Spika Makinda Kaishitukia Serikali Ya Kikwete Haina Huruma na Mtanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika Makinda Kaishitukia Serikali Ya Kikwete Haina Huruma na Mtanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by lifeofmshaba, May 14, 2011.

 1. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  UPDATED 26/05/2011

  kumbe njia hakikufunguliwa umma ulidanganywa

  Mipango Miji yambana Spika afungue barabara
  Spika wa Bunge, Anne Makinda
  Joseph Zablon
  MWENYEKITI wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira Manispaa ya Kinondoni, Abbas Tarimba ametaka barabara iliyofungwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda ifunguliwe akisema hakuna mwenye mamlaka ya kujenga juu ya barabara.

  Akizungumza baada ya kikao cha kamati hiyo kilichofanyika juzi, Tarimba alisema siyo sahihi kwa barabara hiyo inayounganisha eneo la Kijitonyama na Sinza kufungwa.

  "Unaweza kuifunga barabara kwa muda tu, ama kwa kuwa unajenga au kuna tatizo la kijamii kama vile msiba au kitu kingine cha namna hiyo," alisema Tarimba akisisitiza kuwa hata mambo ya namna hiyo yana taratibu zake.
  Tarimba alisema hakuna mtu ambaye ana mamlaka ya kuifunga barabara moja kwa moja kisha akafanya ujenzi katika eneo hilo la njia.

  Alisema ingawa suala hilo halikuwa ajenda ya kikao cha kamati yake, walilijadili baada ya kuwasilishwa na Diwani wa Kata hiyo, Ulole Juma Athuman.

  licha ya kusema kwamba kitendo cha kuifunga barabara hakikuwa sahihi, alimtaka diwani huyo kuwa na subira huku akimsihi kutoitisha mkutano wa wananchi kama alivyoahidi.

  "Najua anataka kutumia ile ‘people's power' (nguvu ya umma) lakini nimemtaka awe na subira kwanza wakati suala hilo linashughulikiwa," alisema Tarimba.hata hivyo, Diwani huyo alisema kuwa dhamira yake iko palepale huku akitangaza kuitisha mkutano wa wakazi wa eneo Jumapili jirani na eneo la tukio.

  Alisema amechukua hatua hiyo kwa kuwa kinachoonekana ni kutupiana mpira baina ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Manispaa ya Kinondoni, huku wananchi wanaoendelea kupata adha wakidai majibu kutoka kwake. "Walinituma kulalamikia hali ya kufungwa kwa barabara hiyo, nimeleta malalamiko kunakohusika. Hatua za maana zisipochukuliwa, nalirudisha jambo hili kwao waamue," alisema Ulole.

  Diwani alisema haoni sababu ya kuendelea kusubiri wakati sheria na taratibu zipo wazi:
  "Hivi kama ningekuwa mimi ndiye nimeziba barabara, hadi sasa wangekuwa wanajadili kweli jambo hilo?" Alihoji na kuongeza kuwa anarudisha majibu kwa mabosi wake ambao ni wananchi siku hiyo ya Jumapili.

  Alisema kwamba wananchi wanaitafsiri hatua ya kufungwa kwa barabara hiyo kama ni kuporwa kipande cha ardhi ya barabara na kugeuza kuwa ni sehemu ya kiwanja cha kiongozi huyo jambo ambalo linawapa adha kubwa wakazi wa eneo hilo na lile la jirani.

  "Safari ya dakika tano kutoka Kijitonyama kwenda Sinza leo unaifanya kwa dakika zaidi ya 45, kisa! Barabara imefungwa na mtu mmoja kwa matakwa yake. Hiyo haiwezekani," alisema.
  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda alisema kuwa suala hilo limeshatoka kwake na lipo mikononi mwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo.

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana alisema juzi kuwa baada ya ofisi yake ilichunguza sababu za kiusalama ambazo zimetajwa kuchangia kufungwa kwa barabara hiyo, ilibaini kuwa hazipo.

  "Nilijaribu kuwasiliana na ngazi za juu kidogo pengine kulikuwa na maagizo yoyote ya kiusalama, lakini hakuna kitu kama hicho hivyo suala hilo wanalo wenyewe manispaa," alisema Rugimbana.Spika alifunga barabara hiyo inayopita jirani na nyumba anayojenga katika kiwanja namba 630 Kitalu 47, mnamo Mei 13, mwaka huu kwa sababu zilizoelezwa kuwa ni za kiusalama.


  13/05/2011 HABARI ILIANZA HAPA
  • Kahamia kwenye nyumba yake Sinza kutoka Hotel alikokuwa anaishi
  • Asema anaokoa pesa ya umma
  • Amewafungia njia wananchi wa Sinza
  • Je matumizi kama haya ni moja ya sababu ya serikali yetu kuwa mufilisi
  • Kwa nini na mawaziri wasirudi kwenye nyumba zao kuepusha gharama kubwa tunazolipa kwa siku

  GAZETI MWANANCHI

  Makinda azuia watu kutumia barabara

  Joseph Zablon

  SPIKA wa Bunge, Anne Makinda anadaiwa kufunga njia inayounganisha eneo la Kijitonyama na Sinza, Dar es Salaam na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji.Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na baadhi ya wakazi wa sehemu hiyo zimeeleza kuwa kutokana na kufungwa kwa njia hiyo, sasa wanalazimika kutumia dakika 45 kufika Sinza kwa miguu badala ya dakika tano hadi 10 walizokuwa wakitumia awali.

  Mkazi wa eneo hilo, Juma Mbegu alieleza kuwa njia hiyo imefungwa katika Mtaa wa Sahara, jirani na Kituo Kidogo cha Polisi cha Mabatini: "Njia hiyo imefungwa eti kuruhusu ujenzi wa nyumba yake ya ghorofa moja. Unajua mtu hadi agundue kuwa njia hiyo imefungwa, inambidi atembee kama dakika tano hivi ndipo akutane na uzio wa mabati."

  Kwa mujibu wa Mbegu, kibao kilichowekwa mwanzoni mwa Mtaa wa Sahara jirani na Kituo hicho cha polisi kuonyesha kuwa barabara imefungwa, nacho kina utata kwani watu wengi wanajua kuwa imefanyika hivyo kwa magari pekee. Alisema kufungwa kwa njia hiyo inayopita jirani na Kiwanja namba 630 katika Kitalu namba 47, kinachomilikiwa na Makinda, kumesababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo na vitongoji vyake.

  Mkazi mwingine ambaye hakutaka kutajwa gazetini alisema kutokana na kufungwa kwa njia hiyo, watu wanalazimika kuzunguka hadi Barabara ya Shekilango eneo la Afrika Sana, ili kufika eneo la Mori, mwendo ambao ni takriban dakika 45.

  Kauli ya uongozi wa Mtaa
  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kijitonyama, Philip Komanya alipoulizwa jana kuhusu suala hilo alisema hana taarifa ya kufungwa kwa njia hiyo."Sina taarifa na ndiyo kwanza nasikia kwako. Mbona hawajanifahamisha?" alihoji mwenyekiti huyo na kuongeza:"Njia hiyo imekuwa ikitumika pia wakati wa mvua kwani njia inayounganisha ile inayopita katika Kituo Kidogo cha Polisi Mabatini, huwa haipitiki kutokana na ubovu."

  Mwenyekiti huyo alisema anachojua ni kuwa Mei mwaka jana, wakazi wa eneo hilo kwa kumtumia Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wao, Athanas Mapunda waliwasilisha maombi ya kutaka kufungwa kwa njia hiyo kwa sababu za kiusalama, ombi ambalo hata hivyo, lilikataliwa.

  "Walileta ombi la kutaka hilo lifanyike lakini kikao cha kamati ya maendeleo ya kata kilikataa ombi hilo kwa sababu ni njia pekee katika eneo hilo ambayo inaunganisha maeneo mawili tofauti," alisema.
  Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, aliwashauri watafute jinsi ya kufanya ikiwa ni pamoja na kuweka lango la kuingilia katika mtaa huo na walinzi.

  "Pia nilishauri waweke muda wa kupita kwa watu wote na muda wa kupita wenyeji tu. Niliwaambia waweke geti, walinzi na waaandike muda wa mwisho kupita kwa watu wa kawaida lakini siyo kufunga njia."

  Mwenyekiti huyo aliahidi kufika katika eneo la tukio kujionea kinachoendelea akieleza kuwa kisheria, kabla ya kufunga barabara hiyo, mmiliki alipaswa kuwasiliana na ofisi yake.

  "Ngoja nifike hapo baadaye nitakupigia. Unajua wakati mwingine kuna watu huwa wanatumia njia za mkato kwenda manispaa kuomba vibali bila kushirikisha mamlaka nyingine halali. Huu ni ukiukwaji wa utaratibu na ni kinyume kabisa na misingi ya utawala bora."
  Kauli ya Spika
  Spika Makinda alipigiwa simu kutoa ufafanuzi wa madai hayo. Hata hivyo, mara baada ya mwandishi kujitambulisha kwake na kabla ya kumweleza lolote alisema: "Naomba niacheni kwanza. Wasiliana na katibu, tafadhali sana."

  Alipodokezwa kuwa suala lenyewe halihusu ofisi yake, bali yeye binafsi tena ni kuhusu kudaiwa kufunga barabara na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa eneo hilo, alikata simu.Baadaye Msaidizi wa Spika, Herman Berege alipiga simu na kukiri kufungwa kwa barabara hiyo akisema hatua hiyo imefikiwa kwa sababu za kiusalama na bosi wake alifuata taratibu zote.

  Alisema Makinda alipeleka maombi ya kufanya hivyo katika Manispaa ya Wilaya ya Kinondoni ambako kwa kuwashirikisha maofisa wa mipango miji na watendaji wengine, walikubali kuifunga njia hiyo. Alipoelezwa kauli ya mwenyekiti wa mtaa kwamba maombi hayo yalipelekwa kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata lakini yakakataliwa, msaidizi huyo wa Makinda alisema si kweli.


  "Tulikwenda na hadidu za rejea za kikao kilichopitisha uamuzi wa kufungwa kwa njia hiyo na makubaliano yalikuwa ama yawekwe matuta, ziwekwe nguzo kuzuia magari au uzio. Barabara hiyo ilikuwa lazima ifungwe kuzuia vitendo vya uhalifu."Alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya Spika Makinda kutaka aishi nyumbani kwake awapo Dar es Salaam badala ya kukaa hotelini kwa gharama za Serikali.

  "Lengo la mheshimiwa ni zuri tu, kunusuru pesa ya Serikali ambayo ingetumika kulipia anapoishi," alisema na kuongeza:"Alikopa kutoka taasisi tofauti ili kujenga nyumba hiyo na kulingana na hadhi yake, watu wa usalama waliona kuna haja ya kuifunga njia hiyo."
  "Nasisitiza kwamba utaratibu ulifuatwa na kama manispaa hawajaifahamisha serikali ya mtaa, hilo si kosa lake

  UPDATED 16/05/211
  Barabara iliyofungwa na Spika Makinda yafunguliwa
  Sunday, 15 May 2011
  Joseph Zablon
  BARABARA iliyokuwa imefungwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda katika eneo la Kijitonyama, Dar es Salaam, imeifunguliwa.Barabara hiyo inayounganisha maeneo ya Sinza na Kijitonyama ambayo inapita nje ya nyumba anayoijenga imeanza kupitika jana lakini ulinzi umeimarishwa katika eneo hilo.

  Makinda alifunga barabara hiyo na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa eneo hilo pamoja na watumiaji wengine kwa kile kilichodaiwa kuwa sababu za kiusalama.

  Barabara hiyo imefunguliwa siku moja baada ya gazeti hili kuripoti kufungwa kwake. Kibao kilichokuwa kinaonyesha kuwa imefungwa, kimeondolewa.Mwandishi wa gazeti hili alifika katika eneo hilo na kukuta kibao cha kuifunga kikiwa kimeondolewa lakini ulinzi wa askari polisi ukiwa umeimarishwa

  "Kaka weka kamera yako katika mkoba, picha hairuhusiwi eneo hili. Askari wa doria wakikukuta na hiyo kamera hapa huenda ukapata matatizo," alisema msamaria mwema mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina na kuongeza kuwa polisi wamekuwa wakifanya doria eneo hilo usiku na mchana.

  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kijitonyama, Philip Komanya alisema barabara hiyo imefunguliwa jana ingawa alidai kuwa suala hilo limemletea matatizo."Habari za huku mbaya, hali si shwari na ile barabara imefunguliwa," alisema.

  Komanya alisema hali katika mtaa wake si shwari kuhusiana na suala hilo akidokeza kwamba juzi alikuwa na kikao na wajumbe wake wa Serikali za Mitaa lakini hakutaka kueleza kwa undani walichojadili.

  Hatua ya kufungwa kwa barabara hiyo ililalamikiwa na wakazi wa eneo hilo na wengine waliokuwa wakiitumia kwa kuwa iliwalazimu kuzunguka hadi Barabara ya Shekilango eneo la Afrika Sana ili kufika eneo la Sinza Mori kwa kutumia takriban dakika 45 badala ya kati ya dakika tano mpaka 1o kupitia hapo.

  Alhamisi iliyopita gazeti hili lilimkariri Komanya akisema Mei mwaka jana wakazi wa eneo hilo kwa kumtumia mjumbe wa serikali ya mtaa wao, Athanas Mapunda, waliwasilisha maombi ya kutaka kufungwa kwa njia hiyo kwa sababu za kiusalama ombi ambalo lilikataliwa.

  Hata hivyo, Msaidizi wa Spika, Herman Berege alisema kuwa bosi wake alifunga barabara hiyo baada ya kufuata taratibu zote.Alisema Makinda alipeleka maombi Manispaa ya Kinondoni ambako kwa kuwashirikisha maofisa wa mipango miji na watendaji wengine walikubali kuifunga njia hiyo.

  Alisema: "Barabara hiyo ilikuwa lazima ifungwe kuzuia vitendo vya uhalifu."Alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya Spika Makinda kutaka aishi nyumbani kwake awapo Dar es Salaam badala ya kupangishiwa na serikali hotelini."Lengo la mheshimiwa ni nzuri tu, kunusuru pesa ya serikali ambayo ingetumika kulipia anapoishi," alisema.


  maoni yangu : media muhimili wa nne na nguvu yake ni dhaili hapa,
  viongozi wetu ni wa binafsi na wakurupukaji hawana uzalendo wala kujali jamii inayowazunguka
  peopleeeeeeee powerrrrrrrrr
   
 2. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2011
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Hivi mawaziri wote wakiishi kwenye nyumba zao na viongozi wengine wa juu serikalini, Wakafunga njia Dar kutakalika tena??Au ndo tutapelekwa kuishi Tandahimba ili viongozi waishi Dar ?Nadhani kuna taratibu maalum za nyumba za viongozi kuishi maeneo fulani.Kama hazitoshi basi wawachukulie viwanja huko Mkuranga na Kimbiji kwani wana magari ya kufika huko! Inanikumbusha kule Harare ,Mugabe hufunga njia ipitayo karibu na makazi yake na muda wote hulindwa na kikosi maalum cha Mizinga hata kama hayupo!!! Ni gharama gani hizo kwa walipa kodi?Acha usumbufu kwa raia!!!!
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  May 14, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,378
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  Wakifanya hivyo mawaziri wote sasa watakula wapi na mshahara wao mdogo huo?....acheni tu wapande mahotelini tutawalipia mbona tz ni nchi tajiri sana au hamuoni rasilimali tulizonazo au mmoja aniambie tumekosa nini mpaka tuwatese mawaziri wetu wapendwa kiasi hicho wakati wanauwezo wa kutusaidia watz ikiwemo kusaini mikataba fasta hata km ikiwa watatakiwa kupanda ndege usiku kwenda kw wawekezaji?.......waacheni jamani ila naoma makinda ni ushamba tu unamsumbau
   
 4. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #4
  May 14, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  haya ndio nchi nzima inawafanyia kazi, nadhani mama alipoletewa bill, hakuamini macho yake, kama ana mwenzake naye tunamlipia chakula asubuhi mchana na jioni?
  sasa weka hao mawaziri wengine sasa, tena kuna wasio hata na mke, wakija viwavi wao sisi tunawalipia bill kwenye VAT
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  May 14, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yaani watu wangejua barabara ya kwenda kwa huyu mama ilivyo mbovu nadhani watu wasingeamini kwamba ni kiongozi wa serikali miaka yote hiyo. My point is kama njia wanazopita wao ziko hivyo je inakuwaje zile barabara za vijijini. Kwa kifupi ni aibu spika wa bunge kupita hiyo barabara eti kwenda nyumbani kwake. Kuvunja hiyo njia hakusaiidii
   
 6. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #6
  May 14, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  lakini je pesa alizokuwa anatumbua huko hotelini katumia busara
  kwenye kuishi nymbani kwake,
  kiwango cha chini ni kama laki moja na nusu kwa siku
  hayo ni makadirio ya chini kabisa
   
 7. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #7
  May 14, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  na wengine wakifunga njia itakuwaje sasa.......
   
 8. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #8
  May 14, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  kufunga njia ni uchizi wao tu, kwani wanafunga njia kwa kuogopa nini?
  mbona kwenye foleni za DAR wanajichanganya ?
  wakienda Dodoma hakuna anayejari usalama wake sio? kila mtu huyo busy kutafuta totos


   
 9. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #9
  May 14, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Tanzania bado hiko salama ila viongozi wetu wanajifanya miungu mtu?
  na kupenda kutafuta kodi yetu, wengi wao nawa mabangalo mazuri tu sema wanaogopa tutajua
  kuna kamamishina wa magereza taifa bwana BAnzi alikuwa naishi ukonga na bado anaishi ukonga,
  kulikuwa na ulinzi ndio lakini hakuna kilichomzuri raia maana ulinzi ulikuwa ndani kwake, wao waweke ukuta
  wafungue njia hiyo
   
 10. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #10
  May 14, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,537
  Likes Received: 2,116
  Trophy Points: 280
  Hivi Nyumba maalum kwa Spika wa Bunge la Muungano kule Oysterbay, Dsm aliyokaa Adam Sapi, Pius Msekwa, Samwel Sitta haipo? Au ndo ilishauzwa?

  Kuna umuhimu wa kuwa na makazi rasmi ya viongozi wetu ili akiondoka kiongozi mmoja madarakani basi anampisha kiongozi mpya anayekuja na siyo kukaa mahotelini au ktk nyumba za kupanga kwa vile kiongozi aliyeondoka madarakani 'kakopeshwa' au 'kapewa nyumba ya serikali'. Matokeo ndo hayo mara gharama za hoteli, kukodisha nyumba mara kufunga mtaa!
   
 11. SaidAlly

  SaidAlly JF-Expert Member

  #11
  May 14, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,806
  Likes Received: 648
  Trophy Points: 280
  Na bado hapo ndio wataelewa sasa kwanini wananchi hatukupenda wajiuzie nyumba za serikali, mtakumbuka Makamba alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar alifikia hotelini hadi akaibiwa Redio yake, laiti nyumba za serikali zingekuwepo hii dhahama kwa wnanchi wala tusingeijua.
   
 12. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #12
  May 14, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  nadhani na yenyewe iliuzwa nadhani kwa huyo mwenye RED hapo chini?
  sasa sijui SITTA alikuwa anakaa wapi?
  au alipoa HOTELINI kwa tumiaka tutano maana kipindi kile tulikuwa hatujashituliwa na huu ujangiri wa serikali
  anyway Magufuli ndiye anayejua alimuhuzia nani?
  i hope yeye Mgufuli ana nyumba ya kukaa na hayuko hotelini
  ili ni tatizo jingine la KIKWETE muoga kuchuua hatau anashindwa nini kuwa rudishia change hao waliouziwa
  kicha kuwapa notes ya kuahama maana hayo maeneo ni bora kwa viongozi itakuwa ngumu sana kupa maeneo kama hayo hapa DAR,
  MIMI UWA NASHINDWA KUELEWA WALIPOUZA WALIKUWA NA PLAN GANI? KUISHI HOTELINI?


   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  May 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kuhamia nyumba zao kutapunguza gharama za serikali na pia kutawapa fulsa watumishi hao pesa za serikali kuingia mifukoni mwao badala ya kupelekwa mahotelini
   
 14. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #14
  May 14, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ile nyumba aliuziwa msekwa aise! By tha way si wakamuweke kwenye nyumba za mawaziri kule mikochen au kumejaa?waache kutupa tabu za bure wananchi wa kawaida jmn
   
 15. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #15
  May 14, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Wanapenda sana starehe kwa pesa ya umma, tatizo wengi wao wanajifanya wote mfisadi kama RA wakati wana ndugu wamechoka huko vijijini kwao, ndio maana wakitoka madarakani wanazee ghafla   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  May 14, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  huyu mama ni crap, ni bora abaki hotelini kuliko kufunga mtaa in the name of security... kama huamini unaowaongoza then why vying for a position in leadership??

  HER PRESENCE KIJITONYAMA NI KERO KWA WANANCHI, ARUDI AKAKE JIMBONI KWAKE AU DODOMA NA SIO KIJITONYAMA
   
 17. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #17
  May 14, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  mangula.jpg wedd12.jpg
  Wanapenda sana starehe kwa pesa ya umma, tatizo wengi wao wanajifanya wote mfisadi kama RA wakati wana ndugu wamechoka huko vijijini kwao, ndio maana wakitoka madarakani wanazee ghafla
   
 18. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #18
  May 14, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Acha kunikumbusha hasira na masikitiko niliyonayo jinsi magufuli alivyotutenda katika kuuza nyumba zetu . Plz!
   
 19. s

  seniorita JF-Expert Member

  #19
  May 14, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mmmmmhhhhhhhh awafungie njia watu......that is so unfair...kwani si ana fedha za kutosha atafute a different place...where she does not disturb local population and the population will not disturb her instead of inconveniencing wananchi to foot 45 mns daily instead of 5-10 mns....ukizidiwa hizo dakika kwa idadi ya watu utapata masaa mengi sana wasted na hiyo ni hasara kwa watu na pia kwa jamii
   
 20. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #20
  May 14, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  tena huyu ni wakumfanyia operation hasirudi mwaka 2015
  kalitia hasara taifa bila sababu phd holder gani anayeshindwa kufanya research
  kwa nini hizo nyumba zilikuwepo at the first place kabla ya kuziuza
  au ndio tamaa ya kupitiliza

   
Loading...