Elections 2010 Spika Anna Makinda na Naibu wake wakalia Kuti Kavu Bunge la 10?

Mtu wa Mungu

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
444
195
Katika historia ya nchi yetu, bunge la 10 litakuwa bunge la umuhimu wa kipekee!!! kutokana na miongoni mwa sababu ni hizi hapa chini:-
1) Ni bunge la kwanza kuwa na serikali mbili, moja ndani ya bunge,serikali kivuli (CDM) na serikali tawala (CCM) upande wa pili!!!!!!!!!Uzoefu wa kipindi cha ufunguzi wa bunge hili umeonyesha dalili za mtafaruku mkubwa wa mijadadala-very hot discussions!!!!!!!!!!!!!!!.
Kwa siku za kwaza mijadala ya bunge hili itatawaliwa kwa sehemu kubwa sana na agenda za:-
(a) Sharti la CDM kutaka iundwe tume huru kuchunguza uhalali wa matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi-hoja ambayo inabeba maslahi makubwa ya taifa hili; kuna mambo ya msingi, kama vile kupata majibu ya maswali yanayoulizwa na wananchi wengi kutaka kujua kwa nini ni wapigakura milioni 8 tu ndiyo waliopiga kura kati ya milioni karibu 20 waliojiandikisha, ukizingatia kwamba uhamasishaji uliofanyika ni wa kihistoria!!!!!
(b) Dai la kuandika katiba mpya ambayo itaambatana na kupatikana tume mpya huru ya uchaguzi-nyenzo ambazo kwa sisiemu ni mwiba!!!!!!!!!!!!!!! lakini hoja za msingi kwa uhai na afya ya taifa letu; tukumbuke kwamba ni nchi yetu tu katika Afrika Mashariki iliyobaki na katiba chakavu na tume ya uchaguzi isiyoendana matakwa ya jamii!!!!
(c) Bado kuna viporo vya EPA,Richmond, Kagoda, Buzwagi, Bulyankulu nk ambavyo vitavuta hot discussions na hisia za wengi sana ndani na nje ya nchi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
(d) Spika Anna Makinda na Naibu wake siyo wanasheria kwa weledi wakati mijadala mingi itatawaliwa lugha za kisheria na hata maamuzi ya spika kutakiwa kuwa ya kisheria katika maeneo mengine ya papo kwa papo !!!!!!!!!!kama kutajitokeza Udhaifu wa spika na Naibu wake kutokuwa wepesi kutoa maamuzi ya kudumisha fairness; kama hili litatokea kuwa obstacle ya fair management ya vikao vya bunge, mimi naona hata uwezekano wa kufikia hatua za serikali kivuli (CDM) kuleta hoja za kutokuwa na imani na spika na naibu wake kwa madai ya kukandamiza upinzani, na uwezekano wa kuingiza bunge kwenye pande mbili zinazovutana!!!!!!!!!! na kupoteza mwelekeo wa constructive discussions; mfano mmoja mdogo kwenye kikao cha ufunguzi ni lile la Sophia Simba kwa bunge la SADC, CDM walibaini kuwa kanuni ya bunge ya uchaguzi imevunjwa lakini naibu spika akaamua kutumia nguvu ya kiti cha spika kuhalalisha uwakalishi batili-mambo kama haya ya spika kutumia nguvu badala ya sheria na haki ni moja ya sababu zinazonifanya kumwona Spika Anna Makinda kukalia kuti kavu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
:angry:
 

kaburunye

JF-Expert Member
May 12, 2010
674
0
We hujui siasa za nchi hii nini. Wakati wa discussions za wabunge spika ana mamlaka kubwa sana anaweza kufanya mambo kibabe tu kwa kutokujua sheria ili kuwaumiza wapinzani wa kweli (CHADEMA). Na kwa kuwa vyama vingine vyote vinaonekana kuwa na ndoa isiyo rasmi na CCM ni vigumu kupinga maamuzi ya kibabe ya spika
 

MSAUZI

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
229
195
Utasikia we Mbowe kaa chini nitakunyima posho ya pili..... "Samahani speaker"...hiiii ni Afrika mwanangu.watu pamoja na pesa zao wahusudisha posho kama nini
 

Newvision

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
446
0
Any way Mbowe hana shida ya pesa anazo nyingi lakini bado nina wasi wasi na Makinda kama ataruhusu fair play hapo mjengoni. Unajua Anna ni mama aliyekuwa frustrated halafu amewekwa kwa malengo maalumu ya kuzima hoja za wapinzani bungeni. I am not sure this calculation by CCM will work to their favour ila CDM kazi ngumu sana.
 

Mtu wa Mungu

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
444
195
Taarifa ya Spika Anna Makinda na Naibu wake Ndugai kwamba ni miongoni mwa wabunge wa sisiemu walio batili kwa mujibu wa katiba ya sasa ni moja ya matukio yanayoondoa stability ya kuti kwa Anna na Ndugai!!!!!!!!!!!! Kadiri pressure ya kesi hizi itakavyokuwa ina-build up, watapanda blood pressure, na loss of umakini unohitajika kuongoza vikao vya bunge!!!!!!!!!Sasa ukiongeza pressure ya hofu ya Tundu Lissu na team yake hali ya kuti itazidi kuwa tete zaidi!!!!!!!!!
 

KERENG'ENDE

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
398
195
Kama Anna ana akili ajenge urafiki na samweli....vinginevyo viatu alivyo vaa havimtoshi kabisaaa......nakama niboya basi limetoboka
 

Mtende

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
6,387
2,000
tatizo anna ni kibaraka wa lowasa na rostam so this time itakula kwake
 

niweze

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
1,008
0
Hongera CCM kwa Kumweka Makinda. Background ya Sheria Mzumbe Itafanya Kazi This Time. Tutaona Atakapo Jibu Vipengele vya Sheria na Taratibu za Bunge Lao Zaidi ya Kusema "Weye Kaa Chini Huna Adabu Kwangu" CCM Jiandaeni Kwa Tactics za Kisheria. Mtakimbia Hii Miaka Mitano na Mtajuta Kwanini Mliiba Kura Tena. CCM Mliona Sitta Hafai na Tutaona Makinda Anovyofaa kwa Inchi. Wale CCM Wanaolala Wataendelea Kulala Kama Kawaida Yao na Kula Kodi ya Wananchi...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom