Spika Ndugai aahirisha Bunge na kuwataka Wabunge kuzingatia masharti ya Serikali kuhusu afya zao pia madereva wao wasikimbie hovyo

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,607
141,431
Spika wa bunge Mh. Ndugai ameahirisha vikao vya bunge hadi watakapokutana tena kwenye mkutano wa vikao vya bajeti mwezi March, 30.

Spika amewataka wabunge kuchukua tahadhari ya afya zao kulingana na miongozo inayotolewa na wizara ya afya kadhalika amewataka wabunge na madereva wao wawe makini wawapo barabarani na kuacha tabia ya kukimbia kimbia hovyo.

Mwisho, Spika Ndugai amewataka wabunge wote kukusanyika kwenye viwanja vya bunge ili kutoa heshima za mwisho kwa mbunge wa Muhambwe aliyefariki dunia kwa ajali.

Chanzo: TBC

Maendeleo hayana vyama!
 
Speed speed kisa bendera mamlaka, magari kiwango, na heshima.
 
Spika wa bunge Mh. Ndugai ameahirisha vikao vya bunge hadi watakapokutana tena kwenye mkutano wa vikao vya bajeti mwezi March, 30.

Spika amewataka wabunge kuchukua tahadhari ya afya zao kulingana na miongozo inayotolewa na wizara ya afya kadhalika amewataka wabunge na madereva wao wawe makini wawapo barabarani na kuacha tabia ya kukimbia kimbia hovyo.

Mwisho, Spika Ndugai amewataka wabunge wote kukusanyika kwenye viwanja vya bunge ili kutoa heshima za mwisho kwa mbunge wa Muhambwe aliyefariki dunia kwa ajali.

Source TBC

Maendeleo hayana vyama!
Ni jambo jema.
 
Tutaelewana tu ! Kauli hiyo ina maana halisi ikimaanisha kuhusu ugonjwa wa Corona! Mwendokasi na kuendesha hovyo haijaanza leo huko Tanzania
 
1613216499012.png

Wanajaribu kumvicha rona lakini hafichiki.
 
Arcado Ntagazwa alikuwa zamani mbunge wa Muhambwe kafariki na Nditiye ni mbunge Current wa Muhambwe kafariki at the same period. .Is it a coincidence or what? Watu wa Muhambwe kulikoni ? ushirikina or what?
 
Back
Top Bottom