Spika Makinda azuia Bunge kuingilia sakata la Mhando

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
SPIKA wa Bunge, Anne Makinda ameizuia Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), kuchunguza sakata la kusimamishwa kwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi William Mhando.Mhando na watendaji wengine watatu walisimamishwa kazi na Bodi ya Wakurugenzi ya shirika hilo Julai 14, mwaka huu wakituhumiwa kwa ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.

read more Spika Makinda azuia Bunge kuingilia sakata la Mhando

Huyu mama atazuia kila jambo mwaka huu
 
Mimi nijuavyo ni kuwa kwanza amekuwa cleaned out of mercy na kurudishiwa nafasi yake...
Ina maana bado kuna tuhuma za ufujaji?
 
Mimi nijuavyo ni kuwa kwanza amekuwa cleaned out of mercy na kurudishiwa nafasi yake...
Ina maana bado kuna tuhuma za ufujaji?

Pengine bodi baada ya kusikia Zitto (CDM) wamelivalia njuga wameogopa kuwa yataibuka mengi. Soma hii kauli ya Zitto akipingana na spika, ""POAC tunahusika na usimamizi wa hesabu za fedha za shirika, tunataka kujua ubadhirifu na masuala ya kisheria na itahakikisha uwajibikaji unaostahili na tutasimamia hilo kwa nguvu zote kwani hatutaki uonevu.""
 
Bodi ya Tanesco nayo hopeless miaka yote hakuna ufanisi bado imo tu si nayo ivunjiliwe mbali tu?!
Hii serikali inakera sana bwana.
 
Kumbe hizi kamati za bunge sio huru? Spika ana uwezo wa kuzuia kamati kufanya kazi zake eh
 
Nawasahuri sisiem na Serikali yake kutokana na kuhojiwa sana na CDM Bungeni kwa kuwasilisha bajeti kiini macho ipandikize mtu kwa Sura ya CDM afungue kesi ya bajeti ya Serikali yake ili isijadiliwe Bungeni mwaka upite bila kujadiliwa. Mahakama ndio mbinu mpya iliyobaki ya kuzuia masuala nyeti ya mstakabali wa Nchi. Bravo sisiem
 
Back
Top Bottom