Spika: Milipuko ya mabomu Gongo la Mboto sio jambo la dharura!



WANANCHI HATUKO SALAMA TENA WALA MALI ZETU, KIIO KILA LEO NA MAYATIMA KUONGEZEKA: KWA HILI SERIKALI NZIMA IJIUZULU HATA KABLA YA MAANDAMANO
YA KUTETEA 'UHAI WA WENZETU' KUANZA KOTE NCHINI


Mheshimiwa Kikwete kama amiri jeshi mkuu ajiuzulu pamoja na serikali yake.

Yalianza na vifo vya raia kule (1) Pemba, baadaye (2) Unguja, Kisha (3) Mbagala, nako Arusha Mjini, (4) mauaji ya wakulima kule Mashamba ya mpunga kule Mabuki Mbeya na sasa (5) Gongolamboto.

Ajabu ni kwamba licha ya wananchi wengi kuuaua na mali zao kuteketea, hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kuwajibika wala kuwajibishwa serikalini. Kote ni kiburi na jeuri tu mbe ya kupotea uhai wa mtu na watoto kubaki miyatima!!!

Jukumu la msingi halijazingatiwa; kuna watu wanasinzia kwenye majukumu nyeti na sasa kutugharimu kiasi hini, wananchi hatuko salama!! Tusianze kuzungusha kiswahili hapa ni uhai umepotea kwa uzembe!!! Hawa mayatima wanahitaji sauti zetu!!

Hatutaki tena tume kwani hata kule Mbagala chombo kama hicho hakikutusaidia zaidi ya kuwapa wanasiasa na makampuni ya kibiashara kujinadi kwenye kioo cha televisheni mgongoni mwa msiba na damu kwa wengine.

Jukumu la kwanza la kuhitajika uwepo wa serikali katikati yetu NI KUHAKIKISHA USALAMA KILA MMOJA WETU NA MALI ZETU. Kwa mtaji hizi picha nilizoona, serikali nzima ya CCM ijiuzulu mara moja

Mauaji Arusha walitupuuza kana kwamba kuliuaua nzi tu. Kule kwenye mashamba ya mpunga wala hawakujishughulisha kitu kuwajibika mtu. Sasa kama kweli kuna JAMBO AMBALO KIUKWELI KABISA KINATUHITAJI KUANDAMANA MPAKA KUELEWEKE NI KATIKA KUTETEA UHAI WA WENZETU.

Kama tutaona vifo hivi kama vile ni ya 'akina wale' na kwamba sisi wengine hatuhusiki basi hapo ndipo kiama chetu kinapoanzia. Kwa vifo hivi vyote 17 taifa tumepata yatima wangapiii?????????????


Gongo1.jpg


Gongo2.jpg

_51307856_munition_ap.jpg

_51307454_bus_ap.jpg

Debris and arms were hurled across the Tanzanian of city of Dar es Salaam on Wednesday night after an accident triggered a series of explosions at Gongola Mboto military base.
_51310264_lostchildren_ap.jpg
Tanzania's Red Cross says about 200 children who lost their parents during the confusion of the blasts are being cared for at the city's stadium.

_51312030_cherehani.jpg



attachment.php
 
Kamanda lisu usiwe na wasiwasi kwani, nimekuja kuangalia hili jambo kwa makini nimegundua spika yupo sawa kwani hili jambo siyo la dharura, kwa sababu alikuwa analifahamu litatokea, anatakiwa abanwe awaeleze watanzania kwa nini hakutoa tahadhari kwa raia wanaoishi eneo hilola gongo la mboto, huku akijua mapomu yangelipuka juzi? .Na alieleze bunge taarifa hizi alizipata wapi?AKISHINDWA AJIUZULU MARA MOJA Kwani dharura nia jambo amabalo linaotkea pasipo kutegemewa. Sasa huyu mama amesema hili siiiiiiiiiiii la daharura kwa sababu alitegemea litatokea na ndiyo maana amemwambia lisu halina haja ya kulujadili KWA SABABU SI JAMBO LA DHARURA KWAKWE. Lakini kwetu siss wananchi ni ladharura kwani hatukujua kama lipo, au laja, au kuna lingine. Huyu ni killlllllllllllllllllllllllaza
Jeshi lilijua kuhusu dalili za milipuko toka saa 4 asubui,milipuko ya ukweli ikaanza saa 3 usiku. Inawezekana kwao ccm ilikuwa sio news kwao kama speaker alivosema, we never know! Waliona uvivu kuwa-allert wananchi kabla au ndio ugaidi wenyewe?
 
Spika wa bunge Anne Makinda amesema hajaridhika kwamba suala la milipuko ya mabomu iliyotokea juzi Gongo la Mboto ni la dharura na lina maslahi kwa umma na kwamba halihitaji kujadiliwa kama jambo la dharura.

Spika amesema hayo kufuatia hoja iliyotolewa na mnadhimu wa kambi ya upinzani Tundu Lissu aliyetaka kanuni itenguliwe ili jambo hilo lijadiliwe bungeni.

Mungu humfichua dhalimu kwa mambo madogo sana.....kama si jambo la dharura,
1. Kwa nini Bunge liliahirishwa jana??
2. Atuambie lilipangwa na nani,lini na kwa nini, hadi kufikia kukosa udharura!!

Akikosa haya majibu,afute kauli zake, aombe msamaha kwa Watanzania...otherwise ataishia motoni,asidhani ushirikiano wake na mafisadi Mungu anaupenda!!
 
Define Dharura katika bunge.

38A (3) Jambo linaloletwa kwa hoja chini ya Kanuni hii litahesabiwa kuwa ni jambo la dharura iwapo:-

(a) Ni wazi kabisa kwamba ni jambo la dharura;

(b) Limetokea siku hiyo au jana yake, na limeletwa bila kuchelewa;

(c) Hakutatokea fursa ya kulijadili siku za karibuni kwa njia ya
kawaida ya kushughulikia mambo ya Bunge.


STANDING ORDERS, 2004 AS AMENDED, PARLIAMENT OF TANZANIA
PROMULGATED UNDER SECTION 89(1) OF THE CONSTITUTION OF TANZANIA, THE UNITED REPUBLIC
 
jamani kwa sababu za kiusalama si sahihi kujadili hili suala bungeni,kuna siri zaweza wekwa wazi wakati wa kujibu ambazo hazipaswi kuwa wazi,si kila kitu kinajadiliwa ovyo nyie watu,lazima wafanye uchunguzi na waweke mambo sawa kwanza(hata kama lilipangwa kuna namna ya kuwasilisha jambo kwa umma na international community inachukua muda).....heeeeeee,kuna haja ya watu kusoma somo la Usalama wa nchi......yaani hamna tofauti na Kikwete ambaye jana karopoka kuwa lile lilikuwa hiyo kati ya maghala makubwa,kwa usalama wa nchi ile si sahihi na hata wakuu wameshamwambia amechemka,leo mnataka lijadiliwe bungeni???mnafikiri nyie zaidi ya ushabiki wa vyama na chuki kwa huyu mama???
Hivi wewe vifo vya watu unaona kuwa ni swala la usalama wa nchi....huwezi hata kuhoji
Report ya mbagala ikwapi, mapendekezo yalikuwa nini na action gani zimesha chukuliwa.
Usalama gani ambao rais anasema wazi wazi kuwa lile ni ghala kubwa na kuu.
 
Makinda ni sifuri ameligeuza bunge wizara ya serikali, anafanya kazi kwa maagizo ya kikwete na pinda, inatia aibu sana huyu mama. Mimi naamini mungu anasikia sauti ya wengi atatulipia hapahapa duniani.
 
Naomba muongozo wa sheria, Kama spika tumemchoka ni nini tunapaswa kufanya ili tupate anayetufaa?
 
Back
Top Bottom