Katika kile kinachoonekana kujipangia mkakati wa kuendelea kuwa kinara wa CCM mkoa wa Tabora Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki ambaye pia ni Spika bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samuel Sita amemsogeza karibu ya ofisi yake (BUNGENI)Kijana mmoja kutoka Tabora(Bw kwikima) kufanya kazi sehemu ya utawala. kibaya zaidi wakati vijana wa kitanzania wakilia usiku na mchana juu ya tatizo la ajira Mh spika amemuachisha kijana kazi ofisi ya Madini mkoa wa Dodoma. habari kutoka chanzo cha uhakika wa habari hizi zinadai kuwa Mh Spika amemsogeza karibu yake kijana huyo na kumshawishi agombee Uenyekiti wa Vijana mkoani kwake ili aendelee kujiwekea matumaini ya kisiasa jimboni urambo kwani kama atafanikisha kijana huyo kuikwaa nafasi hiyo basi atakuwa na ngome katika Kamatiya siasa Mkoa wa Tabora. Swali bwana Spika ni lazima amueke mtu ofisi kwake mtu kutoka Tabora ambaye tayari kijana alishakuwa kibosile katika ofisi ya Madini Mkoa wa Dodoma au ndiyo mikakati ya kila mtu kuchukua chake mapema? kazi kwenu Tabora Bw Spika anawaletea Mkiti wa Kuchonga