Spika Ndugai adai hajapata barua ya kujiuzulu kwa Nyalandu, anamtambua kama mbunge wa CCM. Adai akija Bungeni atampokea

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Spika wa bunge la Tanzania akihojiwa na kituo cha tv cha azam kaonekana kukerwa kwa kujiuzulu kwa mbunge Nyarandu na kudai kama spika hajapata barua rasmi ya kujiuzulu na hawezi kusema lolote na kipi kitafuata zaidi ya kusema yeye kaona kwenye tv na akiipita barua hiyo mpka ajiridhishe kuwa imeandikwa na Nyarandu.

Mtangazaji Charles Hilary alipomuuliza kipi kitafuata spika alijibu kafanya kosa inatakiwa angemwandikia katibu wa ccm kwanza kabla ya kutoka kwenye vyombo vya habari na angemwandikia na spika.

Ila ukimwona spika body language inaonyesha ana hasira na kachukia sana na anaonekana hana furaha.

Akiongea pia na EA radio amesema haya;
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amesema kitendo cha Lazro Nyalandu kujiuzulu ubunge kabla ya kumuandikia yeye barua ni umbea na kuwashwawashwa.

Job Ndugai ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio kwenye kipindi cha East Africa Breakfast, na kusema kwamba Lazaro hakupaswa kutangaza hivyo kabla ya kuhakikisha barua imemfikia.

Pamoja na hayo Spika Ndugai amewataka wabunge wengine kuacha kuwashwa washwa na kufanya mambo ambayo ameyaita ni ya umbea.

Msikilize hapa chini.

==================================

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amesisitiza kuwa bado barua ya kujiuzulu nafasi ya ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu haijafi ka rasmi ofi sini kwake, hivyo anamtambua kiongozi huyo kuwa bado ni mbunge.

Ndugai aliyasema hayo jana alipozungumza kwa njia ya simu na gazeti hili, kuhusu kama ofisi yake imeipata barua hiyo na hatua zinazochukuliwa baada ya mbunge huyo kujiuzulu ubunge na kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Yaani haya mambo mie ninayasikia kwenu tu (waandishi wa habari) na kwenye vyombo vya habari. Sisi kama Bunge mpaka sasa hatuna rekodi yoyote ya Mheshimiwa Nyalandu kujiuzulu nafasi yake ya ubunge,” alisisitiza Ndugai.

Aidha, alionesha kushangazwa na kitendo cha Nyalandu kuchukua uamuzi kujitangaza kwa vyombo vya habari kujiuzulu nafasi yake ya ubunge na kuhama chama kabla ya kuwasilisha barua yake rasmi kwa ofisi ya Bunge.

“Kwa maana rasmi mpaka sasa (jana mchana) mimi kama Spika sitambui kujiuzulu kwa Nyalandu, na ninamtambua kuwa bado ni mbunge wa Singida Kaskazini, na hata akija katika Bunge lijalo, nitampokea kwa mikono miwili hadi pale nitakapopata rasmi barua yake,” alisisitiza.

Nyalandu juzi alitangaza mbele ya waandishi wa habari jijini Arusha, kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya chama ya CCM ikiwemo ujumbe wa Halmashauri Kuu na kukiomba Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumpokea kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa hali ya siasa nchini.

Alisema tayari amemwandikia Spika wa Bunge Ndugai, barua ya kujiuzulu nafasi yake ya ubunge aliyoitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu alipochaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2000 hadi sasa.

Kwa upande wake, Chadema kupitia Katibu wake wa Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema wako tayari kumpokea Nyalandu kwa mikono miwili kama nafsi yake itakuwa ni ya kweli, lakini endapo itakuwa na dhamira ovu atajikuta akibaki peke yake.
 
Spika wa bunge la Tanzania akihojiwa na kituo cha tv cha azam kaonekana kukerwa kwa kujiuzulu kwa mbunge Nyarandu na kudai kama spika hajapata barua rasmi ya kujiuzulu na hawezi kusema lolote na kipi kitafuata zaidi ya kusema yeye kaona kwenye tv na akiipita barua hiyo mpka ajiridhishe kuwa imeandikwa na Nyarandu.

Mtangazaji Charles Hilary alipomuuliza kipi kitafuata spika alijibu kafanya kosa inatakiwa angemwandikia katibu wa ccm kwanza kabla ya kutoka kwenye vyombo vya habari na angemwandikia na spika.

Ila ukimwona spika body language inaonyesha ana hasira na kachukia sana na anaonekana hana furaha.
Sasa akichukia itamsaidia nini eti hadi apokee barua, zile barua za wabunge wa CUF kufukuzwa hata hakuziona lakini alitoa maamuzi ya kutambua kufukuzwa kwake akiwa nje ya nchi.
 
Spika wa bunge la Tanzania akihojiwa na kituo cha tv cha azam kaonekana kukerwa kwa kujiuzulu kwa mbunge Nyarandu na kudai kama spika hajapata barua rasmi ya kujiuzulu na hawezi kusema lolote na kipi kitafuata zaidi ya kusema yeye kaona kwenye tv na akiipita barua hiyo mpka ajiridhishe kuwa imeandikwa na Nyarandu.

Mtangazaji Charles Hilary alipomuuliza kipi kitafuata spika alijibu kafanya kosa inatakiwa angemwandikia katibu wa ccm kwanza kabla ya kutoka kwenye vyombo vya habari na angemwandikia na spika.

Ila ukimwona spika body language inaonyesha ana hasira na kachukia sana na anaonekana hana furaha.
Siku hazigandi atapata tu
 
Back
Top Bottom