Spika, Katibu wa Bunge wampuuza Mnyika kuhusu uchaguzi wa wabunge wa Afrika Mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika, Katibu wa Bunge wampuuza Mnyika kuhusu uchaguzi wa wabunge wa Afrika Mashariki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Habarindiyohiyo, Apr 10, 2012.

 1. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Spika na Katibu wa Bunge wamempuuza mbunge wa Ubungo juu ya madai yake ya mara kwa mara kuwa kanuni za bunge zinapaswa kurekebishwa kabla ya uteuzi wa wagombea wa uchaguzi wa Afrika Mashariki. Mnyika amedai kwenye vyombo vya habari kuwa aliwasilisha mapendekezo mwezi Februari.

  Mnyika anadai kuwa kanuni za uchaguzi huo zinakasoro nyingi. Anadai pia kanuni hizo zinatoa kiti kimoja kwa upinzani badala ya viwili huku mwakilishi huyo wa upinzani akichaguliwa na wabunge wote wengi wao wakiwa wa CCM. Spika na Katibu wa Bunge wamempuuza kwa kuwa hajui kuwa CCM ndio chama kilichoshinda kwenye uchaguzi wa 2010 hivyo kina mamlaka ya kuamua ni wakina nani toka vyama gani wawakilishe Tanzania kwenye bunge hilo.

  .......ndiyohiyo
   
 2. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ni kawaida yao kuwapuuza wabunge wa upinzani lakini wao wakiwapuuza wananchi watawasikiliza mifano ipo,wao wakikaa kimya mawe yataongea
   
 3. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ningependa kukubaliana na Spika kwamba CCM kilishinda 2010. Ila anatakiwa ajiulize, ile imani (kama kweli ilikuwepo) ya wananchi kwa CCM ipo ile ile?
   
 4. h

  holowane Member

  #4
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wanasahau kwamba uchaguzi ule hawakushinda bali walichakachua. Pia wasisahau kwamba baada ya 2015 wao watakuwa chama cha ushindani na kanuni hizohizo kama hazitabadilishwa leo zitawaathiri wao vilevile na wasije kupiga kelele.
   
 5. N

  NICE LAMECK JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Itawauma sana pale watakapo kuwa wapinzani as soon.
   
 6. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,394
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Sheria na kanuni zote zinazotungwa ili kuwalenga/kuwakomoa watu fulani, baada ya muda huwageukia watunzi.
   
 7. K

  KWELI TUPU Member

  #7
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 17, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi nasemaaa, aliyeko juu subiri shuke kaaa hapo chini ya huo mti na njaa ikimzidi atashuka .. sasa kukamatana mashati kutaanzia hapo! Hizi kanuli ndo tutaanza nazo 2015 November baada ya wao magamba kufyata mkia!
   
 8. ossy

  ossy JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 877
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Tatizo la magamba wanadhani na kufikiri ya kwamba watatawala milele....hawasomi alama za nyakati
   
 9. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #9
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umesema kwamba wamempuuza, wamejibu vipi hoja zake hizi:

  JOHN MNYIKA: Turekebishe kwanza kanuni ndipo tufanye Uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki! kama hawajajibu bali wamempuuza tu ni dalili kuwa wamekosa majibu.

  Wao Spika na katibu wa bunge ndio wanastahili kupuuzwa, sisi wananchi tuendelee kujadili.

  serayamajimbo
   
 10. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #10
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Hawa jamaa upeo wao mdogo sana....hawajui kutafakari kabisa wako kichama zaidi
   
 11. B

  Bukutonaga JF-Expert Member

  #11
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 246
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  wewe waache waendelee kupuuza na wao wajue watakuwa wapinzani soon so hilo ni kaburi lao wanajiandalia pindi CDM au chama kingine kikiingia madarakani najua wataleta tena hoja hizihizi wanazozitia kapuni mda huu.

  MUNGU IBARIKI - TANZANIA
   
 12. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #12
  Apr 10, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  CCM madaraka yanawalevya wanasahau wananchi si wale wale kizazi hiki si chakudanganyika tena
   
 13. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #13
  Apr 15, 2012
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM ndio chama tawala, kinastahili viti vinane kati ya 9, upinzani halali yao ni nafasi moja ili kuwe na mwakilishi mmoja wa upinzani. Mbona hamlalamikii sheria zinazoiwezesha CCM kuteua mawaziri wote bila mpinzani hata mmoja? Iweje sasa mnataka marekebisho kanuni za Afrika Mashariki?

  ...ndiyohiyo
   
 14. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #14
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Supika na katibu wasome article 50 ya treaty inayoanzisha EAC, halafu wasome kesi ya Prof. Anyang Nyong'o , wakisoma hivyo na kutafakari Ndio watajua Kama kumpuuza Mh. Mnyika ni sahihi au la.
   
 15. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #15
  Apr 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu unaweza kutusaidia hiyo article 50 inasemaj?
   
 16. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #16
  Apr 15, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,951
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  mkuu dadavua hii kitu.
   
 17. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #17
  Apr 15, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Siku watakapokuwa chama cha upinzani ndiyo watajua msingi wa hoja.
   
 18. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #18
  Apr 15, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Nawezaje ipata hiyo kesi ya prof. Anyang Nyon'go. jina ni tamu kulitamka.
   
 19. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #19
  Apr 15, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Mkuu ungetuwekea hyo article ili tujue kilichomo ndani
   
 20. T

  T.K JF-Expert Member

  #20
  Apr 15, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 345
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Article 50 of the EAC Treaty provides that “the National Assembly of each partner state shall elect, not from among its members, nine members of the Assembly, who shall represent as much as it is feasible, the various political parties represented in the National Assembly, shades of opinion, gender and other special interest groups in that partner state, in accordance with such procedure as the National Assembly of each partner state may determin

  e.  Yeah! hi ilikuwa ni case ambayo wale apoointee wa Mwai kibaki walikuwa challenged mahakamani katika kesi iliyofunguliwa mahakama ya Africa Mashariki kama sikosei, na mahakama ikarule out kuwa taratibu za article ya 50 kilipuuzwa kwani mandate ya kuchagua wawakilishi wa bunge la EA liko mikononi mwabunge 100%....kwa hiyo ile hoja ya kusema eti kuwa chama kilichoshinda uchaguzi (kinachounda serikali) ndio chenye say yanani aende na nani asiende haina mashiko.....uwakilishi utakuwa based on idadi ya ya wabunge wa vyama vilivyoko bungeni na sio kwa kuwa influenced na serikali...bunge litakaporuhusu dola iifluence ni sawa na kujinyang'anya haki yake
   
Loading...