Spika Job Ndugai na Naibu wake wajiuzulu kwa kushindwa kusimamia na kuliongoza Bunge

Fundi Madirisha

Senior Member
Jun 30, 2020
184
987
Wasalaam wana wa Adam,

Kwanza kabisa napongeza sana hotuba nzuri ya leo ya Mhe Rais Mama yetu Samia Suluhu Hassan, ni maneno mazito sana ambayo yamelisuta bunge letu la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Unaposutwa kubali kuwa unakosea sana na unachokifanya hakifai hata kuigwa na yeyote yule.

Rais wetu amesema kuwa bunge limeacha kazi zake za kujadili mambo ya kitaifa na matokeo yake limegeuka kujadili mambo yasiyo na Afya kwa taifa. Hakika haya ni maneno mazito sana kwa wanaoendekeza tabia za hovyo hovyo kama hizo. CAG Mstaafu Prof Assad aliposema kwamba bunge letu ni dhaifu nadhani sasa maneno yake yanaishia. Aliadhibiwa kwa sababu ya watu wachache kutotaka kuambiwa ukweli.

KWANINI SPEAKER NDUNGAI NA NAIBU WAKE WANATAKIWA KUJIUZULU NAFASI ZAO?
Ni wazi kabisa kua maneno ya Mama yamedhibitisha kwamba kuna udhaifu mkubwa sana wa usimamizi na uendeshwaji wa shughuli za bunge, Speaker na naibu wake wasingerndekeza mijadala hii wala tusingefika mahali tupo hivi sasa. Ndungai na naibu wake watalaumiwa sana kwa kushindwa kulisimamia na kulidhibiti bunge hali iliyosababisha mpaka sasa linaonekana kugawanyika.

Hakika huu ni udhaifu mkubwa sana usiovumilika. Kama walipendekeza mambo yasiyokuwa na Afya kwa taifa mpaka kupelekea mkuu wa nchi kuonea maana yake waliunga mkono mambo haya. Hakuna lingine zaidi hawa viongozi kujiuzulu kwa maslahi ya taifa na bunge lenyewe. Raia hatutakubali tutalipigia kelele hili mpaka waondoke wanatuharibia taifa hawa.

USHAURI KWA MHE RAIS
Mhe Rais kauli zako zimeeleweka Mama kua ni za kujenga na kutuweka pamoja asante sana. Mhe Rai, bado wiki moja uthibitishe kua Mwenyekiti wa CCM taifa, ninakuomba sana ingawa bunge ni mhimili mwingine lakini wewe ndiye Rais na mwenyekiti wa CCM anayesubiri kuthibitishwa tu, utajua namna ya kupanga safu yako. Kama speaker na Naibu wake hawatakubali kuwajibika, wewe ni mwenyekiti chama na waziri mkuu ni katibu wa wabunge wa chama hakuna kitakachoshindikana. Wapo wazee Wangu akina Zungu,na wengine wenye busara na uelewa wanaweza kuendesha bunge na kulisimamia vizuri.

Mwisho ninkulitakia mema taifa langu na kuombea umoja na mshikamano.
 
Juzi wakati Job Lusinde akichangia hoja Bungeni, aliishia kuwakejeli na kuwadhalilisha Wasomi waliopo mle Mjengoni na nje ya Bunge.

Chakushangaza ni kwamba nilimuona Mh Waziri Mkuu akigonga meza kuashiria kuwa anakubaliana na Kibajaji.

Hivyo basi Bunge la Ndugai ni la hovyo kabisa kuwahi kutokea. Bado kitambo kidogo Mama kumuumbua kuhusiana na wale Wabunge covid-19.
 
Juzi wakati Job Luside akichangia hoja Bungeni, aliishia kuwakejeli na kuwadhalilisha Wasomi waliopo mle Mjengoni na nje ya Bunge. Chakushangaza ni kwamba nilimuona Mh Waziri Mkuu akigonga meza kuashiria kuwa anakubaliana na Kibajaji.

Hivyo basi Bunge la Ndugai ni la hovyo kabisa kueahi kutokea. Bado kitambo kidogo Mama kumuumbua kuhusiana na wale Wabunge covid-19.
Waziri Mkuu huyu kwa ubovu anazidiwa na Sumaye pekee tangu tupate Uhuru.
 
Back
Top Bottom