Dalili zipo wazi kuwa kuna siri kubwa kwenye mikopo inayofanyika chini ya Ccm ya mama Samia. Hasa huu mkopo wa tril 1.3 huenda una mruerue kibao ambayo yana siri kubwa.

Ila mbali na hayo bunge kutaka kudhibiti ufisadi na kumweleza ukweli rais Samia imekuwa kero kwake.

Mwaka 2025 kama Samia akigombea urais, wananchi watamkataa
Hatogombea
 
"Power is always dangerous, it attracts the worst and corrupts the best" ~ Ragnar (The Vikings)
 
Tujue kama ilikua ni katiba au ni utashi wake huyo job ndugai nae pia itapendeza kama aitwa na kamati ile ya waua paka kama alivyowafanyia wenzie akiwepo member mwenzetu hapa jukwaani paskal mayalla.

Ili nae aonje utamu wa kutolewa jasho na ile kamati ya vingunge,

Nitafurahi huyo spika ajaye haraka sana amuite tujue alikuwa amelewa au ana akili timamu.

Kumbe ni kweli bunge lilikuwa dhaifu!
 
Tujue kama ilikua ni katiba au ni utashi wake huyo job ndugai nae pia itapendeza kama aitwa na kamati ile ya waua paka kama alivyowafanyia wenzie akiwepo member mwenzetu hapa jukwaani paskal mayalla...
Naunga mkono hoja na akikaidi kuitiki wito afuatwe kama alivyokuwa anawafanyia wenzie.Serikali ina mkono mrefu.
 
Tujue kama ilikua ni katiba au ni utashi wake huyo job ndugai nae pia itapendeza kama aitwa na kamati ile ya waua paka kama alivyowafanyia wenzie akiwepo member mwenzetu hapa jukwaani paskal mayalla...
Unataka m-CCM mwenzio aanze kulia kwa mtindo wa mayowe?
 
Power is only given to those who are prepared to lower themselves to pick it up.

We should never be like Horses, Sheeps, Nyumbu who follow the herd in front of us without thinking recognize and realize our collective power to effect, affect and change things.

We have brain for a reason.
 
Job Ndugai wiki hii ameweka historia ya kuwa Spika wa kwanza wa Bunge la Tanzania kujiuzulu wadhifa huo.

Ingawa barua yake ya kujiuzulu wadhifa huo ilieleza sababu ya kufanya hivyo kuwa ni "uamuzi binafsi uliozingatia maslahi mapana ya Bunge, Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM)" lakini ni wazi kwamba kilichoharibu kila kitu ni kuzorota kwa uhusiano wake na Rais Samia Suluhu Hassan katika siku za karibuni.

Kwa waliomfahamu Ndugai, anajulikana kama mwanasiasa ambaye ndoto yake kubwa ilikuwa kuja kuwa Spika wa Bunge la Tanzania. Ndoto yake hiyo hatimaye ilitimia miaka 15 baada ya kuingia bungeni kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000.

Hii, kwa vyovyote vile, haikuwa namna ambayo alitaka kumaliza muda wake wa Uspika.
Hata hivyo, mfululizo wa matukio, kukosea mahesabu ya kisiasa na sadfa (coincidence) za kimaisha, ndiko hatimaye kumehitimisha maisha yake ya ukuu wa mhimili huu wa dola.

Ili kufahamu ilikuwaje Ndugai akapanda kutoka kijana kutoka familia masikini ya Kongwa, Dodoma na kuja kuwa mkuu wa mhimili wa mmojawapo wa dola na mmoja wa wanasiasa watata Tanzania - ni muhimu kwanza kupata historia yake.
 
Back
Top Bottom