Spika Makinda amzima Ole Sendeka, amwambia huwezi kumshitaki Tundu Lissu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika Makinda amzima Ole Sendeka, amwambia huwezi kumshitaki Tundu Lissu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 1, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]JUMATANO, AGOSTI 01, 2012 06:44 NA MAREGESI PAUL, DODOMA

  *Amwambia hawezi kumshitaki Tundu Lissu
  SPIKA wa Bunge, Anne Makinda, amemzima Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka (CCM), aliyetaka kujua kama anaweza kumburuza mahakamani, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA).

  Spika Makinda alisema Ole Sendeka hawezi kumshitaki mahakamani Lissu kwa kuwa mbunge anapotoa shutuma dhidi ya mtu pindi anapokuwa bungeni au nje ya ukumbi wa Bunge, huwa ana kinga ya kutofikishwa katika vyombo vya sheria.

  Spika Makinda alitoa msimamo huo jana, baada ya Ole Sendeka kuomba Mwongozo wa Spika akionyesha nia ya kutaka kumshitaki Lissu kutokana na shutuma dhidi yake zilizotolewa na Lissu juzi, kwamba yeye (Ole Sendeka) ni kati ya wabunge wenye mgongano wa kimaslahi na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

  Akitoa uamuzi wake, Spika Makinda aliwataka wabunge kuwa wavumilivu, kwa kuwa tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge zinafanyiwa kazi na vikao husika.

  “Waheshimiwa wabunge, naomba Bunge hili liwe na subira kwa sababu suala ambalo lilijitokeza Jumamosi nililitolea uamuzi sijui kwa nini mnapenda kulizungumzia.

  “Kuhusu yaliyosemwa jana na Lissu kinga za Bunge ni pamoja na pale aliposemea, aliposema pia ni sehemu ya Bunge, eneo lolote linalohusu eneo lote la mipaka ya Bunge ni eneo la Bunge.

  “Kwa hiyo basi, tunachoshukuru ni kwamba, kwa vile amezungumza hicho, basi yeye atakuwa ndiye msemaji wa kwanza kutoa ushahidi kwa kamati ambayo nimeipa kazi hiyo,” alisema Spika Makinda.

  Awali, Ole Sendeka alimwomba Spika ampe mwongozo kama anaweza kumfikisha mahakamani mbunge mwenzake huyo kwa kuwa kitendo cha kuhusishwa na kudorora kwa TANESCO kimemshushia heshima katika jamii.

  “Mheshimiwa Spika, nimesimama kwa mujibu wa Kanuni ya 68 (7) na kwa kutambua ibara ndogo ya pili katika ibara ya 100 inayozungumzia kinga kwa mbunge kushtakiwa kuhusu jambo alilolitaja au kulitamka bungeni.

  “Lakini, pamoja na kutambua uhuru huo, jana (juzi) mmoja wa wabunge wenzetu ambaye ni Mheshimiwa Tundu Lissu, alifanya mkutano na waandishi wa habari na kuwashutumu baadhi ya wabunge na mimi mwenyewe nikatajwa kwamba tunahusika kuyatetea makampuni anayodai hayakupata zabuni ya kuuza mafuta.

  “Sasa nilichoona ni kwamba, kauli ya Tundu Lissu haikunitendea haki, kwa hiyo, nataka kuomba mwongozo wako, kwamba kauli ya Lissu aliyoitoa nje ya Bunge ina kinga au haina kinga?

  “Mheshimiwa Spika, naomba mwongozo wako ili uweze kutoa mwongozo wako kama ulivyopewa madaraka na Bunge ili jambo hili liweze kupelekwa kunakohusika.

  “Kauli ya Tundu Lissu imenidhalilisha na ni kauli ambayo haina chembe ya ukweli na kama haina kinga nitalazimika kwenda mahakamani ili aweze kwenda kuyathibitisha aliyosema.

  “Naomba kujua kama maneno yake yana kinga au hayana kinga kwa mujibu wa ibara hiyo, ili niweze kuchukua hatua zinazostahili, kwani amenidhalilisha mimi pamoja na wabunge wengine,” alilalamika Ole Sendeka.

  Kwa mujibu wa mbunge huyo, Lissu hakutenda haki, kwa kuwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, aliwatuhumu wabunge wa CCM na kumwacha wa Chadema, ambaye alisema anastahili kuchunguzwa.

  Juzi, Lissu alizungumza na waandishi wa habari mjini hapa na kuwataja baadhi ya wabunge wanaofanya biashara na TANESCO, wakiwamo ambao ni wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini na wenye mgongano wa kimaslahi na TANESCO na Kampuni za kuuza mafuta.

   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Anoother great episode
  Movie inaendelea
  Sakata la Ulimboka limepoa episode yake imepoteza mvuto sasa ni suala la bunge na rushwa
  Watanzania bana tunapelekwa kama upepo kusahau matukio na kwenye hiki kitengo cha kuanzisha matukio anafanya kazi yake vizuri sana maana akiona CD inachuja anaanzisha episode nyingine kuwasahaulisha ile iliyopita
  Mbona watu wana mcheheto sana si watulie waone Kamati ya Bunge ya Maadili inafanya nini
  Mbona wanahangaika sana kutaka kujipatia umaarufu wa bure na kutafuta kuonekana kweney luninga kuwa wamechafuliwa sana
  Au 2015 inakaribia na wanaona hawatarudi bungeni iwapo itathibitika ni kweli wamepokea rushwa
   
 3. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hahaa yaani Ole Sendeka kanuni za bungeni bado zinampiga Chenga mpaka leo?
   
 4. m

  manucho JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sendeka aga bunge na wabunge wenzako kwa sasa, muda wako unaisha sasa
   
 5. Mtumpole

  Mtumpole JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,444
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Huo muda wa kuzipitia KANUNI ZA BUNGE na kuzielewa ataupata wapi! Anaweza akajitetea ni umri!
   
 6. a

  afwe JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Janja ya nyani kula mahindi mabichi. Mh. Ole Sendeka alitumia ile kama nafasi kuuambia umma kuwa hayumo katika tuhuma zilizotajwa. Hakuwa na mahali pengine zaidi ya kutumia approach ile. Angeita press conference anajua maswali yangekuwa mengi na ni lazima angebainika kuwa anahaha tu wakati ni mmoja wao
   
 7. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kwa upande mwingine mama anajua moto wa Lissu, anamwogopa kama ukoma
   
 8. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ole sendeka inabidi awe mpole maana kama atuhumiwa asubiri upelelezi ndio utakuja na jibu
   
 9. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  awaulize wenzie akina kilango,sitta,mwakyembe kwa nini wamefyata kwa mamvi na kujiunga na kambi yake kiaina...mamvi ana nguvu kama za lucifer duniani hapa,hakuna dagaa yoyote wa ccm anayeweza kupambana naye jk included...makamanda wa ukweli wa cdm ndio wanaoweza kutaja jina lake kwa ubaya tu...
   
 10. d

  dguyana JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ole sendeka si angeita waandishi wa habari?
   
 11. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Au angemwambia hilo shauri liko mahakamani na haliwezi kutolewa mwongozo.

  It's Just Another Silly Session of the Silly Season.
   
 12. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #12
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Lissu kweli ni kiboko wa magamba wote manake hawezi kukurupuka tu kuongea anajua impact ya kuongea ovyo.
   
 13. m

  massai JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Huyo sendeka ana hela za tanzanite anazohongwa kila siku ili kuwabeba wazungu wanaovuna asilimali yetu.ukitaka kujua ni kweli angalia anavyokaa kimya kuzungumzia mererani wakati kunashida kuliko maelezo.mererani kunauzwa maji kama dar wakati kilomita kama thelasini kunamaji yanayozidi ziwa viktoria.shame on u sendeka.
   
 14. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #14
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,792
  Likes Received: 3,879
  Trophy Points: 280
  ole sendeka ni mwizi na fisadi namba moja tanzania nitakuja baadae na data zake
   
 15. W

  We know next JF-Expert Member

  #15
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Tunasubiri data OSOKONI
   
 16. Dickson Mpemba

  Dickson Mpemba JF-Expert Member

  #16
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 21, 2010
  Messages: 330
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  hii sheria ya kipumbavu sana kwa kweli tunahitaji katiba mpya ili tuondoe hizi sheria kandamizi no body is above the law, we are all human.
   
 17. mndwadage

  mndwadage JF-Expert Member

  #17
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 345
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unachoongea ni kweli kwanza tuondoe umungu mtu wa raisi mengine yatafuata.!
   
 18. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #18
  Aug 1, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,357
  Likes Received: 3,116
  Trophy Points: 280
  Mizengwe tupu.
   
Loading...