ile kauli yake kuwa analo faili kule Milembe ni mahojiano mafupi yaliyo rekodiwa ktk Tangazo hilo yakimnukuu Ngugai na baadhi ya wabunge kama Mbatia.
Ngugai anaeleza mafanikio makubwa sana yaliyo patikana Katika Bunge la AWAMU ya Tano ni kuwanunulia Wabunge IPAD na kudai kuwa wamekuwa Bunge la kisasa kabisa hapa Duniani.
Hivi kweli Ngugai na wenzie wanajua mahitaji ya wananchi ?
Katika nchi ambayo wanafunzi wamefaulu wanakosa nafasi kidato cha kwanza. Serikali yake inakazana kununua Ndege tena kwa keshi.
Katika nchi ambayo watu wanatekwa na kuuwa, watu wanabambikiwa kesi za kuhujumu uchumi na utakatishaji Pesa. Watu wanapigwa risasi milangoni mwao na wanafunzi wa vyuo vikuu wanakosa mikopo.
Katika nchi ambayo Bunge linajadili mambo ya wananchi likiwa halioneshwi moja kwa moja. Limezuiwa kuoneshwa na muhimili wa serikali kwa kibri tuu.
Katika nchi ambayo Bunge linatunga sheria za kukandamiza raia wake na upinzani, Ngugai anasema watanzania tujivunie kuwa Wabunge wamenunuliwa IPAD.
Hii ni Kejeli ya kiwango cha juu kabisaa inaweza ikafika kiwango cha standard gauge. Hawa ndio aina ya wabunge tulio wachagua wakaisimamie serikali na kuishauri.
Tusifanye tena mzaha ndugu zangu October mwaka huu katika box la kupigia kura. Watu aina ya Ngugai wabakie tuu kulea wajukuu.
Asante sana.