Spika amtwisha mzigo Brigedia Jenerali Ngwilizi; Kamati Wabunge Watano Kuchunguza Ufisadi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
IJUMAA, AGOSTI 03, 2012 05:17 NA MAREGESI PAUL, DODOMA

*Aunda kamati ya wabunge watano kuchunguza ufisadi
*Waziri Muhongo, Tundu Lissu kutoa ushahidi wao

BUNGE limeunda kamati ndogo kwa ajili ya kuchunguza kashfa ya rushwa kwa baadhi ya wabunge.

Kamati hiyo, ilitangazwa bungeni jana na Spika wa Bunge, Anne Makinda, muda mfupi baada ya kuhitimisha kipindi cha maswali na majibu.

Kwa mujibu wa Spika Makinda, kamati hiyo yenye wajumbe watano, itaongozwa na Mbunge wa Mlalo, Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi na itafanya kazi kwa kipindi cha wiki mbili, kisha kuwasilisha ripoti yake kwa Spika.

Pamoja na hayo, Spika alisema tume itatakiwa kuwahoji wabunge wanaoweza kusaidia kupatikana kwa taarifa sahihi, wakiwamo Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

"Waheshimiwa wabunge, wiki iliyopita Mheshimiwa Vita Kawawa (Mbunge wa Namtumbo CCM), alitoa hoja kwa mujibu wa Kanuni ya 53 (2) 55 (3) na 5 (1), kwamba michango mingi iliyotolewa na wabunge wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, iliwatuhumu baadhi ya wabunge kujihusisha na vitendo vya rushwa, wakiwemo wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini.

"Baada ya hoja hiyo, nilitoa mwongozo kwamba kwa mujibu wa Kanuni ya 53 nitazipeleka tuhuma hizo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, ili zifanyiwe uchunguzi ipasavyo.

"Katika utekelezaji wa suala hilo, Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imeandaa hadidu za rejea zitakazotoa mwongozo wakati wa kufuatilia jambo hilo.

"Hadidu hizo za rejea ni kwamba, kamati hiyo itatakiwa kuchunguza na kumshauri Spika, iwapo tuhuma kwa baadhi ya wabunge na wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini ni za kweli au siyo za kweli," alisema Spika Makinda.

Aliwataja wajumbe wa kamati hiyo, kuwa ni Mbunge wa Manyoni Magharibi, John Chiligati (CCM), Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Amour Arfi (CHADEMA), Mbunge wa Karagwe, Gosbert Blandes (CCM) na Mbunge wa Viti Maalum, Riziki Omar Juma (CUF).

"Baada ya mashauriano kati ya Spika na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na kwa kuzingatia ‘nature' ya suala lenyewe, tumeona suala hili linaweza kujadiliwa vizuri kwa mujibu wa Kanuni ya 114 (18) kwa kuunda kamati ndogo ya wajumbe watano, itakayoongozwa na Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

"Kamati hii ndogo, italifanyia kazi suala hilo kwa muda wa wiki mbili na baada ya kazi yake itawasilisha taarifa kwa Spika kama Bunge lilivyopanga na ili kazi ifanyike vizuri, kamati itatakiwa kufanya kazi kama ifuatavyo:

"Kwanza kamati lazima izingatie misingi ya haki asili na pia itatakiwa kuzingatia hansard ya tarehe 27 na tarehe 28 Julai, ambapo bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini iliwasilishwa.

"Pamoja na mambo mengine, lengo la kutumia hansard ya siku za mijadala ni kupata picha halisi ya namna mjadala mzima ulivyoendeshwa kwa siku hizo mbili.

"Pia kamati itatakiwa kuwaita na kuwahoji mashahidi watakaoisaidia kujua ukweli na wanaotakiwa kuhojiwa ni pamoja na Tundu Lissu, ambaye katika mkutano wake na waandishi wa habari, aliwataja wabunge ambao alidai wana maslahi binafsi na TANESCO.

"Mwingine anayetakiwa kuhojiwa ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ambaye katika majumuisho ya hotuba yake, alitaja tuhuma za baadhi ya wabunge.

"Naamini wale wote, waliosema wana ushahidi na walimtaka Spika ataje majina ya wanaotuhumiwa, waende wakataje majina kwenye hiyo kamati na nawaomba waheshimiwa wabunge, yeyote atakayeitwa aende akatoe ushahidi," alisema Spika na kuhitimisha.

NCCR-Mageuzi walalamika

Wabunge wa Chama cha NCCR-Mageuzi, walionyesha kutoridhishwa na muundo wa kamati hiyo kwa kuwa wao hawakujumuishwa.

Hofu hiyo ilielezwa na Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali, wakati alipoomba mwongozo wa Spika akitaka kujua ni kwa nini chama chao hakina mjumbe kwenye kamati hiyo ndogo licha ya kuwa na uwakilishi bungeni.

"Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kamati hii iliyotangazwa na Mheshimiwa Spika, wabunge wa CCM ni watatu, lakini NCCR hatukushirikishwa. Kwa maana hiyo, Mheshimiwa Mwenyekiti naomba mwongozo wako kwa mujibu wa Kanuni ya 68 (7)."

Akijibu mwongozo huo, Mwenyekiti wa Bunge, ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama (CCM), alisema hawezi kulizungumzia zaidi jambo hilo, kwa kuwa Spika ameshalitolea ufafanuzi.

Wiki iliyopita, wakati Bunge likijadili bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013, ziliibuliwa taarifa kuwa, baadhi ya wabunge walikuwa wamekula rushwa kwa ajili ya kuihujumu wizara hiyo.

Wakati huo huo, Kamati ya Wabunge wa NCCR-Mageuzi, imemwandikia barua Spika wa Bunge, kupinga uteuzi wa Mbunge wa Karagwe, Gosbert Blandes (CCM) kuwa katika kamati ndogo ya kuchunguza rushwa kwa wabunge.

Katika barua hiyo, ambayo imeandikwa na Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali, NCCR-Mageuzi wanasema Blandes hastahili kuwa mjumbe wa kamati hiyo, kwa kuwa ni kati ya wabunge waliokuwa wakiwashawishi wenzao waipinge bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.

 

Naona Kamati iliyoundwa ni CLEAN... Jamani Msituangushe Wananchi...

Najua wa CHADEMA harudi tena BUNGENI na ni fair; Wa CUF hana MCHEZO i like him...
 
Hiyo kamati siyo mbaya sana ila huyo Gosbert ka'a ni kweli ni mtuhumiwa hafai katika kamati hiyo.
 
Back
Top Bottom