Spika huadhibiwa kwa utaratibu gani?

SubiriJibu

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
1,788
1,821
Thinkers,

Nimeshuhudia thread nyingi zikitafakari mwenendo spika Anne Makinda utakavyokuwa na hakika wasiwasi ni mwingi kama ilivyo kawaida kwa kitu kipya.

Wapo wanaolalamika tu kama vile spika yuko juu ya kila kitu na kama vile hata akivunja kanuni ya bunge hakuna jinsi ya kumwadabisha au kumwajibisha.

Bado siamini kama hali ni hivyo, eti spika yuko juu ya sheria na kanuni. Nadhani ni ujinga wangu tu kutojua jinsi ya kumdhibiti spika kwa mujibu wa kanuni za bunge, ikibidi sheria za nchi na ikibidi sheria za kimataifa.

Tumeona kanuni zikimsulubu mbunge kama Zitto Kabwe. Ni sahihi. Je, hali inakuwaje ikithibitika kwamba spika ametumia ubabe kuvunja kanuni bungeni?

Naamini akitumia ubabe ule kwa mbunge wa CCM anaweza kutetewa na chama chake watakapokaa chamani kwao, tena yule mbunge anaweza kushughulikiwa ajifunze adabu!

Lakini utaratibu ninaoudadisi ni kwa manufaa ya wabunge wa upinzani ambao huwezi kuwatisha kwa kuitana chamani na hivyo silaha yao pekee ni utaratibu wa kumwadabisha spika.

Nisisitize kwamba suala la nidhamu ya kanuni si suala la hoja kupitishwa au kukataliwa bungeni kwa kupigiwa kura. Spika akiua basi yeye kama raia amevunja sheria ya nchi na ananyongwa kwa sheria hiyohiyo ya nchi bila kujali mle bungeni kuna ana wabunge 100% wa chama chake.

Hivyo hata akivunja kanuni basi lazima awajibike kwa uvunjaji ule, kwani kura za CCM bungeni si za kusafisha utovu wa nidhamu ya kanuni au sheria.

Tusijikute tumemfanya spika kama mtu asiyeguswa kama asivyoguswa rais aliyeko madarakani na walau sheria iko wazi kwa rais kutoguswa kuliko spika.

Wenye uelewa tusaidieni kujadili na hili.

Na wabunge wajue wazi watanzania sasa tunadadisi hili na hatuko tayari kuona mashindano ya jazba badala ya mashindano ya uwajibikaji, hoja, kanuni na sheria.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom