View attachment 2071031
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo Januari 06, 2022 ikiwa ni siku chache tangu kusambaa kwa video ambayo alinukuliwa akisema ipo siku Nchi itapigwa mnada kutokana na madeni

Amesema ameandika Barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM na uamuzi huo ni binafsi na hiari, na ameuchukua kwa kuzingatia maslahi mapana ya Nchi, Serikali na Chama

#JamiiForums

Mbunge wa Kongwa (CCM), Job Ndugai tarehe 10 Novemba 2020, alichaguliwa kuwa Spika wa Bunge la 12 baada ya kupata kura 344 kati ya kura 345 zilizopigwa sawa na asilimia 99.7. Kura moja ilimkataa. Ndugai alikuwa spika katika Bunge la 11 la 2015 - 2020.

Hapo awali akizungumza 28 Desemba 2021 katika mkutano mkuu wa pili wa wanakikundi cha Mikalile Ye Wanyusi uliofanyika jijini Dodoma, Ndugai alitetea uamuzi wa Bunge kuanzisha tozo za miamala ya simu, kuliko kuendelea kukopa kwani ipo Siku Nchi itapigwa Mnada

“Juzi mama ameenda kukopa 1.3 trilioni. hivi ipi bora. Sisi Watanzania wa miaka 60 ya uhuru kuzidi kukopa na madeni au tubanane banane hapa hapa, tujenge wenyewe bila madeni haya makubwa makubwa haya yasiyoeleweka. Ni lini sisi tutafanya wenyewe ‘and how’ (na kwa vipi),” alisema Spika Ndugai.

Job Ndugai alihoji wanaofurahia nchi kukopa na kwamba deni limefika Sh70 trilioni - Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

RAIS SAMIA ASHANGAZWA NA SPIKA NDUGAI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alieleza kushangazwa na kauli za Spika wa Bunge Job Ndugai kusimama hadharani na kukosoa mkopo wa Shilingi Trilioni 1.3 kutoka shirika la Fedha Duniani (IMF) wenye lengo la kuchochea mapambano dhidi ya UVIKO -19 wakati taarifa mbalimbali zinapitia kwenye bunge lake.

Akizungumza Jumanne Januari 4,2022 Jijini Dar es salaama wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ikiwemo elimu, afya,maji na miundombinu, Rais Samia alionyesha kukerwa na kile alichokisema Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu Serikali kukopakopa badala ya kujiendesha kwa pesa za ndani.

“Huwezi kufikiria mtu mliyemuamini, mshika mhimili, aende akasimame aseme yale. Ni stress ya 2025. Inashangaza kuona mtu mwenye uelewa, anasema kuna fedha ya tozo lakini kaenda kukopa, ya nini? Au kwa nini tunaendelea kutoa tozo wakati fedha ya mkopo ipo. Mawaziri tupeni hizo takwimu sasa hivi.

"Mtu na akili yake anasimama na anahoji kuhusu mikopo na tozo, sio lolote ni homa ya 2025, kwa mtu ambaye nilimtegemea kushirikiana naye kwenye maendeleo, sikutegemea kama angesimama na kusema maneno hayo. Huwezi kufikiria mtu mliyemuamini, mshika mhimili, aende akasimame aseme yale. Ni stress ya 2025", alisema Rais Samia.

Soma: Rais Samia amvaa Ndugai. Asema, "Huwezi kuamini mtu mzima ana-argue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3"

Kwa mujibu wa taarifa yake kwa umma, Ndugai amesema kuwa amemuandikia barua Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kujiuuzulu nafasi hiyo ikibainisha kuwa uamuzi huo wa kuachia nafasi hiyo ameufanya kwa hiari.

“Naomba kutoa taarifa kwa uma wa watanzania kuwa leo Tarehe 06 Januari 2022 nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri wa wa Tanzania” imesema sehemu ya taarifa hiyo nakuongeza

“Pia nakala yangu hiyo ya kujiuzulu nimewasilisha kwa katibu wa Bunge
View attachment 2070821

======

WASIFU

Job Yustino Ndugai (58) ni mwanasiasa kutoka Tanzania ambaye anahudumu kama Spika wa Bunge tangu mwaka 2015. Kabla ya hapo alihudumu kama Naibu Spika wa Bunge tangu mwaka 2010.

Alizaliwa Januari 21, 1963 alipata elimu ya msingi kutoka Shule ya Msingi Mtare kuanzia mwaka 1991-1997. Alianza elimu ya Sekondari ya Kibaha mwaka 1978-1981 na kumalizia Shule ya Sekondari Old Moshi kuanzia 1982-1984.

Amesoma Stashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha Mweka kuanzia mwaka 1986-1988, kisha Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1989-1993).

Amesoma Post Graduate kutoka Chuo cha Kilimo nchini Norway kuanzia 1994-1995 na kusoma Shahada ya Umahiri kutoka chuo hicho (1995-1996).

Safari yake ya elimu iliishia Eastern and Southern African Management Institute ambapo alisoma Shahada ya Umahiri katika Usimamizi wa Biashara (2005-2008)

Amekuwa mbunge wa Kongwa kwa miaka 21 sasa (tangu mwaka 2000) na ameshika nafasi mbalimbali ndani ya kamati za bunge.

Alichaguliwa kuwa spika wa bunge Novemba 17, 2015 baada ya kupata kura 254 kati ya 365, na mpinzani wake Goodluck Ole Medeye kutoka CHADEMA akipata kura 109, huku kura mbili zikiharibika.

Mbali na ubunge, amefanya kazi sehemu nyinginezo ikiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Pori la Akiba Selous na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).

Januari 6, 2022 amejiuzulu nafasi ya Uspika kutokana na sababu binafsi na kwa hiari yake.

Ndugai ni mume wa Fatuma Mganga.

=====

UPDATES

=====

Taarifa kutoka kwa katibu wa bunge kuhusu kujiuzulu kwa spika wa bunge
View attachment 2071339
View attachment 2071346
Hatimaye Job Ndugai abwaga manyanga

View attachment 2070772
Kwani katibu wa Bunge anapokea nakala au ndiye mhusika mkuu? CHECHEMEA party
 
Ameomba kwa chama chake kwanza , kama chama kikiridhia basi atakubaliwa na atapewa barua ya chama na hatua zingine kuendelea
 
Kama mnampenda sana Ndugai, mwambieni arudishe kadi ya CCM, na kwenye kikao kijacho cha Bunge, agombee tena u-spika kama Private Candidate na sio kama mwakilishi wa chama... haya mambo simple sana!!!
 
Ndugai hajaandika barua ya kujiuzulu uspika kwenda kwenye Ofisi ya Bunge, bali kaandika kwenda kwenye chama CCM. Bunge haliwezi kufanyia nakala ya barua hio kazi maana halina mamlaka hayo kikatiba.

Kwa msingi huo, bado ni spika kikatiba.

Ndugai aandike barua nyingine kwenda Ofisi ya Bunge ndio atakuwa amejiuzulu.
Hakuna utaratibu wa kikatiba wa namna ya spika kujiuzulu. Kwanza katiba yenyewe haitaji kama spika anaweza kupoteza nafasi yake kwa kujiuzulu, Soma Katiba kifungu cha 84 kuanzia kifungu kidogo cha 7(a) Nakinukuu kwa manufaa yetu sote:

(7) Spika atakoma kuwa Spika na ataacha kiti cha Spika

litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo -

(a) iwapo mtu huyo alichaguliwa kutoka miongoni mwa

Wabunge, basi ikiwa atakoma kuwa Mbunge kwa

sababu yoyote ambayo haihusiki na kuvunjwa Bunge;

au

(b) ikiwa kutatokea jambo lolote ambalo, kama

asingekuwa Spika, lingemfanya mtu huyo asiwe na

sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi wa

Spika; au

(c) Bunge litakapokutana kwa mara ya kwanza baada ya

Uchaguzi Mkuu uliofanywa baada ya Bunge kuvunjwa,

lakini masharti ya aya hii yatatumika bila ya kuathiri

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara ya 90 ya

Katiba hii; au

(d) ikiwa mtu huyo ataondolewa kwenye madaraka ya

Spika kwa azimio la Bunge lililoungwa mkono na

Wabunge amabo idadi yao haipungui theluthi mbili ya

Wabunge wote; au


(e) ikiwa mtu huyo atashindwa kuwasilisha kwa Rais

tamko rasmi kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo

(5) ya ibara hii; au

(f) ikiwa mtu huyo atapatikana na hatia kwa kosa la kutoa

habari za uongo, kwa kiapo kinyume cha sheria ya

Kanuni ya jinai, kuhusu tamko rasmi lolote lililotolewa

kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) ya ibara

hii; au

(g) ikiwa mtu huyo atashindwa kuwasilisha kwa Rais

taarifa ya mali kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo

ya (5) ya ibara hii kabla ya kumalizika muda uliowekwa

kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliotungwa na

Bunge;

(h) ikiwa itathibitika kuwa mtu huyo amevunja masharti ya

Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
 
Binafsi sioni kosa la Spika Job Ndugai, ni mbunge kazi yake ni kushauri, kukosoa, kusimamia , kutunga Sheria, kupitisha Bajeti na mikopo zikiwemo sio kupokea maagizo ya Serikali, kusifia au kuwa praise team wa Serikali
 
Ndugai alikuwa kinara wa kumshughulikia CAG Prof Asaad kwa kusema kuwa Bunge ni dhaifu lakini mwisho wa siku yeye mwenyewe Ndugai kadhihirisha maneno ya Assad baada ya kujisubmit kwa Rais na kuomba msamaha kwa kauli ambayo haikuwa na tatizo lolote. Matokeo yake ni kilichompata sasa
 
imetoa funzo kuwa waafrika huwa tunatumika tu kama tambala na kutupwa huko, swala la spika kujihuzuru kisa ametoa maoni yake ni udikteta wa hali ya juu sana.
Cha kushangaza si bbc, Dot welle ya ujerumani ,chadema, Act wazalendo wala Ulimwengu waliokemea udikteta huu!.
Kama ingekuwa ni kipindi cha Magufuli ungeona ambavyo mishipa imewatoka kukemea udikteta kisa tu alikuwa anawabananga kwelikweli kwenye ulaji wao, leo kwa kuwa rais Samia amewaachia wale jinsi wanavyotaka basi wako kimyaaa wanakenua meno kana kwamba hawaoni kuwa kama kiongozi wa mhimili kama bunge anaweza kufukuzwa kwa kutoa maoni je wewe kikaragosi wa Maswa ndani ndani itakuwaje?
Kipindi cha Magufuli hata kufukuza watumishi hewa waliita ni udikteta.
Mazuzu yameungana kushangilia sasa hao uliowataja watakemea vipi?
 
imetoa funzo kuwa waafrika huwa tunatumika tu kama tambala na kutupwa huko, swala la spika kujihuzuru kisa ametoa maoni yake ni udikteta wa hali ya juu sana.
Cha kushangaza si bbc, Dot welle ya ujerumani ,chadema, Act wazalendo wala Ulimwengu waliokemea udikteta huu!.
Kama ingekuwa ni kipindi cha Magufuli ungeona ambavyo mishipa imewatoka kukemea udikteta kisa tu alikuwa anawabananga kwelikweli kwenye ulaji wao, leo kwa kuwa rais Samia amewaachia wale jinsi wanavyotaka basi wako kimyaaa wanakenua meno kana kwamba hawaoni kuwa kama kiongozi wa mhimili kama bunge anaweza kufukuzwa kwa kutoa maoni je wewe kikaragosi wa Maswa ndani ndani itakuwaje?
Kipindi cha Magufuli hata kufukuza watumishi hewa waliita ni udikteta.
Tena kama machadema ndio bure kabisa!
.
Huwezi amini kama Lema leo hii anashangilia bunge kubanangwa namna hii
 
imetoa funzo kuwa waafrika huwa tunatumika tu kama tambala na kutupwa huko, swala la spika kujihuzuru kisa ametoa maoni yake ni udikteta wa hali ya juu sana.
Cha kushangaza si bbc, Dot welle ya ujerumani ,chadema, Act wazalendo wala Ulimwengu waliokemea udikteta huu!.
Kama ingekuwa ni kipindi cha Magufuli ungeona ambavyo mishipa imewatoka kukemea udikteta kisa tu alikuwa anawabananga kwelikweli kwenye ulaji wao, leo kwa kuwa rais Samia amewaachia wale jinsi wanavyotaka basi wako kimyaaa wanakenua meno kana kwamba hawaoni kuwa kama kiongozi wa mhimili kama bunge anaweza kufukuzwa kwa kutoa maoni je wewe kikaragosi wa Maswa ndani ndani itakuwaje?
Kipindi cha Magufuli hata kufukuza watumishi hewa waliita ni udikteta.
Uandishi wako ni mbovu sana!!
 
Hili sijambo lakawaida kwakuwa ni jipya nadhani ipo haja ya kuliangalia kwa mapana yake kunani TZ.
Kama kwenu Tanzania halijatokea huko nchi nyengine je huwezi kujifunza? au unaishi dunia ipi wewe

Kuwajibika ni jambo la kawaida sana ukifanya uzembe na ujinga kwenye wajibu wako., ni kutunza heshima yako isimalize kabisa kabisa, unataka mtu akae madarakani ata akifanya nini wakati kuna mamilioni ya watu wanamatumaini yao mbali mbali kwa nchi yao
 
Lile soko pale Idodomya bado linasomeka kwa jina lake?
Nashauri lile jina pale lifutwe haraka sana lisije nalo kuporomoka tukaingia hasara wajameni
 
1641546204984.jpeg
 
Back
Top Bottom