Spika Makinda awashauri mawaziri kuwabana watendaji

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
105,111
2,000
Spika Makinda awashauri mawaziri kuwabana watendaji"Mmeyasikia yaliyotokea humo ndani (bungeni), nani waziri alisimama na kwenda kukemea…Kwa hiyo suala la wenzentu kuwajibika ni suala la kimsingi kabisa ili hasira za wananchi ziweze kupoa kama si kuisha.''
Na Sharon Sauwa, Mwananchi

Posted Jumapili,Decemba22 2013 saa 11:41 AM
Kwa ufupi


  • Wakati Spika Makinda akisema hayo, wabunge kwa upande wao wamepongeza hatua ya kuwajibishwa mawaziri wanne na uamuzi wa kuunda Tume ya Uchunguzi wa Kimahakama, kwamba kutasaidia kupunguza machungu yaliyotokana na Operesheni Tokomeza Ujangili

Dodoma. Muda mfupi kabla ya kuahirisha Bunge jana, Spika Anne Makinda amesema moto uliotokea kwenye kikao hicho, ndivyo itakavyokuwa katika siku zijazo wakati wa kujadili taarifa za kamati .

Wakati Spika Makinda akisema hayo, wabunge kwa upande wao wamepongeza hatua ya kuwajibishwa mawaziri wanne na uamuzi wa kuunda Tume ya Uchunguzi wa Kimahakama, kwamba kutasaidia kupunguza machungu yaliyotokana na Operesheni Tokomeza Ujangili.

"Sipendi kuona mawaziri mnaondoka kila mwaka, sipendi kabisa, kabisa, lakini ni dalili kuwa lazima kuwe na mabadiliko, "alisema Spika Makinda na kuongeza;

"Na wala msiwaachie watendaji wenu kila mwaka kwa sababu jamaa hawa (wabunge), watafanya hivyo kila mwaka kwa sababu watawasilisha taarifa zao."

Aliwashauri mawaziri kuhakikisha kuwa wanafanya kazi katika wizara zao, badala ya kuwategemea watendaji tu kwa sababu wanaokuja kuadhibiwa na Bunge ni wao.

"Tunawaomba mawaziri mwangalie sehemu zenu za kazi. Msiache mahali pakalala mkategemea watu wengine mnapokuja kuungua vidole, wao hawapo. Kwa hiyo wengine mjitahidi,"alisema.


Mawaziri ambao uteuzi wao ulitenguliwa na Rais Jakaya Kikwete kutokana na matatizo yaliyojitokeza katika operesheni hiyo ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo.

Wakizungumza juzi jioni mara baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kulitangazia Bunge uamuzi wa Rais Kikwete wa kuwawajibisha mawaziri hao, baadhi ya wabunge walisema uamuzi huo umelisaidia Taifa.

Kwa upande wake Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM), alisema ni uamuzi wa busara kwa sababu ni suala la kuwajibika.

"Si kosa lao lakini makosa yamefanywa na watendaji walio chini yao…kwa hiyo suala hili ni kwa ajili ya kulinda heshima ya nafasi zao, chama chetu na Serikali ni lazima tu wawajibike," alisema.

Alisema; "Mmeyasikia yaliyotokea humo ndani (bungeni), nani waziri alisimama na kwenda kukemea…Kwa hiyo suala la wenzentu kuwajibika ni suala la kimsingi kabisa ili hasira za wananchi ziweze kupoa kama si kuisha,"alisema.

Mbunge wa Igunga, Dk. Dalaly Kafumu (CCM), alisema; "Tatizo limetokea kwenye wizara yako hata kama hukushiriki kwa sababu limetokea katika wizara yako lazima uonyeshe kukomaa kwako kwa hiyo nawapongeza kwa kweli,"alisema Dk. Kafumu.

Naye Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), alimpongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, kwa kuamua kujiuzulu baada ya kusikia kauli za wabunge kuhusiana na operesheni hiyo.

"Lazima tukubali kuwa kuna matatizo ya kimfumo ambayo yamewafanya baadhi ya watendaji kuwa miungu watu," alisema.

Alisema kuna makatibu wakuu na wakurugenzi ambao mawaziri wanashindwa kuwawajibisha baada ya kujiwekea mfumo.

Mbatia alisema Rais Kikwete ndiye mwenye uwezo wa kufumua mfumo huo kwa kutumia Tume ya Uchunguzi wa Kimahakama.

Hata hivyo, alisema vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kusukuma yaliyojitokeza bungeni katika mkutano wa 14 ambao ulikuwa mahususi kwa ajili ya kujadili ripoti za utekelezaji wa kamati za kudumu za Bunge.

 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom