Spika na wabunge warejea kutoka Misri wataka kocha wa Taifa stars mh Amunike ni dalali atimuliwe mara moja

Ni kocha mzuri sema ameingia kwenye nchi yenye maneno mengi mpaka atajuta, angekuwa kocha mbaya leo hii msingekuwa Egypt na msingeleta haya maneno kutoka huko. Chanzo ch kuboronga ni maandalizi hafifu,kuna video zilisambaa humu zikionyesha bondia wetu alivyokuwa anafanya mazoezi kwa kutumia matairi ya gari, tukasema serikali nzima ina kosa budget ya kulipia wana michezo wake gym nzuri ili wanamichezo wakajenga miili na stamina, matokeo yake ndo yale walikuwa wakisumwa wanaanguka wenyewe, hawana nguvu, miguu kama inadegedege kocha afanye nini? misingi mibovu ya michezo.

Kosa la kocha ni moja tu kwangu, kupanga watu wenye lishe duni, mabeki wafupi ambao hawakuweza kuhimili wachezaji wa Senegal, naona tutafungwa 10 za Algeria , Tanzania tunatakiwa tuje na mpango kwanza wa kuimarisha afya bora kwa watoto wetu katika ngazi za familia na mashuleni, tuanzishe programme muhimu ya lishe maziwa kuanzia majumbani, na mashuleni, shuleni iwekwe ratiba ya watoto kunywa maziwa kila siku pakiti mbili, baada ya hapo tuhamasishe michezo katika ngazi zote, baada ya hapo tuchague vijana watakao tuwakilisha vyema katika michezo mbalimbali na tuwaandae vizuri. Hatuwei kuwa na vijana legelege tukatarajia matokeo makubwa tunajidanganya, chukueni Africa mashari ,utagundua ni Tz pekee ndio tuna miili hafifu, programme zetu za lishe majumbani na mashuleni ni 0, na maandalizi yetu ya michezo ni F.

Ushauri ni wa bure, kila mtu akapitie Hotuba ya Prof Lipumba juzi katika mkutano wake Diamond jubilee akizindua sera mpya, ameeleza jinsi report za kimataifa zinaonyesha ni jinsi gani ya kuandaa watoto kwa taifa imara lijalo, Tanzania hatuchachelewa.
 
Wabunge wa ccm bana wanachekesha ile mbaya, baada ya kuona jinsi watu walivyofurahia hiyo timu kufungwa wanatafuta pa kutokea. Ukweli ni kuwa sisi hatuna uwezo wa soka na gundu lilizidi ccm walivyoanza kuweka kimbelembele kwenye hiyo timu. Ni kweli Amunike sio kocha, je ilikuwaje huo upuuzi wanaoongea sasa hawakuongea wakati timu ilipofuzu kwenda Afcon? Sisi tunajua timu iliyofungwa sio ya taifa bali ni ya ccm.
Pole Pole anasemaje?
FB_IMG_15613930537626791.jpeg
 
Aah aaah pamoja na ubove wa amonike... Ila kutoa hukumu kisa game ya senegal ni makosa kwa kweli....

Senegal si level yetu... Na kilichotokea hakuna ambayw hakukitegemea.
 
Ameingia kama Paul Makonda siyo kama mkuu wa mkoa maana Taifa stars ni tofauti na Mzizima United!
Sawa subiri AFCON ikiisha atakuja kuisifia serikali ya awamu ya 5 kwa taifa star kuchukua kombe la afcon..na wewe jiandae kwenda uwanja wa ndege kupokea kombe!
 
Busara sifuri kabisa...

Sisiemu ndio imefikisha nchi hapa ilipo, haya yote tunayovuna iwe ni kwa michezo n.k ni matokeo ya kutawaliwa na sisiemu
 
Wangesubiri mashindano yaishe ndipo watoe ushauri huo, katikati ya mashindano unaweza kuathiri morali wa kocha na wachezaji.

Ukisikia usaliti ndio kama huo.
Team bado iko vitani wao wanaleta maneno ya kike kike.

Ila wao wakiitwa DHAIFU wanachukia.

Ni ulimbukeni tu unawasumbua
 
Uganda wamekusaidieni ...Amunike kakubebeni ...mnataka nini tena ...mlitegemea muwafunge Senegal ningelitembea uchi ...kushiriki tu ni mafanikio tosha!!!
 
Taifa Stars ni sawa na ushindi dhidi ya senegal,ukizingatia kipa wetu ndio alikuwa Man Of The Match,kutokana na siku ile tulivyo pigwa Mande na COMBINE YA ULAYA

*SENEGAL SQUAD*

*Goalkeepers:*

-Abdoulaye Diallo (Rennes, France)
-Alfred Gomis (Spal, Italy)
-Edouard Mendy (Reims, France)

*Defenders:*

-Kalidou Koulibaly (Napoli, Italy)
-Moussa Wague (FC Barcelona, Spain)
-Pape Abdou Cisse (Olympiacos, Greece)
-Salif Sane (Schalke,Germany)
-Youssouf Sabaly (Bordeaux,France)
-Lamine Gassama (Goztepe, Turkey)
-Saliou Ciss (Valenciennes, France)
-Cheikhou Kouyate (Crystal Palace, England)

*Midfielders:*

-Alfred Ndiaye (Malaga, Spain)
- Santy Ngom (Nancy, France)
- Idrissa Gana Gueye (Everton, England)
-Keprin Diatta (Club Brugge, Belgium)
-Pape Alioune Ndiaye (Galatasaray, Turkey)
-Sidy Sarr (Lorient, France)
-Henri Saivet (Bursaspor, Turkey)

*Forwards:*

-Ismaila Sarr (Rennes, France)
-Keita Balde (Inter Milan, Italy)
- Mbye Niang (Rennes, France)
-Moussa Konate (Amiens, France)
-Mbaye Diagne (Galatasaray, Turkey)
- Sada Thioub (Nimes, France)
-Sadio Mane (Liverpool, England)

Mungu ibarik taifa stars .......‍♂
 
Nina imani Taifa stars sasa watapumua na Kenya tutamfunga!
Tatizo siyo kocha ni wachezaji. Ukubali ukatae mpira bado Tanzania. Watafukuza sana makocha lakini mpira bado. Huyu wanayemfukuza ndiyo huyo aliyeisadia timu mpaka imeingia AFCON. Tatizo la Tanzania kila kitu wameingia siasa na kwasasa kuna makundi mawili ya CCM na upinzani. Sasa hivi taifa stars imekuwa CCM STARS.
Uzuri timu yangu bado ipo Misri nina hakika itachukua kombe. Naishi Tanzania lakini mpaka keshokutwa siwezi kuishabikia Taifa stars, hata tukikutana nje ya nchi nitajitambulisha kama Mkenya. Usiniulize maswali. Ndiyo hivyo.
 
Back
Top Bottom