Spika Job Ndugai, sisi vijana sio wezi

Phazo Khan

Member
Aug 26, 2019
70
80
Mh Spika wa bunge la 12 Job Ndugai, mmegoma kutoa ajira kwa vijana, mmeacha kutunga sera/shera nzuri ambazo zinaweza kuvutia uwezekaji mkubwa na kuleta ajira kwa vijana, mmeacha kupitsha sheria ambazo zitamruhusu kijana kupata mkopo ambao unaweza kumkwamua,

Mwisho wa siku unakuja kutuchongea kwa wadosi kuwa vijana hawana uaminifu, vijana wasipoiba wanajiona wajinga na mazonge mengi mengi tu.

Mh Spika sisi vijana sio wezi na uaminifu tunao, ukitaka usiibiwe basi mlipe kijana ako vizuri tu na mjengee mazingira mazuri ya uaminifu.

Kwakumalizia Mh Spika kauli kama hizo tena kwa kiongozi mkubwa wa mhimili wa nchi, naona sio nzuri sana vinaharibu na kuchafua taswira ya vijana.
 
Kwanza yeye hata hapo alipo tu anajiona ni safi kuanzia ujana wake mpaka alipofikia? Alianza na boda boda anaendelezea na kutuchafua vijana nchi nzima na aendelee kujua hao vijana wasio waaminifu wao ndiyo chanzo na umimi wao wa kujilimbikizia kila kitu wao na misheria yao wanayopitisha sijui kwa manufaa ya nani afu wanakuja kusema vijana siyo waaminifu.
 
Hivi tuwe wakweli kabisa, Spika anayeapisha wabunge wasiokuwa na chama akijua kabisa kuwa anavunja Katiba anapata wapi moral authority ya kukemea wengine juu ya uadilifu na uaminifu?
20210415_112529.jpg
 
Wizi ni tabia ambayo mtu au watu wanaiona.

Kuna mambo ya kukosa uadilifu/uaminifu unafanywa kwenye jamii na hata baadhi ya sekta/ofisi za serikali na watu wazima au vijana ni tunakumbuka machache miaka ya nyuma vyombo vya habari vimekua vikiandika sana kuhusu masuala ya "upigwaji" ambapo tukipima tutaona hii ni matokeo ya kukosekana kwa uaminifu katika taasisi za umma na ukifanywa na baadhi ya watendaji hasa wakubwa kwa vyeo na umri. Na tujibukubushe baadhi ya kashfa ambazo wahusika wa kukosa uaminifu hawakuwa vijana bali ni watu wazima wenye heshima zao
sekeke la EPA pale BoT
TEGEGA ESCROW pale BoT
RICHMOND na ndugue Dowans
Kagoda, Meremeta;
Wafanyakazi hewa kulipwa mshahara na huku kila mwaka CAG alikuwa aki-report
Wawekezaji (wazungu au Indians) kutupiga, rejea Makinikia/Bart Airtel kutupiga kwenye kampuni ya simu toka enzi ya Tritel na mikataba mibaya iliyopitishwa bungeni kwa hati ya dharura au wingi wa wabunge wa CCM wakati fulani;
rushwa polisi barabarani au polisi ili kupata dhamana
rushwa uhamiaji ili kupata pasi za kusafiria au vibali cha ukazi
rushwa idara ya kazi ili kupata vibali vya kazi kwa wageni
rushwa NEMC ili kupata vyeti (Environmental impact assessment)
rushwa mahakamani ili kupata dhamana
rushwa za ngono vyuo vikuu na baadhi ya maafisa utumishi
rushwa idara ya ardhi kwenye halmashauri au wizarani
bashasha kwa wanahabari ili story iende hewani
rushwa studio ili msanii nyimbo zake zipigwe
rushwa kwa ma-super star wa film ili msanii chipukizi apate platform
rushwa kwa maafisa wa mifuko ya jamii ili mstaafu apate haki yake
rushwa za ngono ili wanafunzi kupata mikopo ya bodi
Twiga kuondoka nchini kwa ndege ya jeshi toka nchi moja hivi
rushwa kuungiwa umeme kinyemela kwa kutumia vishoka wa Tanesco miaka ya nyuma.
rushwa kupata TIN certificate kwa kutumia vishoka huko nyuma
Tembo kuuwawa na pembe kutoroshwa kupitia mufumo rasmi ikiwemo bandari
undugunization kwenye ajira, rejea sekeseke la uhamiaji miaka ya nyuma watoto wa "wakubwa wa uhamiaji" kupendelewa
sakata la BoT kuajiri watoto wa wakubwa miaka ya nyuma kwa level ya form IV tu; tunajua baadae walijiendeleza lakini hasa wale walioamua.
bandarini miaka ya nyuma mtu yeyote alieajiriwa hata messenger tu, ilionekana kama ni taasisi yenye "neema" kumbe ni ma-deal

Sina maana ninaunga mkono upigwaji unaofanywa na vijana wakiajiriwa; sio sawa kujenga jamii ya wezi maana itakuwa tabu sana.

Uki-scan jamii yetu Tanzania au Africa maana tunatembea hata nchi zingine ukienda za SADC ni halali kuingia ila bila dola 50 kwenye passport maafisa wanazingua.

Rushwa/bahasha/ma-deal ndio msingi wa kukosekana uaminifu na uadilifu. Kama vijana wanaona wazee wao wanapiga, ndio watoto wa mjini wanasema kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake.

Viongozi wa dini hawatakuwa na msaada sana pale wanapo-deal na maafisa wa serikali ambao baadhi yao hata kura walipata kwa "kuwaweka sawa wajumbe".

Yote haya ni ishara ya mmomonyoko wa maadili ambao ni nani asie "mwizi/mpigaji" ili awakemee wengine jamani acheni?

Yesu akasema, yeye asie na dhambi, awe wa kwanza kumtupia jiwe yule mwanamke aliekutwa "akila uroda"; cha ajabu wale wanaume mwanaume mwenzao walimwacha na kumpeleka mwanamke, kosa la kwanza. Walipojikagua nafsi zao na kujiona sio wasafi "wakalala mbele"

It takes effort kujenga taifa la watu waadilifu na waaminifu; tusiwalaumu vijana pekee, tujirekebishe jamii yote.
 
Vijana wenyewe wamewa nyooshea wazee waliyopewa dhamana,kuongoza taasisi mbali mbali za serikali,maana siyo kwa mishindo hiyo

Ova
 
Ndugai ana hoja ya msingi tu, sio vyema kushambuliwa! Vijana wengi wakipewa Ajira hawana uaminifu, I speak from experience! Unasema kijana alipwe vizuri na kujengewa mazingira ya uaminifu uko sahihi lakini kumbuka kijana huyu anaingia makubaliano ya kazi kwa ujira kadhaa, kama ujira hautoshi ni vyema akaangalia sehemu nyingine yenye mshahara atakaoona unamfaa!

Bahati mbaya sana vijana wengi wana haraka ya maendeleo; kijana anataka akimaliza shule leo basi ndani ya muda mfupi awe na nyumba na gari. Anajilinganisha na mtu mwenye miaka 40 ambaye yupo kazini miaka 10 plus. Tusimlaumu tu Ndugai, kweli uaminifu ni tatizo sio tu kwa vijana Bali kwa makundi yote pamoja na hao wanasiasa!
 
Ndugai ana hoja ya msingi tu, sio vyema kushambuliwa! Vijana wengi wakipewa Ajira hawana uaminifu, I speak from experience! Unasema kijana alipwe vizuri na kujengewa mazingira ya uaminifu uko sahihi lakini kumbuka kijana huyu anaingia makubaliano ya kazi kwa ujira kadhaa...
Hoja yake ni nzuri ila tu kama angetumia maneno tofauti na aliyoyasema. Unajua unapotoa kauli za shutma tena kwa kiongozi wa ngazi yake, haileti afya njema kwenye mazingra ya vijana ukizingatia soko la ushindani wa ajira ni gumu sana
 
Wizi ni tabia ambayo mtu au watu wanaiona.

Kuna mambo ya kukosa uadilifu/uaminifu unafanywa kwenye jamii na hata baadhi ya sekta/ofisi za serikali na watu wazima au vijana ni tunakumbuka machache miaka ya nyuma vyombo vya habari vimekua vikiandika sana kuhusu masuala ya "upigwaji" ambapo tukipima tutaona hii ni matokeo ya kukosekana kwa uaminifu katika taasisi za umma na ukifanywa na baadhi ya watendaji hasa wakubwa kwa vyeo na umri...
Asee umeifafanua vizuri sana...kumbe hizo mambo za wizi zipo kuanzia ngazi za juu kabisa, ila tu Mh kaona wizi wa bukubuku kwa vijana.

Tukianza kukemea wizi basi viongozi wetu nao hawana budi ya kuachana na mipango ya upigaji,

Personally, mekuelewa sana
 
Kuna mwingine nimemuona analalamika sana kuwa vijana hatuna nguvu za kiume, sasa sijui huu utafiti aliufanyia kwa vijana wangapi, mikoa mingapi mpaka akaenda kusema bungeni kuwa vijana hawana nguvu za kiume.

Hili bunge kwa aina ya wabunge waliopo sidhani kama wana uwezo wa kutosha kuishauri serikali, kutunga sheria na kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora. Wengi wao uwezo wa kuangalia maslahi ya nchi na watu wake ni mdogo mno kiasi cha kupiga porojo na kusozana.

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Halafu anae yasema hayo n mbunge wa viti maalumu, anatufanya watu tufikirie vingi, ikiwemo tabia zake binafsi, mana kitendo cha kusema vijana hawana nguvu za kiume, ye kama wa jinsi ya kike amejuaje?

Viongozi wetu walio wengi wamekosa weledi
 
Back
Top Bottom