Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,510
- 4,224
Wakati waziri wa fedha akisoma bajeti ambayo ndiyo msingi na hatma ya watanzania 2022/2023 Spika wa JMT Mh Dr.Tulia Ackson amemzuia waziri wa fedha Mh Mwigulu Nchemba kuimba nyimbo za sifa na kurudia rudia kauli za pongezi kwa Rais.
Je, huu ni mwanzo wa mwisho wa tabia za kuingiza siasa na pongezi zisizokuwa na tija hususan kwenye mambo nyeti na muhimu kwa taifa kama bajeti kuu ya serikali?
Tabia hii ya kutoa pongezi na kusifia hovyo hovyo hata pale pasipokuwa na ukweli au ulazima wa kufanya hivyo imekuwa jambo la kawaida kwa viongozi wengi hususan mawaziri.Hali hii imepelekea hata katika mambo ya msingi na nyeti viongozi kushindwa kuongea ukweli na kuingiza siasa kwa lengo la kujinufaisha wao binafsi mbele ya Rais.
Hali hii huwafanya viongozi wa juu hususan Rais kushindwa kuupata ukweli na endapo hatachukua hatua za ziada katika kuutambua na kutafuta ukweli na uhalisia basi hali hubaki midomoni na siasa za hapa na pale huku wananchi wa chini wakiumia.
Je, Nini kifanyike kukomesha tabia hii?