Spika anapodhani waliosema ndio wameshinda!

Sabung'ori

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
2,166
1,247
...wabunge sasa nawahoji...wanaokubali waseme ndio...wasiokubali waseme sio...NADHANI waliosema ndio wameshinda.Huu ndio utaratibu unaotumika ktk bunge letu kupitisha au kutopisha mambo muhim ya nchi.Ndugu zangu wana-jamii nimelileta kwenu jambo hili mnisaidie kwani nimekuwa nikitatizwa sana na huo utaratibu wa bunge.Labda niweke wazi kile kinacho nitatiza,1.nashidwa kuelewa speka anatumia kipimo gani cha sauti kutambua kuwa walioshinda au shindwa ni wangapi?.2. Kuwatangaza washindi na walioshindwa bila ya kuwa na uhakika yaani kwa KUDHANIA tu.Baada ya kuutafakali kwa kina utaratibu huu nmegundua yakuwa baadhi ya matatizo yanayoikabili nchi hii yametokana na huo utaratibu wa viongozi wetu wa KUDHANI badala ya kufanya tafiti na kupata majibu yasokuwa na shaka.Leo taifa limekwama kwenyetope la ufukala kwa sababu viongozi wanakaa maofisi kutwa wakidhania tu,spika anadhani waliosema ndio wameshinda,waziri mkuu anadhan tatizo la wauza mafuta alimuhusu,raisi anadhani mgao wa umeme ni ukame,daktari anadhani mgonjwa anaumwa kichwa anampasua mguu nk.Mwisho ngependa kuwahasa wabunge wabadiri huo utaratibu kwani haufai na unalea uzembe,kudhani ktk mambo ya msingi ni sawa na kuyachezea kamali maisha ya watanzania...UMDHANIAE NDIYE KUMBE SIYE!

Kwa hakika hili ni kosa. Spika wa Bunge hawezi kuruhusu Mswada wa sheria au hoja yoyote ya serikali ipite i.e budget kwa 'KUDHANI'. Lazima kuwepo na uhakika. Beyond reasonable doubt kwamba upande fulani ndio umesema hivi na ule umesema vile. Na hii sio kwa kusikiliza sauti. Huu ni mfumo wa ki-ujima. Sijui kwa nini viongozi wetu wa bunge hawako innovative?

Kwa nini kusiwepo na utaratibu wa wabunge kupiga kura ijulikani wazi nani alisema ndiyo na nani alisema hapana. Tena hii ingekuwa kitu muhimu sana maana mpiga kura atajuwa mwakilishi wake yuko upande gani kwa kila hoja inayopita bungeni. Marekani ukitaka kujua 'voting record' ya senator wako unaweza kupata. Hapa sio rahisi kwa sababu hata kama alisema ndiyo, anaweza kutoka nje na kudai hakusema chochote au alisema hapana.

Kuwepo na 'electronic device' chenye NDIYO & HAPANA na inapofika wakati wa ku-voti, basi mbunge abonyeze NDIYO au HAPANA. Hii mambo ya kusema 'nadhani' upande fulani umeshinda ni wrong wrong wrong.

Ingefaa wakati mjadaka unakaribia mwisho,
Wapewe vikaratasi vya vote iwe kura ya siri.
Wengi hua wanaogopa kuonekana na wenzao ndo maana wanasema ndio ya mdomoni, huku moyoni wakijua ni sio

ni Tanzania pekee ndio tuna spika/naibu spika wa aina yake mwenye kpaji cha kuhesabu sauti. hakika anahitajika kuingia ktk kitabu cha guines na awe kivutio cha watalii pia. "SPIKA ANAYEWEZA KUHESABU SAUTI" Tutapata pesa nyingi za kigeni, au mnasemaje

Uwingi wa waliosema ndiooooooooooooooooo na sioooooooooooooo uko sawa. Ila nikashngaa spika kasema waliosema ndio wameshinda hapo hapo nikagundua wanaamua kufosi mambo yapite hata kama hamna hoja za msingi.

Haki ya nani sina imani kabisa na hili bunge,huyo spika ndio kabisaa hayuko siriaz na kazi yake..kutoa comments zisizo maana,kutoa kauli asonauhakika nazo inshort nahoji sana uwezo wake wa kazi kama spika..nilishuhudia pale pa NDIO na SIO,haihitaji jinias kutambua uozo wa hyo system ya kupitisha maswala muhimu ya kitaifa. Hata nilivokua chekechea tulikua tunapiga kura kupitisha monita na monitres,ni lini nchi yetu itakua siriaz jamanii!?INAUMA SANA

hizo ndo sera za CCM. mwenye akili na atazame kwa makini na kutambua kwa mtazamo chanya!

Ndio maana ya kuitajika katiba mpya kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015. Kura katika bunge inahitajika iwe ya siri kwa mbunge.
Kwa mfumo wa kutumbukiza karatasi katika box ambalo litawekwa mbele ya bunge. Na sio mfumo uliopitwa na wakati ukiwa
bado unaendelea ambao ni wa kuwakutishana kwa wabunge wa chama tawala.

ni Tanzania pekee ndio tuna spika/naibu spika wa aina yake mwenye kpaji cha kuhesabu sauti. hakika anahitajika kuingia ktk kitabu cha guines na awe kivutio cha watalii pia. "SPIKA ANAYEWEZA KUHESABU SAUTI" Tutapata pesa nyingi za kigeni, au mnasemaje
Sidhani kama Spika ndo mwenye matatizo. naona matatizo yapo kwenye kanuni zinazotumika, zinahitaji kurekebishwa ili ktuoruhusu upuuzi kama huo unaompa Spika mamlaka ya kupitisha kitu kwa kudhani

kanuni zeeeeeeeeeee!!kiboko chao katibaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa mpya chenye mwanzo mwisho huo hapo suluali zitawabana na vitambi walivyonavyo!!!!!sipati picha.

Huu utaratibu kwa kweli ni wa kitoto kabisa utafikiri mchezo wa kuigiza..

ni Tanzania pekee ndio tuna spika/naibu spika wa aina yake mwenye kpaji cha kuhesabu sauti. hakika anahitajika kuingia ktk kitabu cha guines na awe kivutio cha watalii pia. "SPIKA ANAYEWEZA KUHESABU SAUTI" Tutapata pesa nyingi za kigeni, au mnasemaje

Ndiyoooo!!

Haki ya nani sina imani kabisa na hili bunge,huyo spika ndio kabisaa hayuko siriaz na kazi yake..kutoa comments zisizo maana,kutoa kauli asonauhakika nazo inshort nahoji sana uwezo wake wa kazi kama spika..nilishuhudia pale pa NDIO na SIO,haihitaji jinias kutambua uozo wa hyo system ya kupitisha maswala muhimu ya kitaifa. Hata nilivokua chekechea tulikua tunapiga kura kupitisha monita na monitres,ni lini nchi yetu itakua siriaz jamanii!?INAUMA SANA

Userious utakuwepo pindi tutakapowaondoa CCM madarakani

Sidhani kama Spika ndo mwenye matatizo. naona matatizo yapo kwenye kanuni zinazotumika, zinahitaji kurekebishwa ili ktuoruhusu upuuzi kama huo unaompa Spika mamlaka ya kupitisha kitu kwa kudhani

Anayo matatizo makubwa tu ndio maana bunge linamshinda kwakuelemea upande mmoja

Kijana ndo tunatakiwa kufanya mabadiliko ya nchi yetu kwahiyo tuchukue hatua

Ingefaa wakati mjadaka unakaribia mwisho,
Wapewe vikaratasi vya vote iwe kura ya siri.
Wengi hua wanaogopa kuonekana na wenzao ndo maana wanasema ndio ya mdomoni, huku moyoni wakijua ni sio

Comment ya #2 hapo juu: ELECTRONIC DEVICE. Hilo ndilo suluhisho. Mbona vipaza sauti wanavyo kila mmoja? Si ni vidude vile vile vinavyofanyakazi kwa kanuni zile zile za ki-digital-electronics?

ni Tanzania pekee ndio tuna spika/naibu spika wa aina yake mwenye kpaji cha kuhesabu sauti. hakika anahitajika kuingia ktk kitabu cha guines na awe kivutio cha watalii pia. "SPIKA ANAYEWEZA KUHESABU SAUTI" Tutapata pesa nyingi za kigeni, au mnasemaje

<br / Haswaaaaa!!!

Back
Top Bottom