Spika Anne Makinda na Waziri Ummy Mwalimu Waombeni Radhi Wahadhiri

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
Katika hali ya kushangaza viongozi wa ngazi za juu wametoa kauli zinazokidhalilisha Chuo kikuu Cha Dodoma (UDOM) kuwa chuo hicho kimejaa rushwa ya ngono na udhalilishaji kwa watoto wa kike. Viongozi hao ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mh. Anne Makinda na Naibu waziri wa Jamii, Jinsia na Watoto - Ummy Mwalimu.

Naibu Ummy Mwalimu alimuuza mbunge Murtaza Mangungu (CCM) aliyekuwa angombea ujumbe wa Baraza la chuo kikuu cha Dodoma kuwa UDOM imejaa rushwa ya ngono yeye (mgombea) atafanya nini ili kuondoa kero hiyo. Ndipo Mh.Musa Haji Kombo (CUF) akaomba swali hilo lifutwe kwani linakidhalilisha chuo. Mh. Spika akadai "hakifutwi kitu hapa, hali ndivyo ilivyo".

Ndugu wanajamvi:
1. Kama hali ya udhalilishaji ni mbaya kiasi hicho, viongozi hao walishawahi kuchukua hatua yoyote ili kuondoa au kupunguza unyanyasi huo?
2. Kama kuna mtumishi mmoja au wawili ambao walishawahi kuwa na tabia hiyo kwanini ionekane kuwa tatizo hilo ni kubwa kiasi hicho?
3. Je tatizo la lushwa ya ngono likoje katika vyuo vingine vya umma hapa Tanzania?
4. Tunaomba kusikia kutoka kwa wasemaji wa chuo kuhusu hayo yanayodaiwa na viongozi wetu.
 
Kama kilichoongelewa ni kweli then why hao lecturers waombwe radhi?
 
Lugha za kubembelezana ndizozilizo tufikisha tulipo,Mtu kakamatwa akiiba asiitwe mwizi eti ni Mtuhumiwa mpaka atakapo hukumiwa na mahakama,Wahusika wa UDOM mpaka sasa hawajatoa tamko lolote wewe huruma hiyo unaitoa wapi ndugu!?
 
Hilo suala lipo vyuo vingi na taasisi mbalimbali tu nchi hii, pale UDSM nimesoma hali ni mbaya zaidi..hata humo ccm ndio usiseme!
 
sasa nani wa kulaumiwa hapo wakati wanaoendeleza haya wako huko huko?mimi naona kwanza bunge ndio linazidisha hii ishu kukaa bungeni muda mrefu na wabunge wengi hawaendi na wake zao au vimada vyao
 
Nyie mnawaonea tu wahadhiri...wasichana wanajirahisisha sana...tena wengine wanawataka kwa nguvu...hiki kitu kitaendelea kuwepo.
 
PROF kikula thibitisha au kanusha juu ya habari hii au ndo hauna ripoti kamili? ila sidhani kama atakuja maana hiyo kitu hapo ipo. tena baina ya walimu na wanafunzi hususan kipindi cha mitihani na matokeo, wapo wengi sanaa.
 
​Juma Nkamia naye anasoma hapo anaweza kuthibisha ama kukanusha mbona mkanda wa udini wa Selasini alikanusha?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom