Spika amkatalia Zitto kuweka muda zaidi wa maoni ya mswada wa Tume ya Maoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika amkatalia Zitto kuweka muda zaidi wa maoni ya mswada wa Tume ya Maoni

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by POMPO, Apr 5, 2011.

 1. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Wakuu! Asubuh bungeni wakati wakijadili mswada wa namna ya kutunga sheria ya kusimamia rasmu ya katiba, Zitto aliomba muongozo wa spika, na kusema kuwa, ni vema wabunge wakapata muda wa kwenda kujadili na wapiga kula wao ili wananchi washirikishwe toka mwanzo.
  { Zitto alitoa wazo zuri}
  ANAUMBULIWA:
  Spika Makinda, alisema wazi wazi kuwa zitto alikuwa ni miungoni mwa wajumbe, aliomba mswada huo upelekwe bungeni kwa hati ya dharura.
  My take:
  kwa nini Zitto hakuliona swala la wapiga kura ndani ya kamati kabla ya bungeni wakati anapendekeza hati ya dharura...
  Akiwa kwenye kamati zake mtu mwingine akiwa bungeni kiini macho!?
   
 2. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  ndio sasa mumfahamu vizuri ni mtu wa aina gani, sio kumshabikia tu kama wengi wafanyavyo kwa babu wa samunge!
   
 3. m

  matunge JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  amelewa sifa mapema
   
 4. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  zito anapenda kufanya mambo kwa kujionyesha ili apewe sifa.
   
 5. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Zitto anaendelea kutoa utata.Ni bora alivyoumbuliwa.anataka kutuzuga sisi?Muumbue kama ana ndimi mbili.
   
 6. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,901
  Trophy Points: 280
  Wekeni habari vizuri tuielewe.
   
 7. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Zitto is a double dealer; anayosema hadharani ni tofauti na yale ayasemayo/ayatendayo nyuma ya pazia!! Hei is after publicity.
   
 8. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,229
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  Akiwa kwenye vikao vya mafichoni, wapiga kura huwa sio subject. akitokeza kwenye public anajifanya wapiga kura ndio subject. stupid boy. tuliyaona hayo wakati wenzie waliposusia hotuba ya JK hatukumuelewa ila sasa tunamsoma vyema. he is opportunist. cheap polika politician.
   
 9. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sasa ni wazi kwamba huyu babu wa loliondo anatishia mapato yako au ya mumeo huko kanisani kwenu. Watu wanakwenda tu kupata kikombe na kurudi kwenye madhehebu yao. Haingilii miradi ya makanisa!!
   
 10. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,057
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Mwacheni wadau tuzidi kupata ugoro wake mwingi siku ikfika tupate kumwambia kila tukio kwa mwaka,mwezi,wiki,siku na mda na kila mahali alipokuwa wakati wa usaliti.. a.k.a mR.MISIFA
   
 11. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #11
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  Mtoa hoja ,Makinda anasema Zito aliomba mswaada upelekwe bungeni kwa hati ya dharura. Umefika bungeni siyo?

  Sasa ulitaka wazo la sasa la Zito angelitoa wakati gani? kamati ya zito ni mambo ya fedha, au yumo kwenye kamati ya katiba? imeundwa lini hiyo kamati??

  Guys, huwa naogopa sana kujibu baadhi ya hoja kwa kuonekana great thinker sana na kuonekana pro-chadema au pro-zito. Ila huwa ninakuwa na wasiwasi sana kuyafuatilia baadhi ya mambo ya Zito, maana yamekaa kiujanja ujanja ambao kwangu mimi huwa nahesabu magoli ya kisiasa kwa sababu hii ni SIASA.

  Ugumu ulikuwa mjadala kwnda bungeni,umefika, la pili ni kukusanya maoni ya wananchi ambapo kila mtu anataka, tatizo la zito liko wapi??

  Ok, ebu tujadili kibinadamu zaidi

  Suppose zito alijisahau hii hoja yake, na leo hii ameisema, is it too late??? kama alichosema leo unakiri ni kizuri, then NANI, LINI na wapi katika hao wengine waliothubutu hata kusema uende kwa wananchi hata kabla haujafika bungeni? wangetumia methodology gani??

  Katika wabunge 320 mnataka aonekane zito tu?? wengine wanafanya nini? au walifanya nini?

  Mwisho je maoni ya Zito bungeni huwa ni Zito au huwa ni chama chake??

  Ni wakati gani maoni ya zito yanaonekana personal na maoni ya zito yanaonekana ya kichama zaidi??


  Do I sound like great thinker...yes! yes! LMAO!
   
 12. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  HUELEWEKI kasikilize tena uelewe.... Futa upupu wako huu Tafadhari... Umeanza kumrithi Mzee Makamba wa Mipasho Modern Taarab
   
 13. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  KATIKA HILI ZITTO KABWE YUKO SAHIHI KABISA NA KWAMBA BAADA YA OFISI YA SPIKA KUWAGAWIA WABUNGE NAKALA YA MUSWADA WA MOI SASA KILA MBUNGE ARUDI JIMBONI TUKASHAURIANE KWANZA TENA BILA KUKOSA!!!!

  Katika hili mchangon wa Mheshimiwa Zitto IKO SAHIHI KABISA.

  Kiukweli nawaasa Wapiganaji, tusiwe wanafiki kwamba kama hatukubaliani na Zitto juu ya mambo kaadha, sawa na mimi nisivyokubaliana naye juu ya mambo mengi, basi hata pale anapotetea msingi unaokubaliana na matakwa yetu kama Umma wa Tanzania (na wala si kutetea msingi wa mafisadi) basi sisi ni kukimbilia tu KUMWAGA MAJI NJE PAMOJA NA MTOTO NDANI YA BESENI.

  Kimsingi kabisa, ni kwamba mara baada ya ofisi ya bunge kuwagawia kila mbunge nakala ya mswada wa CCM basi sasa ni muda muafaka kwa KILA MBUNGE KURUDI JIMBONI KWAKE KWENDA KUSHAURIANA NA MABOSI WA (Sisi Wapiga Kura) juu ya aina ya muswada uliowashilishwa bungeni, maana na mantiki yake, kwa kiasi gani inavyowakilisha maoni yetu.

  Tena ni kwamba hadi hapo sasa SISI KAMA WAPIGA KURA TUNAMPA MHESHIMIWA MBUNGE WETU UJUMBE GANI WA KWENDA KUCHANGIA KULE bungeni pindi mjadala utakapoanza; yaani ni kwamba tutakuwa tunamwelekeza mbunge wetu juu ya kitu gani akiunge mkono, kipi kirekebishwe vipi na mambo yapi akayakatae moja kwa moja.

  Hakika alichokisema Mhe Zitto endapo haitozingatiwa na Wabunge kudiriki kushiriki mjadala wa HUU MUSWADA BATILI WA CCM bila kwanza kuomba maelekezo ya wapiga kura basi mjue ya kwamba WABUNGE WENGI SANA WATAKAOPINGANA NA UMMA basi ni dhahiri kwamba kibarua chao kitaota mbawa.

  Huu mswada, kwa watu makini na wadadisi wa mambo watagundua kwa AG Werema kaudesa kutoka kwa MUSWADA WA MOI WA KENYA enzi hizo alipojitia kicha ngumu kukubali wananchi wake kujiundia katiba mpya. Leo hii Moi hayupo madarakani huko lakini wananchi wapo wamejaa tele na KATIBA MPYA kabisa kutokana na wananchi moja kwa moja sasa hivi inafanya kazi.

  Jamani huu mswada wa Moi ambayo hivi sasa Kikwete Kaudesa nukta kwa nukta isipokua kafanya tu kazi ya kuingiza 'Unite Republic of Tanzania' kila mahali kwenye ile nafasi iliyoandikwa Republi of Kenya, hata kule kwa Kibaki alikoidesea Kikwete nako pia iliwahi kukataliwa na kutupiliwa mbali na kamati ya bunge inayoshughulikia mambo ya sheria na katiba na AG kulazimishwa kushauriana kwanza na wadau wote na kuingiza mapendekezo yao moja kwa moja ndani ya muswada ndio mambo yaendelee kwenye sakafu la bunge.

  Na hiyo ndio siri kwa nini huo mswada muhimu sana kwa kila raia haukuandikwa kwa lugha yetu ya Kiswahili. Maswali zaidi muulizeni Msekwa aliyeenda huko majuzi kuchukua zaidi ya MOI'S UNPOPULAR FILE ON CONSTITUTION ili waje kuvijaribishia kwetu kama tutakubali.

  Tumsikilize Zitto katika hili na hatua ya kufuatia ya maandamano nchi nzima kupinga huu mswada dhalimu ni kwamba maelekezo tutapeana kwa wakati na mtindo stahiki endapo kweli serikali haitoingiza maoni ya Wadau wa katiba kwenye huo muswada.

  Aluta Continua!! Vijana kote nchini tukae tayari mkao wa kulikomboa taifa letu, ONCE AND FOR ALL, kutoka mikononi mwa MAFISADI endapo maslahi yao ndio itakayoonekana wa muhimu zaidi hapa!!!!!!!!!!!!

  Naona safari ya kamba kukatikia pabovu, baada ya kuibiwa sana kura zetu, kudhalilishwa sana kimaisha na MAFISADI, baada ya kulaghaiwa sana na na vingozi wa CCM, ndio huu!!!!!!
   
Loading...