Spika kumwita CAG kuhojiwa na Kamati ya Bunge: Nimeikumbuka kesi ya Hayati Mtikila na Mzee Mrema

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,196
25,516
Nawasalimu waungwana wa JF,

Tangu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Job Yustino Ndugai kumtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad ajitokeze mbele ya Kamati ya Haki,Maadili na Madaraka ya Bunge tarehe 21 mwezi huu, kumekuwa na mjadala mkubwa. Wito huo ni kumtaka CAG Assad 'akajieleze' juu ya kauli yake ya kusema Bunge ni dhaifu katika kuiwajibisha Serikali iliyotafsirika kama kulidharau na kulidhalilisha Bunge.

Wapo wenye mtazamo kuwa kikatiba na kisheria, CAG hawezi kuitwa na kuhojiwa Bungeni au mbele ya Kamati za Bunge (hivyobasi Spika hana mamlaka ya kumtaka CAG kujitokeza mbele ya Kamati tajwa). Wapo wenye mtazamo kuwa Bunge linaweza kumuita na kumhoji mtu yeyote ilimradi tu Katiba, Sheria na Kanuni za Bunge zinaruhusu hivyo. Siandiki hapa kwa ajili ya kujiunga na kundi lolote katika mitazamo hiyo. Nami naandika mtazamo wangu.

Iko wazi kuwa, katika tuhuma za kulidharau na kulidhalilisha Bunge, wapo waliowahi kuitwa na kuhojiwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na baadaye Bunge kufikia uamuzi. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na mwandishi nguli, kaka na mtani wangu Pascal Mayalla ni mifano ya walioitwa na kuhojiwa na Kamati tajwa ya Bunge kwa tuhuma zinazofanana na za CAG Assad.

Ndiyo maana, katika kufikiri Zaidi na Zaidi, nimeikumbuka kesi ya madai iliyounguruma Mahakama Kuu ya Tanzania kati ya Marehemu Mchungaji Mtikila na Mzee Augustino Mrema iliyokuwa mbele ya Jaji Barnabas Samatta (kama alivyokuwa). Jambo kubwa katika kesi hii ni uamuzi wa Mahakama Kuu kutenganisha kauli binafsi na zile za kiserikali. Niliwahi kujadili suala hili kwenye uzi huu:RC Makonda, umejiandaa? yasije yakakukuta ya Mrema mwaka 1991-1993 - JamiiForums

Wengi wetu tunajua kuwa, kikatiba, kila mtanzania ana haki ya kutoa maoni juu ya jambo lolote ilimradi tu asivunje Sheria. Mmoja wa watanzania hao ni CAG Prof. Mussa Assad aliyetoa maoni yake kuhusu uchambuliwaji,usimamiwajina utekelezaji wa Ripoti za CAG hasa zile zinazobeba ufisadi katika maeneo ya Serikali. Ingawa aliulizwa kama CAG, majibu yake yalikuwa ni binafsi kuhusu Bunge.

Kimsingi, maoni ya CAG Assad yalikuwa binafsi na hayakuwa maoni ya Ofisi ya CAG. Katika muktadha huo, na mantiki iliyojengwa kwenye kesi ya Mchungaji Mtikila niliyoitaja hapo juu, Bunge linamuita Prof. Assad kama aliyetoa maoni yake juu ya Bunge na utekelezaji wa Ripoti za CAG na si kama CAG au Ofisi ya CAG. Prof. Assad atakwenda Bungeni kama mtu binafsi. Kikubwa kwake ni 'kuthibitisha' kuwa Bunge ni 'dhaifu' katika kutenda alilolisema.
 
Nawasalimu waungwana wa JF,

Tangu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Job Yustino Ndugai kumtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad ajitokeze mbele ya Kamati ya Haki,Maadili na Madaraka ya Bunge tarehe 21 mwezi huu, kumekuwa na mjadala mkubwa. Wito huo ni kumtaka CAG Assad 'akajieleze' juu ya kauli yake ya kusema Bunge ni dhaifu katika kuiwajibisha Serikali iliyotafsirika kama kulidharau na kulidhalilisha Bunge.

Wapo wenye mtazamo kuwa kikatiba na kisheria, CAG hawezi kuitwa na kuhojiwa Bungeni au mbele ya Kamati za Bunge (hivyobasi Spika hana mamlaka ya kumtaka CAG kujitokeza mbele ya Kamati tajwa). Wapo wenye mtazamo kuwa Bunge linaweza kumuita na kumhoji mtu yeyote ilimradi tu Katiba, Sheria na Kanuni za Bunge zinaruhusu hivyo. Siandiki hapa kwa ajili ya kujiunga na kundi lolote katika mitazamo hiyo. Nami naandika mtazamo wangu.

Iko wazi kuwa, katika tuhuma za kulidharau na kulidhalilisha Bunge, wapo waliowahi kuitwa na kuhojiwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na baadaye Bunge kufikia uamuzi. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na mwandishi nguli, kaka na mtani wangu Pascal Mayalla ni mifano ya walioitwa na kuhojiwa na Kamati tajwa ya Bunge kwa tuhuma zinazofanana na za CAG Assad.

Ndiyo maana, katika kufikiri Zaidi na Zaidi, nimeikumbuka kesi ya madai iliyounguruma Mahakama Kuu ya Tanzania kati ya Marehemu Mchungaji Mtikila na Mzee Augustino Mrema iliyokuwa mbele ya Jaji Barnabas Samatta (kama alivyokuwa). Jambo kubwa katika kesi hii ni uamuzi wa Mahakama Kuu kutenganisha kauli binafsi na zile za kiserikali. Niliwahi kujadili suala hili kwenye uzi huu:RC Makonda, umejiandaa? yasije yakakukuta ya Mrema mwaka 1991-1993 - JamiiForums

Wengi wetu tunajua kuwa, kikatiba, kila mtanzania ana haki ya kutoa maoni juu ya jambo lolote ilimradi tu asivunje Sheria. Mmoja wa watanzania hao ni CAG Prof. Mussa Assad aliyetoa maoni yake kuhusu uchambuliwaji,usimamiwajina utekelezaji wa Ripoti za CAG hasa zile zinazobeba ufisadi katika maeneo ya Serikali. Ingawa aliulizwa kama CAG, majibu yake yalikuwa ni binafsi kuhusu Bunge.

Kimsingi, maoni ya CAG Assad yalikuwa binafsi na hatakuwa maoni ya Ofisi ya CAG. Katika muktadha huo, na mantiki iliyojengwa kwenye kesi ya Mchungaji Mtikila niliyoitaja hapo juu, Bunge linamuita Prof. Assad kama aliyetoa maoni yake juu ya Bunge na utekelezaji wa Ripoti za CAG na si kama CAG au Ofisi ya CAG. Prof. Assad atakwenda Bungeni kama mtu binafsi. Kikubwa kwake ni 'kuthibitisha' kuwa Bunge ni 'dhaifu' katika kutenda alilolisema.
Huwezi kutenganisha kauli za CAG anazozitoa zinazohusu mamlaka yake! Akilisema lolote,linalohusu kazi yake ni kauli ya ofisi ya CAG. Ulitaka atumie njia gani ili iwe kauli ya CAG? Waraka? Aliulizwa kama CAG, mwandishi alimtafuta na kumhoji CAG na si Assad! (ref to clip yake, tafuta clip uisikilize). Matamko ya Magufduli majukwaani yanakuwa matamshi ya Rais na si Magufuli wa Chato!
All in all, this is your reasoning!
 
Hivi kwani office ya CAG haina msemaji wake ili tumtofautishe Huyu Ustadhi na Office?
Mi naona inawezekana katafsiriwa vibaya ila anayo haki ya kutoa maoni yake kama mtanzania yeyote. Halafu Huyu sio wabkwanza kutuhumu muhimili mwinginee kwa udhaifu hata Mnyika aliwahi kulifanya hili
Hapa labda ije inshu ya immunity n.k
 
Nawasalimu waungwana wa JF,

Tangu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Job Yustino Ndugai kumtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad ajitokeze mbele ya Kamati ya Haki,Maadili na Madaraka ya Bunge tarehe 21 mwezi huu, kumekuwa na mjadala mkubwa. Wito huo ni kumtaka CAG Assad 'akajieleze' juu ya kauli yake ya kusema Bunge ni dhaifu katika kuiwajibisha Serikali iliyotafsirika kama kulidharau na kulidhalilisha Bunge.

Wapo wenye mtazamo kuwa kikatiba na kisheria, CAG hawezi kuitwa na kuhojiwa Bungeni au mbele ya Kamati za Bunge (hivyobasi Spika hana mamlaka ya kumtaka CAG kujitokeza mbele ya Kamati tajwa). Wapo wenye mtazamo kuwa Bunge linaweza kumuita na kumhoji mtu yeyote ilimradi tu Katiba, Sheria na Kanuni za Bunge zinaruhusu hivyo. Siandiki hapa kwa ajili ya kujiunga na kundi lolote katika mitazamo hiyo. Nami naandika mtazamo wangu.

Iko wazi kuwa, katika tuhuma za kulidharau na kulidhalilisha Bunge, wapo waliowahi kuitwa na kuhojiwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na baadaye Bunge kufikia uamuzi. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na mwandishi nguli, kaka na mtani wangu Pascal Mayalla ni mifano ya walioitwa na kuhojiwa na Kamati tajwa ya Bunge kwa tuhuma zinazofanana na za CAG Assad.

Ndiyo maana, katika kufikiri Zaidi na Zaidi, nimeikumbuka kesi ya madai iliyounguruma Mahakama Kuu ya Tanzania kati ya Marehemu Mchungaji Mtikila na Mzee Augustino Mrema iliyokuwa mbele ya Jaji Barnabas Samatta (kama alivyokuwa). Jambo kubwa katika kesi hii ni uamuzi wa Mahakama Kuu kutenganisha kauli binafsi na zile za kiserikali. Niliwahi kujadili suala hili kwenye uzi huu:RC Makonda, umejiandaa? yasije yakakukuta ya Mrema mwaka 1991-1993 - JamiiForums

Wengi wetu tunajua kuwa, kikatiba, kila mtanzania ana haki ya kutoa maoni juu ya jambo lolote ilimradi tu asivunje Sheria. Mmoja wa watanzania hao ni CAG Prof. Mussa Assad aliyetoa maoni yake kuhusu uchambuliwaji,usimamiwajina utekelezaji wa Ripoti za CAG hasa zile zinazobeba ufisadi katika maeneo ya Serikali. Ingawa aliulizwa kama CAG, majibu yake yalikuwa ni binafsi kuhusu Bunge.

Kimsingi, maoni ya CAG Assad yalikuwa binafsi na hatakuwa maoni ya Ofisi ya CAG. Katika muktadha huo, na mantiki iliyojengwa kwenye kesi ya Mchungaji Mtikila niliyoitaja hapo juu, Bunge linamuita Prof. Assad kama aliyetoa maoni yake juu ya Bunge na utekelezaji wa Ripoti za CAG na si kama CAG au Ofisi ya CAG. Prof. Assad atakwenda Bungeni kama mtu binafsi. Kikubwa kwake ni 'kuthibitisha' kuwa Bunge ni 'dhaifu' katika kutenda alilolisema.
Kuna mstari mwembamba sana Kati ya Prof Assad na CAG...Na yote yanaweza kuwa majibu sahihi.

Swali; Pale Ikulu alipoulizwa na Rais kuhusu zile trillion 1.5 alijibu kama Assad au CAG?
 
Kwa kweli maandiko yako nayasoma mara kwa mara, najifunza mengi sana kwenye maandiko yako, ila kwa leo reasoning yako ipo TOO NARROW. Ni ngumu kutenganisha kauli za Assad versus CAG. Nakupa homework tu, tangu JPM aingie madarakani, nitajie kauli zake 2 tu ambazo ni kauli binafsi amezitoa alipokuwa jukwaani.
 
Asante sana Mkuu kwa mchango wako
 
Back
Top Bottom