Spika:"Hansard Ni Kwa Faida Ya Vizazi Vijavyo Sio kwa Faida Ya Siasa Za Leo" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika:"Hansard Ni Kwa Faida Ya Vizazi Vijavyo Sio kwa Faida Ya Siasa Za Leo"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DSN, Aug 3, 2011.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Bunge letu linaendeshwa kwa kodi ya Watanzania wa leo huku likiacha rekodi [HANSARD] yake ya leo ili ije kuwa faida ya kutumika kwa kizazi kijacho [Coming New Generation]. Tendo la tamko la Mwenyekiti [Spika] aliyekuwa anaendesha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jioni ya leo tarehe 3/08/2011,kazuia waandishi wa Bunge wasiandike kwenye Hansard ya Bunge maneno ya yaliyotamkwa na Mbunge wa CCM toka jimbo la Ludewa bwana FURUKUNJOMBE.

  Maneno hayao yaliyotamkwa na Mbunge huyo ni kama kuwa bila Wizara ya Uchukuzi kutenga pesa kwa ajili ya kivuko cha wilayani kwao kuepusha vifo vya mara kwa mara vya Wananchi vipatavyo watu ishrini kwa mwaka,wakiwa ni wahanga wa vifo vya maji kwa kuzama wakivuka maji na vifaa vyao kama mitumbwi yao.Hivyo basi Mbunge huyo atashawishi Wananchi wake waandamane hili kama hoja ya bajeti hiyo itapita pasipo kusikilizwa ombi lao.Pia akatoa Mchango wake kuwa ikibidi Serikali iwanyonge Wabunge wote wasiotimiza ama kukidhi mahitaji ya kutatua matatizo ya Wananchi.

  Hakika yalikuwa maneno mwiba sana kwa CCM kwa kuwa ndio chama tawala ukizangatia yamesemwa na Mbunge wa chama hicho hicho pia.Lakini yalikuwa ni maneno muhimu sana kuingia kurekodiwa kwenye Hansard ya Bunge letu kuweka kumbukumbu sahihi ya alichokizungumza mbunge huyu.

  Sikuona TUSI ama shambulio lolote la AIBU dhidi ya matamshi ya MBUNGE huyu machachari wa CCM. Ni kwa faida ya TAIFA kuweka kumbukumbu kwa VIZAZI VIJAVYO [COMING GENERATION].Kumbe kupitia Hansard vizazi viijavyo vitapima uwezo wa WABUNGE WETU katika kufikilia kupitia hizo hizo HANSARD HIZI ZINAZOANDIKWA LEO,uenda wakajifunza uwezo wa kufikili wa Wabunge wa Sasa baada ya miaka Hamsini [50] hata Mia [100] ijayo.

  Watapima uwezo wa kutoa hoja kwa Wabunge wetu uenda mawazo ya Mbunge wa Ludewa Bwana FURUKUNJOMBE aliyoyatamka leo na kisha Mwenyekiti akakata yasiandikwe kwenye Hansard yanaweaza yakawa ni kivutio na kutumika kwa usahihi kwenye kizazi hicho kijacho kama sio leo na wao kumuona kuwa alikuwa kiona mbali [Man of Vision] katika kuhukumu Watendaji wa Umma na uenda wakampa Nishani ya kutukuka kama zama hizi amefikilia hivi basi angeishi kizazi chao angekuwa wanaelewana Lugha Moja.


  Hakika Bunge letu litakuwa alijawatendea haki wana Ludewa kwa kuto andika maneno ya Mbunge wao kwenye Hansard.Kiti lini MTAACHA ITIKADI YA UCCM ILI MTENDE MAMBO KWA NIA NA FAIDA YA TAIFA NA VIZAZI VIAJVYO.HAKIKA NITAOMBA MATAMKO YA MBUNGE HUYO YAANDIKWE NDANI YA HANSARD VINGINEVYO TUAMBIWE KAMA KUNA SHERIA YOYOTE YA NCHI AU KANUNI ZA BUNGE KAVUNJA.NA KAMA ALIVUNJA YAANDIKWE ILI KAMA NI KOSA ILI WATAKAO KUJA KUJIFUNZA WAONE MBUNGE HUYO FURUKUNJOMBE ALIHUKUMIWA KWA KUTAMKA MANENO HAYA,AMBAYO KWA KANUNI HUSIKA ZA BUNGE LILIKUWA NI KOSA NA HAKAHUKUMIWA, NA SIO USHABIKI WA KUKIMBIA UKWELI KWA KUWA MBUNGE HUYO WA CCM ATAKUWA ANASHABIKIA MFUMO WA CHAMA CHA CHADEMA WA KUDAI HAKI KWA MAANDAMANO KAMA CHADEMA WANAVYOPENDELEA KUUTUMIA.

  Mtakataa wasisome kwenye Hansard za Bunge kisha wakakuta taarifa hizo huku baada ya miaka hiyo hamsini au mia ijayo watawazalau wale wote walioshriki kuzuia yasiandikwe kwenye kwenye Hansard.Ndipo hapo watawazodoa vizazi vyenu kuwa wamerithi woga na nidhamu ya ovyo isiyo na tija wala nia ya kujenga bali kufukia na kufunika yasiyo na sababu.

  Kwani lipi baya kusema likawa limesikika au kuandika na kuacha kumbukumbu ili Mbunge huyo kama Watanzania WAMEMUHUKUMU KWA UBAYA AU UZURI [POSITIVE OR NEGETIVE] BASI NI HAKI KUWAANDIKIA HANSARD VIZIZA VIJAVYO NAO WAMUHUKUMU KIVYAO KAMA NI HASI AU CHANYA KWA MUJIBU WAO WENYEWE.

  HELLOOOOW CCM KIKWETE NAMPA POLE JAMANI JAMANI JAMANI KUNA SEHEMU UWA NIKIFIKA NAJIULIZA NAKUKILI KWELI KIKWETE KWA AINA HII YA VIONGOZI WASIOJUA NI KWA NINI WAMEKUA VIONGOZI NA WAMEFIKAJE KUWA VIONGOZI NI HATARI SANA.POLE MR PRESIDENT!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mwenyekiti wa mjadala wa jana alipwaya sana na nimekuwa nikijiuliza hii tabia ya Spika na Naibu wake kuwa hawapo muda mwingi wa mijadala ya Bunge. Kikao hiki kimeshuhudia mingi ya mijadala ikiendeshwa na wenyeviti tofauti tofauti na hivyo kukosa seriousness na hata consistency katika tafsiri ya kanuni na maamuzi yake.
   
 3. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,674
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Hiyo ni kawaida sana.Ila udikteta wa kutoruhusu maneno fulani yasiwekwe kwenye hansard ni utovu wa nidhamu!..kwa kuendelea zaidi,ingekuwa vizuri tuwe na voting records za wabunge,haya mambo ya kupayuka ndiyoo!!au sawa!! na kugonga meza ni mambo ya kienyeji mno na yamepitwa na wakati.
   
 4. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hakika tena huyu aliyeendesha kikao hiki cha matamshi ya Mbunge FURUKUNJOMBE ilikuwa balaa,manake unajiuliza Kiti cha Spika wa Bunge ni kwa niaba ya Serikali au ni kwa niaba ya Wananchi wa Tanzania.
   
 5. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,067
  Trophy Points: 280
  Hili kwa kweli ni la muhimu sana....juzi tu tunawasikia kwenye chama wanakataa bei ya mafuta taa wakati ni wale wale waliopeleka mswada bungeni ambao pamoja na mambo mengine uliongeza kodi kwenye mafuta ya taa (tena kinyume na mapendekezo ya kikosi kazi cha kuboresha kodi) na ni hao hao waliopitisha mswada huo kwa kuupayuka tu ndiyooo. Si ajabu mwenyekiti wao ameshasaini muswada huo kuwa sheria!
   
 6. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2017
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Hii kitu "Hansard" ndio nini jamani!
  Ni nini sababu ya ku "Hansard"

  Tunaweza kuzitumia hansard kufanyia nini!?

  Nina maanisha hansard za bunge

  Nijuzeni wakuu.
   
 7. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2017
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Ina maana hakuna ajuae?
   
 8. Saplaiz

  Saplaiz JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2017
  Joined: Mar 26, 2014
  Messages: 244
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 60
  Ungeulizia kuhusu papuchi, thread ingekuwa iko page ya 44
   
 9. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2017
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Ukweli 100%
   
 10. corasco

  corasco JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2017
  Joined: Jan 17, 2016
  Messages: 1,764
  Likes Received: 1,272
  Trophy Points: 280
  Navyojua Mimi Hansard ni kumbukumbu za bunge ya mambo yote yaliyojadiliwa mfano sheria yoyote,na kazi yake utumika maktaba kwa kumbukumbu au marejeo pia hutumika kama source of information ya kilichojadiliwa bungeni.
   
 11. corasco

  corasco JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2017
  Joined: Jan 17, 2016
  Messages: 1,764
  Likes Received: 1,272
  Trophy Points: 280
  Hutumika katika tafit mbalimbali pia.
   
 12. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2017
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Huwa ni kumbukumbu rejea, nimekupata mkuu
   
 13. Zawadi B Lupelo

  Zawadi B Lupelo JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2017
  Joined: Jul 19, 2015
  Messages: 1,865
  Likes Received: 2,262
  Trophy Points: 280
  Hansard za bunge hurekodi kila kinachojadiliwa bungeni, maoni na mchango wa kila mbunge huingizwa kwenye Hansard.

  Hutumika sehemu nyingi na kwa shughuli nyingi hasa unaweza kurejea kujua mbunge fulani mwaka 1995 alisema nini.

  Moja ya matumizi ya Hansard za bunge hutumiwa na majaji kwenye kutafsiri sheria under mischief rule and purposive approach, hapa ni pale mahakama inapotaka kuitafsiri sheria ili kugundua lengo la bunge kutunga sheria fulani ilikuwa ni nini ( intention of the legislature) majaji huwa wanaamua kurudi kwenye Hansard za bunge kwa mfano jaji anataka kupata maana ya vifungu Fulani vya sheria ya mtandao Cybercrime Act anaweza kutafuta Hansard za 2015 siku waliyokuwa wanajadili upitishwaji wa hiyo sheria akaangalia wabunge walisema nini hii inasaidia kujua tafsiri na lengo halisi la bunge kutunga sheria husika. Japo kuwa hii haifanywi mara kwa mara na mahakama Bali ni pale mahakama ikiamua ku resort to a mischief rule or purposive approach tofauti na aina zingine za kutafsiri sheria
   
 14. tueur de lion

  tueur de lion JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2017
  Joined: Apr 21, 2017
  Messages: 838
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 180
  Napita tu
   
 15. corasco

  corasco JF-Expert Member

  #15
  Jun 2, 2017
  Joined: Jan 17, 2016
  Messages: 1,764
  Likes Received: 1,272
  Trophy Points: 280
  Umeongea kishwria mkuu sijui kama watakupata hapa.simplify
   
 16. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #16
  Jun 2, 2017
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Nakushukuru kwa kututoa tongotongo.
   
Loading...