Spika kusema "hapa hakuna kupiga kura" ni kumuogopa rais? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika kusema "hapa hakuna kupiga kura" ni kumuogopa rais?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by .Daniel., Feb 10, 2012.

 1. .Daniel.

  .Daniel. Member

  #1
  Feb 10, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jana katika kikao cha bunge cha jioni spika alisema,kwa uendeshaji bora wa bunge suala lililozua mjadala juu ya nani ashirikiane na kamati maalum ya kukusanya maoni juu ya katiba mpya katika ngazi ya wilaya analipeleka kwenye kamati ndogo ya sheria ya bunge na kwamba katika hilo hakuna kupiga kura

  mgogoro wa kimawazo uliopo ni kwamba kambi rasmi ya upinzani inakubaliana na mapendekezo ya marekebisho yaliyoletwa na serikali ya kumtoa mkuu wa wilaya na kumuweka mkurugenzi nakwa upande wa pili wabunge wengi wa CCM wanayakataa marekebisho hayo ya serikali yao na kutaka mkuu wa wilaya aendelee kama ilivyo kwenye sheria.

  mzozo wa aina hii unamalizwa kwa kupiga kura kuamua juu ya marekebisho yaliyowasilishwa, kitendo cha spika kutotaka kura zipigwe ni kuwazuia wabunge kutekeleza wajibu wao wa kikatiba na kutaka kuwaamulia

  my take: nakubaliana na kambi rasmi ya upinzani ya kuwatoa wakuu wa wilaya na kuwaingiza wakurugenzi.ila hoja yangu ya msingi ni juu ya huu udhaifu mkubwa wa spika kwa serikali,juu ya hofu aliyonayo endapo bunge litakataa mapendekezo ya serikali ambayo yana mkono wa raisi.kitendo hiki ni hatari kwa taifa kwa kuwa spika anatumia wingi wa CCM bungeni kudhibiti hoja za upinzani na kuilinda serikali matokeo yake sheria mbovu zinapita na marekebisho mazuri yanapotaka kufanyika yanapata kikwazo kikubwa.
  wabunge wa CCM unafiki wenu leo unawalazimisha kula matapishi yenu.spika wenu anaogopa kile kinachoitwa 'uasi' kwa rais.leo ni lazima mchague kuasi au kula matapishi,mimi nawashauri mle matapishi kwa maslahi ya taifa isitoshe matapishi ni yenu wenyewe yaliyotokana na unafiki wenu.tunawasikiliza!
   
 2. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Kanuni za Bunge walizojiwekea nafikiri zinamruhusu Spika anaweza kufanya alivyofanya. Vinginevyo, ungesikia miongozo mingi inaombwa!
   
 3. Stanley.

  Stanley. JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Fahamu kwamba spika anaruhusiwa kuangalia uendeshaji bora wa shughuli za bunge. alichokifanya ni kutoa muda zaidi kwa jambo hilo kuzingatiwa na kamati ya bunge ya sheria na utawala ili wapate muafaka mzuri. hakukosea japokuwa majibu yaliyorudi ni kama yale yale kwani DC na DED wote watahusika.
   
 4. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  Makinda hana quality ya uspika ni mzigo kwa taifa hili!!
   
 5. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  c makinda tu hata mwanasheria mkuu naye alikuwa anaogopa ...ilifika kiipindi anna kilango anayejiita mpambanaji alipokuwa akichangia baada ya kumuona spika hasemi lolote kuhusu kupiga kura akawaamrisha vilaza wenzie wasimame nao wakasimama bila kufikiri lakini bado spika aliwakaushia wakakaa tena chini kilango alisema " eehe simameni simameni ndio tunaunga mkono hoja ndio"
   
 6. e

  ejogo JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Well done Madam speaker!
   
Loading...