Spika Dkt. Tulia awatahadharisha Wenyeviti wa Kamati za kudumu za Bunge kutoshawishiwa na asasi za kiraia

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,803
4,471
Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson amewataka wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge kuwa makini kuepuka kuingizwa kwenye mitego ya kudanganywa na asasi za kiraia zinapotaka ushawishi wa chombo hicho kupitisha ajenda fulani kwa utashi na maslahi yao.

“Bunge huwa ni chombo ha ushawishi, kwahiyo linapokuwapo jambo kwenye jamii asasi zitakuja ili kushawishi, watakuja kwenye kamati kwahiyo wenyeviti wanatakiwa kuwa makini na mambo hayo yanapotokea ili kujiridhisha kukwepa kutoingia kwenye mitego ya kudanganywa.

Dk Tulia ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Februari 21, 2021 wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya kamati ya uongozi, makamu wenyeviti wa kamati na wajumbe wa Tume utumishi wa bunge katika ofisi ndogo ya Bunge Tunguu, Zanzibar.

Mwananchi
 
Vipi Serikali ? Yenyewe Ruksa Kushawishi (Sorry Kushinikiza) na kutumia Bunge kama Rubber Stamp ?

Sioni tatizo la kushawishi (kwa hoja lakini sio mlungula)
 
Lobbying ni mchakato usioepukika kwa chombo chochote chenye kufanya maamuzi mazito yanayobeba maslahi ya wengi.

Sister Tulia bado ana mengi ya kujifunza kwenye hii nafasi.

Binafsi namtakia shule njema.
 
Bado sijamuelewa spika kuhusu hili.
Yeye alitaka taasisi za kiraia zifanye nini ikiwa zina agenda zao zenye kutakiwa kupitishwa na bunge?

Kama ni taasisi halali na zinafanya shughuli halali, wasiwasi wa nini?
 
Bado sijamuelewa spika kuhusu hili.
Yeye alitaka taasisi za kiraia zifanye nini ikiwa zina agenda zao zenye kutakiwa kupitishwa na bunge?

Kama ni taasisi halali na zinafanya shughuli halali, wasiwasi wa nini?
Pamoja na zile
  1. zinazotaka watoto wasichapwe?!
  2. zinazotaka mahari itolewe?!
  3. zinazokataa kukeketa lakini zinaunga mkono kujichubua na kuongeza ukubwa wa viungo!?
  4. zinazounga ndoa ya jinsia moja?!
  5. zinazotaka wanaume wawe sawa na wanawake!?
 
Back
Top Bottom