Spika amzuia Waziri Mkuu kuongea bungeni kuhusu mauaji ya raia Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika amzuia Waziri Mkuu kuongea bungeni kuhusu mauaji ya raia Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fasta fasta, Jun 17, 2011.

 1. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Lissu aibua bungeni mauaji ya Nyamongo

  NA WAANDISHI WETU

  [​IMG]
  Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, (Chadema)

  Spika wa Bunge Anne Makinda, ametaka Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, (Chadema), apeleke kwa maandishi malalamiko yake ya kutoridhishwa na kukataliwa kujibiwa kwa swali lake alilouliza kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kuhusiana na mauaji ya wananchi katika mgodi wa North Mara uliopo Nyamongo, wilayani Tarime mkoani Mara.

  Hatua hiyo ilifuatia Lissu kuomba mwongozo kutoka kwa Spika Makinda baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika bungeni jana baada Spika kumkatalia yeye na Mbunge wa Viti Maalum kupitia chama hicho, Esther Matiku kujibiwa maswali yaliyohusiana na mauaji ya raia yanayodaiwa kufanywa na polisi kwenye mgodi huo.

  Spika alikataa kujibiwa kwa maswali hayo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwa maelezo kesi ipo mahakamani.

  "Mheshimiwa Spika hadi sasa hakuna kesi hata moja inayowahusu waliohusika na mauaji haya na hakuna hata polisi mmoja aliyeshtakiwa," alisema.

  Spika alisema kuwa wamepokea malalamiko kutoka katika muhimili huo wa dola (Mahakama) kuwa wamekuwa wanaingilia uhuru wa mahakama na hivyo kukataa swali hilo.

  Akiomba mwongozo, Lissu alisema ingawa Spika alikataa swali lake lakini, hakuna kesi ya mauaji inayohusisha mgodi huo labda kama Spika Makinda anafahamu uwepo wa kesi.
  Alisema yeye na Matiku wanashitakiwa, lakini kesi yao haihusiani na mauaji.

  Akijibu muongozo huo, Spika alimtaka kuandika kwa njia ya maandishi kwa Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah, iwapo watahisi uamuzi wa Spika haukuwatendea haki, na suala hilo litajadiliwa na kuamuliwa na Kamati ya uongozi wa Bunge.

  Lissu katika swali lake alimtaka Waziri Mkuu afafanue juu ya taarifa ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ya mwaka jana iliyotolewa Mei mwaka huu na kuungwa mkono na taarifa ya Mambo ya Nje ya Marekani kuwa polisi nchini wanashiriki katika kuua raia 52.

  Pia alisema kwa upande wa Tarime polisi wameua wanakijiji 26 wa mgodi wa North Mara.

  Kabla Spika hajajibu mwongozo huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, alitoa utaratibu kwa kutumia kifungu cha kanuni za Bunge na kueleza kuwa anaamini kuwa Lissu na Matiko maswali yao yaligusa kesi zinazowakabili kwa kuwa yote yanahusu mambo yanayoendelea katika mgodi wa North Mara Tarime.

  "Mheshimiwa Spika ni kweli Lissu ameshtakiwa na ni kweli kesi inahusu mgodi wa Nyamongo na Tarime na kanuni inasema, mbunge hatazungumzia jambo lolote linalohusiana na mahakama, ushauri wangu mheshimiwa asubiri mahakama imalize kesi hii, iwe ya mgodi au polisi maswali haya yanaingilia uhuru wa mahakama," alisema.


  Awali Lissu, katika kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alimwuliza kuwa serikali imehalalisha mauaji ya raia yanayofanywa na Jeshi la Polisi kwani matokio hayo yamekuwa ya kawaida.

  Akijibu mwongozo na utaratibu wa wabunge hao, Spika alisema "Waheshimiwa wabunge tusijifanye sisi tunajua kila kitu na kuhukumu, Matiko na Lissu wako nje kwa dhamana sasa wao ndio waulizaji wa maswali haya ni haki kweli hiyo? Ndio maana ninasema jambo hili tuliache huko huko lisuluhishwe tuwaachie mahakama.

  Spika Anne Makinda alikataa swali hilo lisijibiwe na Pinda kwa kuwa suala la mauaji bado liko mahakamani na Bunge lisingependa kuingilia mihimili mingine ya dola.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kuna ugumu hapo.
   
 3. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Kama hali ndio hii ni nani msemaji wa haya mauwaji yanayojitokeza kila kukicha mara albino mara polisi.
  Kama nimemwelewa Mh Lissu anataka kujua je serikali nayo imejiandaa vipi ua ni hatua gani zitumike mara haya mambo yanapo jitokeza. Lakini mh makinda amefunga kombe ili mwanaharamu apite.
   
 4. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Noana Makindaa anayocheza makida hata kwenye vitu serious.. mauaji? CCm wanatumia lugha rahisi rahisi tu? hii itawa-cost hata hapo baadaedamu za watu haziendi bure.. Its true polisi sasa wanauwa watu onyo onyo tu, badala Pinda achukue hatua kaanza kuwa mtazamaji..ni lin Pinda alimuita huyo AGP na Nahodha wangalau akawakanya? the way forward hapa ni Chadema watetezi wa wanyonge nendeni mahakama za kimataifa kuwashitaki kina pinda na wenzake.
   
 5. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Katika mashitaka waliyofunguliwa wakina Lissu hakuna hata moja liliotaja "mauaji ya raia yaliyofanywa na Polisi" au "Polisi wameua raia". Mengi yali-base kwenye vurugu za kuwazuia polisi wasiibe maiti, wakatunga uongo.

  Hapa thamani ya Samweli Sitta ndipo inapooneka, ktk kuchambua na kutafsiri lugha za kisheria. Pia yule mzee ni msomaji wa magazeti. Huyu bibi koroboi nafikiri anachungulia vichwa vya habari. Hoja za Lissu zinazidi "kumvua nguo" huyo bibi koroboi. Naona huruma.
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  Prime Minister Mizengo Pinda  National Assembly Speaker Anne Makinda yesterday forbade the Prime Minister from answering two questions from Chadema legislators, saying they interfered with judicial independence.

  The questions were asked by Singida-East legislator Tundu Lissu and Special Seats MP Esther Matiko.

  The two MPs had asked the questions relating to the killing of people in Nyamongo who the police say had illegally invaded North Mara Gold Mine.

  In his question Lissu asked the PM that according to the Human Rights Report issued by Legal and Human Rights Centre police have been involved in extra-judicial killings of 52 people, and in Tarime the police had been involved in the killing of 26 Nyamongo villagers around North Mara Gold Mine.

  Lissu had asked whether it was government policy to allow the police to shoot to kill people.

  For her part, Matiku had reminded the prime minister about a promise he gave in the last parliamentary session in April that he would direct the Home Affairs minister to take action regarding the killing of 10 civilians and humiliation and torture done to people in Nyamongo.

  However, the Speaker intervened in both cases, saying that they had been receiving complaints about parliamentary interference in the independence of other state organs.

  "This matter is in court. I can not allow the Prime Minister to respond because there have been complaints that we are interfering in the independence of other organs," Makinda insisted.

  However, Lissu was not satisfied and asked for the Speaker's guidance, reminding her that there was not a single case in court relating to the killing of the 52 people; hence demanded an answer from the Prime Minister.

  However, Minister of State Prime Minister's Office (Policy, Coordination and Parliament Affairs) William Lukuvi said that both MPs were referring to a case related to North Mara Gold Mine, thus asked them to leave the matter to the courts because discussing it meant interfering with judicial independence.

  "We should not pretend that we are the court and decide on everything. These two MPs are out on bail, thus, to be on the safe side, let's leave this matter to the courts," Speaker Makinda insisted.

  Simanjiro legislator Christopher Ole–Sendeka told Lissu that parliamentary standing orders directed that if an MP was not satisfied with a decision reached by the Speaker he could write to the Clerk of the National Assembly for further action.


  By Lydia Shekighenda, The Guardian
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  What judicial independence? Is Nyamongo killings a judicial issue? What nonsense. Huyu mama mlimtoa wapi?
   
Loading...