Spika Makinda ang’ang’aniwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika Makinda ang’ang’aniwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Jul 30, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  JUMATATU, JULAI 30, 2012 05:03 NA WAANDISHI WETU, DAR NA DODOMA

  *Atakiwa kutaja wabunge waliohusika
  *NCCR Mageuzi yampatia wiki moja
  *Watuhumiwa hatarini kupoteza ubunge wao
  *January Makamba apigilia msumari wa mwisho

  LICHA ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kutangaza kuivunja Kamati ya Nishati na Madini na kamati nyingine kutokana na tuhuma za kukithiri kwa vitendo vya rushwa, baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na watu wa kada mbalimbali, wameendelea kumng'ang'ania awataje kwa majina wabunge wote wanaotuhumiwa.

  Kwa nyakati tofauti jana, viongozi wa vyama vya siasa waliitisha mikutano na waandishi wa habari na kusema hiyo ndiyo fursa pekee ambayo itarejesha imani kwa wananchi.


  Kutokana na hali hiyo, Chama cha NCCR-Mageuzi, kimesema kama Spika Makinda atashindwa kuwataja wabunge hao, basi chenyewe kiko tayari kutaja majina ya wabunge wanaotuhumiwa kudai na kupokea rushwa.


  Msimamo huo, umetolewa jana na wabunge wa chama hicho, walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.


  Katika mkutano huo, alikuwepo Mbunge wa Kuteuliwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia, Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali na Mbunge wa Kasulu Vijijini, Zaitun Buyogela.


  Katika mkutano huo, Mbatia alisema wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa wanajulikana na kwamba hata juzi wakati wa kupitisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, walishindwa kuhudhuria Bunge kutokana na aibu waliyokuwanayo.


  "Hawa watu wanajulikana kwa majina kwani hata jana (juzi), wakati tunapitisha bajeti ya Wizara ya Nishati, walitoroka bungeni na mimi niliwachunguza hadi nje sikuwaona.


  "Wakati wengine walitoroka, baadhi waliingia na hao ni wale wachache wajanja wajanja ambao wanapenda kupuliza huku na huko.


  "Kwa kuwa tabia hii imelichafua Bunge, tunamuomba Spika wa Bunge awataje kwa majina na kama atashindwa kuwataja kabla Bunge halijaahirishwa, basi sisi tutawataja kwa sababu tunawajua," alisema Mbatia na kuungwa mkono na wenzake.


  Kwa mujibu wa Mbatia, wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa, wanatakiwa kutajwa kwa kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kulirejeshea Bunge heshima iliyoshuka.


  "Hata Waziri Sospeter Muhongo, alipokuwa akihitimisha bajeti ya wizara yake ya Nishati na Madini, alisema kuna baadhi ya wabunge wanafanya biashara na TANESCO, hawa nao lazima watajwe kwa majina.


  "Lazima wachukuliwe hatua, kwani sisi tunaendesha Bunge letu wakati mwingine kwa kufuata nchi za Jumuiya ya Madola zikiwamo Uingereza na India, ambazo ziliwahi kuwachukulia hatua wabunge wake waliokumbwa na kashfa ya rushwa," alisema.


  Akizungumzia kauli ya Spika wa Bunge, Anne Makinda, aliyosema juzi, kwamba ameiagiza Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, ili ichunguze tuhuma dhidi ya rushwa kwa wabunge, alisema baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo ni watuhumiwa wa rushwa.


  Kutokana na hali hiyo, aliwataka wajumbe hao kujiondoa ndani ya kamati hiyo vinginevyo haki haitatendeka kwa kuwa nao ni watuhumiwa.


  "Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo ni wachafu, kwa hiyo, ili uchunguzi ufanyike vizuri lazima kwanza wajitakase ili haki itendeke.


  "Bunge sasa limechafuka, kila mtu analishangaa na ili lionekane ni Bunge safi, lazima maamuzi juu ya kashfa hii yawe wazi na usifanyike upendeleo.


  "Pia mbunge yeyote anayeamini anatuhumiwa kwa rushwa, awe ni wa chama changu au wa chama chochote, uwe ni wewe Machali au wewe mama, ondoka na katika hili nitakuwa na sura nyingine kabisa pindi mtakapokuwa mkiwajibishwa.


  "Hata wabunge wale waliotajwa na Profesa Muhongo, wanafanya biashara na TANESCO, nao waachie ngazi.


  "Vyama vinavyojiita viadilifu viige mfano wa CUF, maana katika Bunge la nane wakati Msekwa ni Spika, kuna wabunge wanne wa chama hicho walikumbwa na kashfa ya rushwa na wakafikishwa mahakamani na pia CUF yenyewe ikawapiga marufuku kushika nyadhifa zozote ndani ya chama hicho.


  "Kwa hiyo, hawa watuhumiwa wajipime na kama hawajui, nawaambia Sheria namba 3 ya mwaka 1988 ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, inasema Mbunge anaweza kufungwa miaka mitano kama atapatikana na hatia ya rushwa.


  "Sisi tunayasema haya kwa nia njema, tunataka heshima ya Bunge irejee, pia tunamtaka Spika azitaje na kuzivunja kamati hizo alizosema atazivunja kwa kashfa hii ya rushwa, kwa sababu sisi tunajua ziko takribani kamati sita," alisema.


  Alitoa mfano jinsi Bunge, lilivyokaa kimya juu ya hoja iliyowasilishwa bungeni mwaka jana na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), aliyewataja kwa majina baadhi ya wabunge wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, kwamba walikuwa na kashfa ya kudai rushwa.


  Naye, Machali alisisitiza kama Spika wa Bunge atashindwa kuwataja kwa majina wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa, watatajwa baada ya wiki moja. "Kama tulivyosema, Spika akishindwa kuwataja baada ya wiki moja, sisi tutawataja na pia tutawasilisha hoja binafsi bungeni kutaka jambo hili lijadiliwe.

  JANUARY MAKAMBA
  Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ambaye awali alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, alisema ni sahihi kamati hiyo kuvunjwa, kwa sababu imekithiri vitendo vya rushwa.

  "Wakati mimi nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, vilikuwapo vitendo vya rushwa, si kwa wajumbe wote ila baadhi yao walikuwa vinara, kutokana na hali hiyo nilivipigia kelele na nimepata shida sana kupambana navyo," alisema na kuongeza:

  "Tuliweka msimamo ndani ya Kamati kwamba vitendo hivyo havikubaliki hata kidogo na ilifikia hatua nilienda kuwashitaki kwa Spika, Anne Makinda, kuhusu tabia ya baadhi ya wajumbe kupokea rushwa na alikubaliana na mimi kisha naye alikemea vitendo hivyo.

  "Kusema ukweli tulifanikiwa kuvidhibiti kutokana na msimamo wa pamoja tuliokuwa nao. Baadhi ya wajumbe wa kamati wakalalamika kwanini nimeenda kusema kwa Spika, unajua ni wabunge wachache ndiyo wanaoharibu sifa ya wabunge wengine.

  "Kwa hiyo, wananchi wasidhani wajumbe wote wa Kamati ya Nishati na Madini ni wala rushwa, hapana, wanaofanya vitendo hivyo ni wachache kama nilivyosema hapo mwanzo.

  "Mimi nataka uchunguzi huo ufanywe haraka na wote wanaohusika wajulikane."

  Katika hatua nyingine, alisema wakati akiwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, kuna baadhi ya watu walikwenda kwa baba yake, Yusuph Makamba kwa ajili ya kumshawishi alegeze msimamo wake.

  "Unajua Kamati hii ina ‘deal' na mambo makubwa na yenye maslahi ya watu, kwa hiyo usipokuwa makini kama kiongozi wa kamati au mjumbe wa kamati, watu wengi watakufuata na kukushawishi kwa fedha," alisema na kuongeza:

  "Mimi nilikuwa na msimamo wangu na ndio maana hata watu wengine wakawa wanaogopa kuanza kunifuata na kunieleza wanayotaka niyafanye.

  "Nakumbuka siku moja, kabla ya kwenda katika mdahalo wa Star Tv kuna watu walimfuata mzee Makamba na kutaka anishawishi nisizungumzie mradi mmoja wa umeme ambao ulikuwa na walakini.

  "Lakini Mzee Makamba akawajibu kwamba mimi sikai kwake na nimehama tangu nikiwa na umri wa miaka 18, kwa hiyo hana namna yoyote ya kufanya. Kwa hiyo mtu unatakiwa uwe na msimamo na ifikie hatua wakuogope."

  CUF NAYO YANENA
  Nacho Chama cha Wananchi (CUF), kimevitaka vyama ambavyo wabunge wake wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa, kulihujumu Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), vijisafishe haraka kwa kuwachukulia hatua kali wabunge wao, ikiwa ni pamoja na kuwavua uanachama.

  Kauli hiyo, imetolewa mjini Dar es Salaam jana na Naibu Katibu Mkuu Bara, Julius Mtatiro, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali yaliyoibuka nchini.

  Alisema CUF, kimesikitishwa na kitendo cha wabunge hao kupokea ‘milungula', kwa ajili ya maslahi yao binafsi badala ya kuwatetea wananchi.

  "Inasikitisha kuona Bunge ndilo linalotakiwa kuielekeza Serikali na wabunge nao, lakini cha ajabu wabunge wake wanajihusisha na vitendo vya rushwa kwa maslahi yao binafsi…wanakuwa mstari wa mbele kuwatetea wafanyabiashara.

  "Hiki ni kitendo ambacho kinatia kinyaa na kichefuchefu kwa sababu hata Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, anasema vitendo hivi havijaanza leo, inaonekana vimeota mizizi.

  Akizungumzia kuhusu mkanganyiko uliojitokeza kuhusu mabadiliko ya muswada wa mabadiliko ya Sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Mtatiro aliitaka serikali iache kuwadanganya wananchi. "Hii ni sawa na danganya toto, kwa sababu kitendo cha Mkurugenzi wa SSRA kudai eti kuna miongozo na kanuni ambazo zitairekebisha sheria hii, ni jambo ambalo haliwezekani.


  KUVULIWA UBUNGE

  Taarifa za uhakika zilizopatikana jana kutoka mjini Dodoma, zinasema wabunge wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa, wako hatarini kupoteza ubunge wao.

  "Ndugu yangu mambo yako wazi, ngoja tume iliyopewa kazi hiyo ifanye kazi yake, lakini jambo kubwa ambalo naweza kukwambia ni kwamba wale wanaotuhumiwa wako hatarini kuvuliwa ubunge wao," kilisema chanzo chetu.   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Kwanini Bunge letu liwe chombo cha kuchagua, kulinda, na kuficha Majina ya Majangili tuliowatuma kutunga Sheria na

  kutulinda. Speaker anawalinda Kuficha Majina yao? Kwanini kila kitu kikifika BUNGENI ni SIRI? Mabunge ya NCHI

  ZINGINE ndiko siri zinapotoka... Ina Maana Ma-Speaker wetu ni Madikteta???? HAYA BASI WAWAVUE UBUNGE...
   
 3. A

  Asa79 JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 591
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Makinda bado ni kinda ktk kusimamia masuala mengi mazito....anapwaya kupita kiasi ni hasara tupu kuwa na spika km makinda
   
 4. B

  Bob G JF Bronze Member

  #4
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wiki moja ya nini Mbatia Unampa ajenti wa Mafisadi huyo mama, Toa maasaa 5 tu leo tujue? Hio wiki ninavyowajua watahongwa wabunge na hio mada itakufa kifo cha mende na mtasikia waziri na katibu mkuu wake hawana kazi, hukuona mwingine alishaanza kujitangaza eti ni mwadilifu na anafaa kuwa amiri jeshi mkuu anawaza mambo ya jirani na kwao huko Burundi, congo na Rwanda vita 2
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  * I failed to Understand why MODS moved this TOPIC from "HABARI ZA SIASA" to "HABARI MCHANGANYIKO"

  Is it really not a political Issue? I failed to understand their Intentions...


  WOW IT HIT'S ME... INAKATISHA TAMAA KWELI KAMA UHURU WAKO KIDOGO UNACHUKULIWA KIBABE...
   
 6. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kama Spika naye anahusika????.
   
 7. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Yes, ikibainika wavuliwe ubunge pasipo kujali wametoka chama gani.
   
 8. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Spika wa bunge hili asipoyataja majina ya wabunge wala rushwa ni dhahiri kwamba hata ka reputation kadogo ka bunge kalililikokuwa kamebaki kwa wananchi nako katapotea.

  Na asitegemee tena kwamba bunge hili litaweza kupata tena nafasi ya kujisahihisha na kujisafisha toka katika tope la rushwa zaidi ya hii ya sasa.

  Kafulila aliwahi kuzungumza "live" bungeni lakini mama makinda kwa kutumia busara za kamati yake ya uongozi akalitia kapuni, muda mfupi baadae mtuhumiwa mmoja wa Kafulila akabambwa ba Takukuru anachukua rushwa. Hiyo ilitosha kumzindua usingizi spika lakini kwa bahati mbaya ameendelea kuwalinda wabunge wala rushwa kwakuwa mara zote wamekuwa ni wabunge wa chama chake cha CCM.

  Kwakuwa safari hii kuna wabunge wa upinzani wanatajwa, basi nadhani anaweza kupata ujasiri wa kuwataja ili kujisafisha yeye binafsi pamoja na bunge na kujitenga na genge la wala rushwa.
   
 9. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,806
  Likes Received: 1,053
  Trophy Points: 280
  Nafasi ya kuchafuana imewadia, kigezo gani kitatumika? wabunge lini wamezuiwa kufanya biashara na serikali au mashirika yake!

  Kila mtua atataja wa kwake, mi naanza na Mnyika...... nnavomuona ni mla rushwa mkubwa, spika andika jina lake.
   
 10. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mh hebu nyie akina Mbatia wiki ndefu tutajieni mapema
   
 11. Sibhonike

  Sibhonike Senior Member

  #11
  Jul 30, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hakuna atakayebaki aiseee!!
   
 12. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Ataje Kwani ile Sera ya Kulindana Imefutwa?
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  KAFULILA ALIWATAJA AKINA ZABEIN MHITA.... nini kilifanyika??
   
 14. M

  Mbozib JF-Expert Member

  #14
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapo msishangae spika kuwataja wabunge wa CDM tu kwasababu ya ushabiki na chuki binafsi
   
 15. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #15
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  Mh. Mleta mada, hicho kichwa cha habari kimenifanya nikurupuke kuacha ugali wangu ukapoa nikifikiri Madame Supika amekamatwa na Puli za banji na tunguli Bungeni!!!! Au kang'ang'aniwa na yale mawig anayovaa kama nguchiro pale mbele Bungeni. Nitake radhi mkuu,kwa kuwa imenibidi nirudi kusonga ugali usiku huu na sufuria niiazime kwa mama mwenye nyumba.
   
 16. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #16
  Jul 31, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Spika hatuna bana mbona mnaumiza kichwa kwa mambo rahisi
   
 17. d

  dizo Member

  #17
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wahusika wanafahamika inachotakiwa spika awataje na wanyongwe adhrani
   
Loading...