Spika: Milipuko ya mabomu Gongo la Mboto sio jambo la dharura!

Tumezisikia deals za rada, helikopta na magari ya jeshi ikiwa ni ufisadi mtupu. Inawezekana kwenye procurement za hizi silaha nako kulikuwa na ufisadi, watu wakanunua mabomu yakiwa mabomu (Nikimaanisha expired bombs). Kama waliweza kununua vifaa bomu vinavyotumika kila siku kwa shughuli za jeshi, iweje washindwe kununua vitu bomu vinavyotumika wakati wa dharura.
These leaders need to come clean here.
 
Kwa hiyo wapuuzi warushe mipasho bungeni ila kujadili janga kama hili anasema sio dharura?
 
Ukweli ni upi, je ni kweli kuwa katika kipindi hihi Mhe. Kikwete kawekwa na jeshi. Katika hili, kama mkuu wa majeshi na waziri husika watashindwa kuwajibika, basi tuamini linalosemwa kuwa wanajeshi walinsaidia Kikwete kuchakachua matoke ya uchaguzi :mullet:
 
Sijui dharura kwa huyu mama aliepewa uspika kiufisadi ni nini?!! lakini pia nawalaumu/ tujilaumu sisi wenyewe Watanzania hatuwezi kuwafanya viongozi watuogope na kutekelza majukumu yao kwetu wao wanaogopa mafisadi na sio sisi wenye nchi!!

Kama ingekua nchi ingine tungemfukuza huyu mama kwenye uspika maana hafai, kwa kuandamana mpaka atoke na waziri wa ulinzi na pia mkuu wa majeshi.

alipewa uspika kiufisadi au waliona ana K...
 
Spika wa bunge Anne Makinda amesema hajaridhika kwamba suala la milipuko ya mabomu iliyotokea juzi Gongo la Mboto ni la dharura na lina maslahi kwa umma na kwamba halihitaji kujadiliwa kama jambo la dharura.

Spika amesema hayo kufuatia hoja iliyotolewa na mnadhimu wa kambi ya upinzani Tundu Lissu aliyetaka kanuni itenguliwe ili jambo hilo lijadiliwe bungeni.

JAMANI MNIWIE RADHI LAMA NITAWAKERA ila ninaamini Makinda hajasema hayo mloyaainisha humu. I REFUSE TO ACCEPT THAT FACT!!!!!!: KAMA AMESEMA KWELI NAOMBA ALIYE KARIBU NAYE ANISAIDIE KUYAJIBU HAYA:
1. Kwanini uwanja wa Mwl JK ulifungwa?
2. Mkurugenzi wa Anga alisema nini kwa mamlaka ya anga ya kimataifa kuhusu huo ufungaji?
3. Kwa nini aliahirisha Bunge baada ya kupata hiyo taarifa?
4. Kwa nini Waziri Mkuu kupitia Bunge kaomba wa-TZ na wahisani wasaidie hilo janga la dharura?
5. Kwa nini wanahamasisha wa-TZ wachangie damu ili kuokoa maisha ya Majeruhi wa kadhia hiyo?
6. Kama Zaidi ya Watanzania Mia nne wamejeruhiwa katika tukio la muda mfupi vile, Je ni tukio lenye kujeruhi watu wangapi, litachukuliwa kuwa ni dharura?
7. Tangu tupate uhuru hakujawahi kutokea tukio la mlipuko lililosababisha uwanja wa ndege wa kimataifa kufungwa, Kama hili ni tukio la kawaida kwa nini uwanja wa ndege ulifungwa? Je, kufungwa kwa uwanja wa ndege ghafla vile si dharura?
8. Kama si dharura kwa nini wa-TZ wenzetu wapatao elfu na zaidi wapewe malazi ya muda uwanja wa taifa badala ya kwenda kulala kwenye mahoteli au guest house au majumbani mwao?
9. Kova aliagiza askari wote waende eneo hilo, kama ni tukio la kawaida kwanini asimameshe shughuli nyinge zoote za ulinzi kwa ajili hiyo?
10. Kama si dharura kwa nini jeshi pamoja na Rais wa nchi watoe tamko?
MAKINDA ITS NOT ABOUT OPPOSITION PARTIES, ITS ABOUT SOVEREIGNTY OF THE PARLIAMENT!!
 
katika hili nakubaliana naye; siyo jambo la dharura. hivi wanajuaje kuwa siyo ughaidi?
Lahaulah kwahiyo speach ya mkwere isiyo na kichwa wala miguu ilikuwa sawa kujadiliwa kwa siku tano? This is an event that has re-occured twice what else do you need?
 
WANANCHI HATUKO SALAMA TENA NA MALI ZETU, KIIO KILA LEO NA MAYATIMA
KUONGEZEKA HIVYO SERIKALI NZIMA IJIUZULU HATA KABLA YA MAANDAMANO
YA KUTETEA 'UHAI WA WENZETU' KUANZA KOTE NCHINI


Mheshimiwa Kikwete kama amiri jeshi mkuu ajiuzulu pamoja na serikali yake. Jukumu la msingi halijazingatiwa; wananchi hatuko salama!! Tusianze kuzungusha kiswahili hapa ni uhai umepotea kwa uzembe!!! Hawa mayatima wanahitaji sauti zetu!!

Hatutaki tena tume kwa hata kule Mbagala chombo kama hicho hakikutusaidia zaidi ya kuwapa wanasiasa na makampuni ya kibiashara kujinadi kwenye kioo cha televisheni mgongoni mwa msiba na damu kwa wengine.

Jukumu la kwanza la kuhitajika uwepo wa serikali katikati yetu NI KUHAKIKISHA USALAMA KILA MMOJA WETU NA MALI ZETU. Kwa mtaji hizi picha nilizoona, serikali nzima ya CCM ijiuzulu mara moja

Mauaji Arusha walitupuuza kana kwamba kuliuaua nzi tu. Kule kwenye mashamba ya mpunga wala hawakujishughulisha kitu kuwajibika mtu. Sasa kama kweli kuna JAMBO AMBALO KIUKWELI KABISA KINATUHITAJI KUANDAMANA MPAKA KUELEWEKE NI KATIKA KUTETEA UHAI WA WENZETU.

Kama tutaona vifo hivi kama vile ni ya 'akina wale' na kwamba sisi wengine hatuhusiki basi hapo ndipo kiama chetu kinapoanzia. Kwa vifo hivi vyote 17 taifa tumepata yatima wangapiii?????????????
 
It is has become a government of blunders. Na ndiyo njia rahisi ya kututoa kwenye tatizo moja kwenda lingine. Tulikuwa tunapiga kelele kuhusu bei za umeme kupanda, ghafla umeme ukawa hamna tukasahau bei na kuanza kujadili giza na propaganda za kwa nini hakuna umeme. Kelele zilipozidi sana wakaibuka na malipo ya Dowans-tukaanza kumjadili Rostam na hiyo mihela tunayotakiwa tulipe. Hatujakaa sawa, mabomu na kauli za ovyo ovyo. What is next?
 
Kwa heshima na tahadhima nimekuteua wewe rasmi uwe mtu wa kumshughulikia mpaka akili zake zikae sawa.
Usijari maana nusu ya Mshahara wake atakupa wewe maadamu uwe unamfikisha kwenye kumweka sawa kiakili. Uteuzi huu umeanza rasmi leo. Kwa baraka zote za jamhuri tukufu ya Muungano.
Kama angekufa Fisadi Kikwete na au familia yoyote ya CCM ungesikia wanajadili. Huyu Mama nilishasema kuwa anahitaji mtu wa kumshughulikia mpaka akili zake zika sawa
 
hii serikali bwana ni kichekesho kabisa,
nilikuwa naongea na Mwananjeshi mmoja ananiembia kuwa hayo mabomu mengiu yalikuwa ni ya mwaka 1971,1972..etc
inasemekana walikuwa wakipewa pesa kila mwaka kununua mapya na vifaa vingine jamaa wanaweka kibindoni na kuthaminisha hayo yaliyo expire.
Ni uwazi usiopingika kuwa wanajeshi woye walijua kuwa hayo mabomu yangeweza kulipuka mda wowote
hivyo si ajabu wote wakawa wameshakimbia nyumba zao kabla ya mlipuko
wasingeweza kutoa taarifa kwa wannchi kwani waliogopa kujulikana kuwa walijua litatokea na kwa nini walishindwa kuyazuia mapema?
Hivyo hilo lilijulikana, na kama hawajafa ..inawezekana kabisa ikawa hivyo
Hata jamaa yangu kanieleza kuwa hakuna mwanjeshi hata mmoja aliyekufa( unless kama ameniingiza mjini kwa hilo):usa2:
Well,

Kwa sisi wenye akili timamu, tunafahamu kuwa "this was part of the plan"

Mtakuja kufahamu baada kwanini baadhi ya vifaa vipya vya kijeshi navyo pia viliteketea!!!
 
Mbona miaka hii mitano tutakoma, mara mtasikia waliokufa katika milipuko hiyo ni VIHEREHERE ndo SPIKA wa CCM huyo
 
Spika wa bunge Anne Makinda amesema hajaridhika kwamba suala la milipuko ya mabomu iliyotokea juzi Gongo la Mboto ni la dharura na lina maslahi kwa umma na kwamba halihitaji kujadiliwa kama jambo la dharura.

Spika amesema hayo kufuatia hoja iliyotolewa na mnadhimu wa kambi ya upinzani Tundu Lissu aliyetaka kanuni itenguliwe ili jambo hilo lijadiliwe bungeni.

Pambafu sake huyu mama!
 
Akili zake hazijatulia inaelekea anataka kutafutiwa mtu ali akili zikae sawa, kwani huoni mambo yake anayoyafanya bungeni ya kupayuka bila ya kutumia busara. Inahitajika ifanyike Rescue mission ya kumsaidia huyu mama Makimba aili akili zake zikae sawa:laugh:

Kwani Makamba yuko wapi amshughulikie? Watapata akili wakikutana hawa!
 
Spika wa bunge Anne Makinda amesema hajaridhika kwamba suala la milipuko ya mabomu iliyotokea juzi Gongo la Mboto ni la dharura na lina maslahi kwa umma na kwamba halihitaji kujadiliwa kama jambo la dharura.

Spika amesema hayo kufuatia hoja iliyotolewa na mnadhimu wa kambi ya upinzani Tundu Lissu aliyetaka kanuni itenguliwe ili jambo hilo lijadiliwe bungeni.

Ndio maana nilisema nchi hii kila kiongozi anajisema atakavyo. Hatujui nani ni nani or kila mtu anakula ofisini kwake. Yaani Rais wa nchi amsema hili ni janga la kitaifa, spika anasema hakuna issue hapo? Kumbuka hii issue inahusu pia Jeshi letu. Adui wetu sasa hivi wanajua ghala letu kuu la silaha limeungua moto na kuna uwezakano hatuna silaha za kutosha. Halafu anasema sio jambo la dharura. Kama sio jambo la dharura mbona jana alihairisha kikao cha bunge?
 
jamani kwa sababu za kiusalama si sahihi kujadili hili suala bungeni,kuna siri zaweza wekwa wazi wakati wa kujibu ambazo hazipaswi kuwa wazi,si kila kitu kinajadiliwa ovyo nyie watu,lazima wafanye uchunguzi na waweke mambo sawa kwanza(hata kama lilipangwa kuna namna ya kuwasilisha jambo kwa umma na international community inachukua muda).....heeeeeee,kuna haja ya watu kusoma somo la Usalama wa nchi......yaani hamna tofauti na Kikwete ambaye jana karopoka kuwa lile lilikuwa hiyo kati ya maghala makubwa,kwa usalama wa nchi ile si sahihi na hata wakuu wameshamwambia amechemka,leo mnataka lijadiliwe bungeni???mnafikiri nyie zaidi ya ushabiki wa vyama na chuki kwa huyu mama???

Michelle yeye amesema jambo sio dharura. Hakusema hawawezi kujadili suala kwa sababu za kiusalama. Angesema hivyo nimgemwelewa.
 
Spika wa bunge Anne Makinda amesema hajaridhika kwamba suala la milipuko ya mabomu iliyotokea juzi Gongo la Mboto ni la dharura na lina maslahi kwa umma na kwamba halihitaji kujadiliwa kama jambo la dharura.

Spika amesema hayo kufuatia hoja iliyotolewa na mnadhimu wa kambi ya upinzani Tundu Lissu aliyetaka kanuni itenguliwe ili jambo hilo lijadiliwe bungeni.[

hakika bunge letu la Tanzania limepata spika, spika Makinda. du sijui kama tutafika. niliwahi kuandika humu JF kwamba hakika bunge la Tanzania sio bunge tena, nadhani sasa yanatimia
 
Mheshimiwa Spika Makinda,
Inawezekana kuwa tuna tumia dictionary tofauti kutafsiri neno dharura (emergency). Vyovyote vile iwavyo kwa tukio la gongola mboto kama sio dharura basi hatuna dharura nchini.!! Watu wamekufa ghafla katika dk chache sana, watu wapo hospitalini kwa mauimivu na wengine ni vilema wa maisha. Watu wamepoteza watoto wao, wake na waume zao, waleta mkate wa kila siku, Makinda hiyo haioni dharura! pengine kumwagiza lema alete ushahidi jumatatu hiyo ndiyo dharura.
Kama si dharura kwanini aliahirisha kikao cha bunge? kama si dharura kwanini Rais akutane na mkuu wa majeshi saa 9 usiku? kama si dharura kwanini Red cross wajae uwanja wa taifa? kama si dharura kwani serikali yote ilikwenda Gongo la mboto juzi? Kama si dharura kwanini Polisi itoe taarifa kwa umma? kama si dharura kwa nini bomu la jeshi litue Tabata chumbani kwa mtu? Ni kwanini vyombo vyote vya habari duniani viliandika kuhusu tukio hili?

Kumekuwa na dhana potofu juu ya uwezo wa Wanawake kuongoza. wapo wanoamini kuwa Tanzania bado hatujafikia hatua hiyo. Kwa kauli na matendo ya Makinda wenye wasi wasi huo sasa hawana wasi wasi tena.
Makinda iwe changamoto kwa akina mama, TAMWA, TAULA,MEWATA n.k Makinda anawavuta nyuma, anaharibu taswira nzuri mliojijengea. Mama huyu asiyejua dharura ya maisha ya wanadamu kama mama na kiongozi hawatendei haki. Mkemeeni jamani anawarudisha nyuma miaka ya 40.
 
Back
Top Bottom