Spika Mstaafu Msekwa awapongeza CHADEMA kwa kuwafukuza uanachama wabunge waliokwenda kinyume na taratibu zao

Namhurumia sana yule dogo..wamemuingiza chaka..watu wana roo mbaya!!
 
Pius msekwa ameyasema hayo alipo hojiwa na EATV .

Anasema kwa katiba yao wamefanya jambo la maana kabisa na hakuna chama kinacho weza endekeza wanachama wasio fuata taratibu za chama chao.

Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pius Msekwa, amesema kuwa CHADEMA wako sahihi kuwafukuza wanachama wake ambao wameenda kinyume na taratibu zao kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.

Mzee Msekwa ameyabainisha hayo alipofanya mazungumza maalum na EATV&EA Radio Digital.

"Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kiko sahihi kuwafukuza wabunge wake kutoka kwenye chama hicho, hivyo mamlaka hayo wanayo kwa mujibu wa katiba ya chama" amesema Mzee Msekwa.

Hivi karibuni CHADEMA kupitia kwa Katibu wa chama hicho John Mnyika, kiliwafukuza uanachama wabunge wake wanne, akiwemo David Silinde, Anthony Komu, Wilfred Lwakatare na Joseph Selasini, baada ya kukiuka maagizo na maelekezo ya chama.
Kwani kuna watu ambao wameona sio sahihi?
 
Namhurumia sana yule dogo..wamemuingiza chaka..watu wana roo mbaya!!
Ukishatoka Chadema na kwenda kuunga mkono juhudi basi na biashara inaishia hapo,usidanganyike na kina kafulila,machali,katambi,mollel,mikwabe etc hao 2021 wanapotea kwenye ramani ya siasa!!
 
Hongera kwa chadema ila spiker ana discretionary power bungeni pia.
Umeelewa kwa nini nimekuquote mkuu? Nilikuuliza kwenye ile thread ambayo msekwa aliunga mkono uamuzi wa ndugai kuhusu CDM kuwavua uanachama wabunge wake na ukasema kwenye kanuni za bunge msekwa yuko vema, leo msekwa huyo huyo anaipongeza CDM kwa kuchukua maamuzi aliyo yapinga awali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani tangu lini chadema kuondoka kwao bungeni kulishaleta impact? watu wameshindwa kusoma alama za nyakati kwa muda wa miaka 4.5,bado wanafanya siasa zile zile
 
Umeelewa kwa nini nimekuquote mkuu? Nilikuuliza kwenye ile thread ambayo msekwa aliunga mkono uamuzi wa ndugai kuhusu CDM kuwavua uanachama wabunge wake na ukasema kwenye kanuni za bunge msekwa yuko vema, leo msekwa huyo huyo anaipongeza CDM kwa kuchukua maamuzi aliyo yapinga awali.

Sent using Jamii Forums mobile app
36803C8E-FCFB-4057-A180-B678B084BF14.jpeg
45AABDD8-FAA2-4109-BFD1-ABBFDD485A48.jpeg

Nilisema inapokuja suala la kanuni za bunge kati ya wewe na msekwa, wewe haunishawishi zaidi yake!

MSEKWA ASEMA NDUGAI YUKO SAHIHI KUKATAA MAAMUZI YA CHADEMA.

Ukisikiliza kwa makini utaona kuwa hamna mahali Msekwa alisema chadema hawako sahihi.
 
Taja kwanza makosa ya hao wabunge mliwafukuza nikushushie nondo hapa tudihamishe mjadala kwanza poa kidogo tu lete sababu hao Wa bunge kufukuzwa uanachama ni zipi be specific usiongee ohh chama kimeamua ohh wameenda kinyume na chama kivipi.Tutulie tuongee kwa utulivu leta sababu za kuwafuta uanachama wabunge wa chadema waliohudhuria vikao vya bunge
Makosa yao ni kwenda kinyume na maazimio halali ya chama. Sema kosa la Membe
 
Makosa yao ni kwenda kinyume na maazimio halali ya chama.
yepi unajua nyie chadema mnaleta ngonjera mimi ni consultant wa donors na niko very fair nimeulizwa hilo swali mna jibu au hamna ? na nimewapa link ya jamii forums waingie hata google translator kama hawawaamini translators wao

nimewaambia opposition parrty waonezi na hawana democtracy ni ka cite wabunge wa chadema waliofukuzwa uanachama kwa kuhudhuria vikao vya bunge ambavyo ni wajibu wao kuhudhuria kama wabunge
jitetetee hapa maamuzi yepi ya chama waliyokiuka hao wabunge mliowafukuza uanachama? niko serious kama consultant be also very serious to annswer because what you say will be taken seriously by donors and it will affect future your relationship not only with donors but will also affect their countries stand and views on Tanzanian opposition parties
 
Sema kosa la Membe, acha maneno mengi
 
Sema kosa la Membe, acha maneno mengi
Yeye mwenyewe Membe baada ya kuhojiwa na CCM Dodoma hakusema alipoulizwa na waandishi Wa habari akaema yalikuwa tu mazungumzo mazuri sasa kana yeye hakusema baada ya kutoka kwenye mahojiano unataka Mimi nimsemee wakati toka mahojiano Yale yeye hajawahi sema? Au Wewe alikwambia baada ya Yale mahojiano Dodoma kuwa waliongea kitu gani? Yeye hakusema Mimi ndio niseme kamuulize mwenyewe
 
CHADEMA jiongezeni, Mzee wetu Pius Msekwa ni CCM damu damu, sasa nyie mnavyofukuzana ndio furaha kwetu tupate wanachama wapya, hilo nawamegea tu. Sasa ukiwaza direct utadhania anawatetea, but sio hivyo. CDM mna vichwa panzi sana haa
 
Yeye mwenyewe Membe baada ya kuhojiwa na CCM Dodoma hakusema alipoulizwa na waandishi Wa habari akaema yalikuwa tu mazungumzo mazuri sasa kana yeye hakusema baada ya kutoka kwenye mahojiano unataka Mimi nimsemee wakati toka mahojiano Yale yeye hajawahi sema? Au Wewe alikwambia baada ya Yale mahojiano Dodoma kuwa waliongea kitu gani? Yeye hakusema Mimi ndio niseme kamuulize mwenyewe
It's clear hauna majibu kuhusu kosa la Membe. Nikusaidie tu, sheria za vyama hazina viwango sawa na za nchi. Chadema haijawafukuza ubunge, imewafukuza uanachama, sasa hayo mengine wakakate rufaa wanakojua. I rest my case
 
Kwa maneno mengine, Spika Msekwa asema Ndugai haujui atendalo na wala asemalo na anaropoka tu, kuwa ni kihiyo wa Uspika. Ila amesema maneno hayo kistaarabu!
Hivi ktk Bunge la awamu hii ya tano kuna Spika kweli?? Sidhani. Kuna mtu aliyekalia tu kile kiti kukilinda kusiwe wazi kwani Spika wa kweli yuko magogoni a.k.a. chattle.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom