Spika Mstaafu Msekwa awapongeza CHADEMA kwa kuwafukuza uanachama wabunge waliokwenda kinyume na taratibu zao

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,108
18,325
Pius msekwa ameyasema hayo alipo hojiwa na EATV .

Anasema kwa katiba yao wamefanya jambo la maana kabisa na hakuna chama kinacho weza endekeza wanachama wasio fuata taratibu za chama chao.


PIUS MSEKWA WEB.jpg

Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pius Msekwa, amesema kuwa CHADEMA wako sahihi kuwafukuza wanachama wake ambao wameenda kinyume na taratibu zao kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.

Mzee Msekwa ameyabainisha hayo alipofanya mazungumza maalum na EATV&EA Radio Digital.

"Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kiko sahihi kuwafukuza wabunge wake kutoka kwenye chama hicho, hivyo mamlaka hayo wanayo kwa mujibu wa katiba ya chama" amesema Mzee Msekwa.

Hivi karibuni CHADEMA kupitia kwa Katibu wa chama hicho John Mnyika, kiliwafukuza uanachama wabunge wake wanne, akiwemo David Silinde, Anthony Komu, Wilfred Lwakatare na Joseph Selasini, baada ya kukiuka maagizo na maelekezo ya chama.
 
Kumbe ngoja mida ya kahawa ifike wazee wa siasa waje , apongezwe vizuri
 
Back
Top Bottom