Gurudumu
JF-Expert Member
- Feb 5, 2008
- 2,349
- 261
Alisoma waraka ulioonekana wazi kwamba ulikuwa umeandaliwa kabla.
Katika waraka huo alidai kwamba kuna vyama vya siasa vinavyotumia fursa ya Mswada wa kutunga Katiba mpya kujijenga kisiasa. Alidai pia kwamba vyama hivyo vinachochea vijana kuleta vurugu katika zoezi la kukusanya maoni.
Alikemea vyama hivyo na kuahirisha Bunge ili kuwapa wabunge fursa ya kushiriki katika zoezi la kutoa maoni.
Kimantiki, hii ilikuwa na tafsiri ya kuwapa wabunge nafasi kwenda kudhibiti hilo wimbi la wananchi waliochochewa kuleta vurugu kwenye mikutano ya kukusanya maoni. Nalazimika kufikiri hivyo kwa sababu Spika hakutoa hoja iliyothibitisha kwamba Wabunge walikuwa hawana muda wa kutoa maoni yao kwenye Public hearing na kwamba hiyo ndiyo siku pekee iliyobakia wao kutoa maoni.
Zaidi, sina uhakika kama Spika alikusudia kutuambia kwamba polisi walishindwa kudhibiti hizo vurugu na kwamba anawafungulia Wabunge wake ili wakaifanye hiyo kazi kikamilifu.
Lakini, nini kazi ya kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba? Je, Public hearing ni ya wabunge au wananchi? Je, si Mswada huu utafikishwa Bungeni ili Wabunge wajadili na kutoa maoni yao kisha waupitishe au kuukataa? Na kwa mantiki, Wabunge wanatoa maoni kwa nani?
Je, ni wabunge wangapi na wa chama gani waliojiorodhesha katika mikutano ya kutoa maoni siku hiyo ya Ijumaa katika mikoa ya Dar, Dodoma na Zanzibar? Idadi hiyo waliojiorodhesha/waliohudhuria inapelekea kuahirisha Bunge zima?
Je, nini ilikuwa ratiba ya kikao cha Bunge cha siku hiyo na ni namna gani yaliyokuwa yajadiliwe siku hiyo yanapata kujadiliwa? Kwa nini ni rahisi kiasi hicho Spika (bila kuuliza maoni ya wabunge wote) kuamua aahirishe bunge bila kujali maslahi na matarajio ya Wabunge na Wananchi katika hoja ambazo zilikuwa zijadiliwe siku hiyo?
Je, ni sahihi kufikiri kwamba Makinda aliamrishwa (na mamlaka fulani ambayo siifahamu) kuahirisha Bunge ili kutoa muda wa wabunge wa ccm ambao walikuwa kwenye mchakato wa vikao vya juu vya chama kujiandaa/kushiriki?
Kama fikra hizo zikiwa sahihi (natamani zisiwe sahihi), Je, ni pesa kiasi gani zilitumika kuweka wabunge Dodoma siku hiyo aliyoahirisha Bunge? Ni nani anabeba hizo gharama, ccm au serikali (wananchi)?
I am just thinking aloud, Naomba tujadili na wenye taarifa sahihi watupatie please