Spika na Wabunge Wetu: Je Haya Mnayafahamu na Mnaridhika Nayo???? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika na Wabunge Wetu: Je Haya Mnayafahamu na Mnaridhika Nayo????

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Amanikwenu, Feb 5, 2011.

 1. A

  Amanikwenu Senior Member

  #1
  Feb 5, 2011
  Joined: Dec 1, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wiki ijayo Wabunge wetu wanaelekea Dodoma kwa ajili ya kikao chao cha kwanza baada ya uchaguzi mkuu.

  Wakati wabunge wetu wakielekea Dodoma je wanayafahamu haya

  1. Kiwango cha fedha anacholipwa Mbunge mmoja kwa mwaka ni zaidi ya fedha ambayo Serikali inatoa kama ruzuku katika kuendesha zaidi ya shule 62 kwa mwaka.

  2. Serikali 'haitoi' hata shilingi moja kama Capitation Grant kwa ajili ya kuendesha na kununua vifaa mbalimbali kama vitabu kwa shule zetu za Sekondari.

  3. Wastani wa fedha ya Capitation Grant ambayo Serikali inatoa kwa kila shule ya msingi kwa mwaka ni shilingi 2,300,000 tu.

  Mapendekezo

  1. Tunaomba fedha ya ada ya mwaka wanayolipa wanafunzi wa kutwa (20,000) na bweni (70,000) wa sekondari iwe inabaki katika akaunti ya shule badala ya kupelekwa Hazina na pia isihesabiwe kama sehemu ya capitation Grant toka Serikalini.

  2. Serikali itenge angalau asilimia 7 ya makusanyo yake ya kodi kila mwezi kwa ajili ya maendeleo ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari hapa nchini. Fedha hizi ziundiwe Mfuko Maalum ambao utawajibika kwa Bunge moja kwa moja.

  3. Capitation Grant kwa shule za msingi iongezwe kutoka shilingi 10,000 kwa mwaka kwa mwanafunzi mpaka shilingi 45,000 kwa mwaka kwa mwanafunzi. Na kwa upande wa Sekondari kiwango cha Capitation Grant kiwe shilingi 75,000 kwa mwaka kwa mwanafunzi.
   
 2. A

  Amanikwenu Senior Member

  #2
  Feb 5, 2011
  Joined: Dec 1, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni muhimu sana kama taifa tukaelewa na kukubaliana kuwa njia bora zaidi ya kuifikia kila familia na kuisaidia kupambana na umaskini ni kwa kila familia kuipatia elimu bora hasa kupitia watoto wa familia husika.
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hapa kazi bado!
   
 4. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,231
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Wasi wasi wangu ni nani mwenye ujasiri huo...hii ya posho ya wabunge inawagusa waheshimiwa moja kwa moja hivyo sitegemei jipya...mengine mawili umegusa shule tu...nadhani kuna Hospitali na mengine mengi ya kuhitaji uangalizi kwa maana pasipo afya bado mengine hayatafanikiwa!
   
 5. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kweli mkuu sio shule tu, hospitali pia zinahitaji kuangaliwa!!
   
 6. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mtumie Mwanyika na Zitto...si member hapa. au hapo unagusa maslahi yao?hahaha
   
 7. A

  Amanikwenu Senior Member

  #7
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 1, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni kweli pia suala la Afya nalo ni muhimu sana na niamini kuwa yote yanawezekana kuyatekeleza kwa pamoja. Tatizo viongozi wetu hawana dhamira na nia ya kuibadilisha na kuiendeleza nchi yetu. Jamani hali ya shule zetu inatisha kupita kiasi.
   
Loading...