Spika Ndugai adai tena kuwa Lissu alishalipwa pesa zake zote

Eti lisu hali yake iwe mbaya halafu amwambie yule mgogo aliyepewa bunge kwakukosa msimamo. Pathetic hiv ndugai ana nini hasa Cha kujivunia au kujilinganisha na lisu

Ukiondoa vile ving'ombe vyake vyenye kwashakoo anavyolingia navyo hamna kingine zaidi ya umasikini tu.

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Kabisa ! si tu aibu kwa familia yake but ni aibu kwa taifa
Ndugai ana kibri Cha uzima hajui madaraka ni ya mpito atendee wenzake haki na awe na utu. Huyu mzee kichefu chefu Sana, nchi ni yetu sote regardless ya ma vyama Yao.
 
Ila kwaleo ndu gai kamuonea Lissu kwa sababu Lissu alisema anaamini yaliyopo mitandaini hayana ukweli baada yakumuuliza mhusika wa wizard ya fedha. Yeye anaenda.bali zaidi nakumsema vibaya wkt yete hakutajwapopote. Dah, Spike unafeli sana. Bahati mbaya hata makofi bungeni yamepungua siku hz
 
You are very right.Nani alijua kuwa Magu atavuta very mysteriously but imewezekana kwa uwezo wa Mungu,Mungu kala kichwa cha Magu bila kumwaga damu.Nchi hii ilikuwa ni one man show daaaah,aisee nimeamini Mungu fundi
Ndugai ana kibri Cha uzima hajui madaraka ni ya mpito atendee wenzake haki na awe na utu. Huyu mzee kichefu chefu Sana, nchi ni yetu sote regardless ya ma vyama Yao.
 
You are very right.Nani alijua kuwa Magu atavuta very mysteriously but imewezekana kwa uwezo wa Mungu,Mungu kala kichwa cha Magu bila kumwaga damu.Nchi hii ilikuwa ni one man show daaaah,aisee nimeamini Mungu fundi
Mungu atusaidie tu hata kwa huyo ndugai mharibu bunge la nchi yake na hivi ana Kinga yakutokushtakiwa ndo shida haswa
 
Naona kama Ndugai amekata tamaa na maisha yake hivyo anafanya vurugu zote. Hama cha kupoteza. Kifupi kajizira.
 
Leo nimefurahishwa Sana na michango ya Wadau wa JF.
Kuna mengi nimejifunza. Inaonekana kwamba baada ya Speaker Ndugai kutoa ufafanuzi kukanusha taarifa ile, taswira kadhaa zimejitokeza;
Kuna watu wameumia kwa nini ametolea maelezo!! Ni Bora angekaa kimya!!
Zaidi ya 80% ya michango imetoka nje ya mada badala ya kujadili ukweli wa taarifa iliyokanushwa watu wamejikita kumuandama Spika.
Kumbe wanaleta taarifa za uongo makusudi halafu wanaumia zikikanushwa. Yaani badala ya kumbana aliyeleta taarifa za uongo tunamsakama anayekanusha uongo.
Angalau basi hata angeitwa au angeombwa Lisu aje atoe maelezo binafsi ili kukiridhisha na kauli ya Ndugai
Kwa muktadha huu hatuna uhalali wa kudai JF tunawakilisha maoni ya Watanzania walio wengi manake siamini kwamba Watanzania ktk ujumla wetu Ni wanafiki na wenyechuki Kama sisi humu JF...!!

Halafu tunajiita eti sisi ni great thinkers

Great Thinker my foot!!
Lol
Kulikuwa kuna haja gani ya kumshambulia Lissu?Kama ni kujibu angejibu tu kuwa hakuna anayedai na Lissu ameshalipwa!
Hiyo ya kuanza kumsakama Lissu kuwa kama ameishiwa huko Ulaya aseme,kwani Lissu ndiye kaeneza huo uzushi?
Isitoshe kabla ya kauli ya Ndugai,Lissu mwenyewe alikanusha uzushi huo wa mitandaoni na kusema si kweli!
Hapo ndipo watu wanamuona Ndugai ana chuki binafsi na Lissu!
Kama hujaliona hilo basi jitafakari uwezo wako wa ufahamu!
 
Ameanza kujishtukia kama taarifa si ya kweli anakanusha na kutoa maelezo ya nini?
 
Stahiki gani alizolipwa Lissu?

Huyu spika wakati akitangaza kumvua Lissu ubunge sababu iliyotolewa ni kwamba bunge halina taarifa za wapi alipo (mtoro).

1. Sasa leo tena anasema alilipwa, iweje bunge lilipe stahiki za mtoro?

2. Kama alilipwa stahiki maana yake bunge lilikuwa na taarifa za wapi alipo, kwa nini alivuliwa ubunge?

good
 
Huyu naye uongo ndio ameona ni ukweli na ukweli ni uongo
Katiba Mpya inakuya weh haya tu....
 
kitu inapigwa mtandaoni anacheza bungeni
Kajjihisi na sijui hofu ni ya nini aliyonayo?
 
SPIKA NDUGAI: HAKUNA ANAYELIDAI BUNGE, "KAMA MTU AMEISHIWA HUKO ULAYA SI ASEME"

Spika wa bunge Job Ndugai amewaonya wanaotoa taarifa za upotoshaji zenye lengo la kulichafua bunge kuacha kufanya hivyo kwa kuwa sasa hatua zitaanza kuchukuliwa ikiwemo kuitwa kwenye kamati ya maadili ya bunge

Spika Ndugai ameyasema hayo bungeni Dodoma leo Juni 25,2021 wakati akitolea ufafanuzi wa orodha inayozagaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha majina ya waliokuwa wabunge wa bunge la 11 likiwemo la Tundu Lissu kuwa wanalidai bunge hivyo walipwe

Spika amesema taarifa hiyo ni ya uongo kwa kuwa ilikuwa ya mwaka 2018 na kwamba hakuna mbunge wala aliyekuwa mbunge hata mmoja anayelidai bunge

"Na hata huyo mtu wao alilipwa kila kitu, ila zilipoingia benki walizichukua zote, na kama mtu kaishiwa huko ulaya alipo si aseme tu, bunge ni taasisi iliyopo makini na haimuonei mtu, hakuna hata mmoja anayeidai" amesema Spika Ndugai

==========

"Na hata huyo mtu wao alilipwa kila kitu, ila zilipoingia benki walizichukua zote, na kama mtu kaishiwa huko Ulaya alipo si aseme tu, Bunge ni taasisi iliyopo makini na haimuonei mtu, hakuna hata mmoja anayeidai"

Amesema Spika Ndugai

===========

Spika Ndugai akiwa Bungeni leo Ijumaa Juni 25, 2021 amekanusha Tangazo lilitoka na kuelezea madai ya wabunge wanaolidai Bunge.

Spika Ndugai: Jana kuna tangazo fulani lilitoka la majina mengi kwamba limetolewa na TRA, katika majina yale mengi ya wizara mbalimbali yapo na majina ya wabunge wa Bunge la 11 lililomaliza muda wake.

Kumbe lengo lao ni kumfatilia mtu mmoja tu wanayemtaka wao kuonyesha ana madai fulani bungeni lakini Orodha imetolewa ndefu na wakaanza kumshambulia Spika na kuchonganisha na kadhalika.

Tangazo hilo ni la uongo, ni tangazo lilikuwa la mwaka 2018 huko nyuma na malipo hayo yalisharekebishwa na niwaambie wabunge wa Bunge ambalo limemaliza muda wake maana wengine hali ni mbaya huko, sasa walipoona lile tangazo, simu ya spika imejaa bwana tuna madeni tunadai kwako.

Hakuna anaedai Bunge, hakuna. Katika chombo ambacho kinafanya kazi vizuri, kimojawapo ni bunge. Hakuna anaedai na kama mtu ameishiwa huko Ulaya au wapi si aseme tu kuliko kusingizia Bunge kila wakati kwamba kuna madai, hakuna anaedai, hayupo na hata huyo mtu wao alilipwa kila kitu.
Spika acha masiala,Lissu ni mtu mzima na ana akili timamu, kwamba akusingizie ili iweje ? Acha kabisa mchezo huo Mara moja Mungu anakuonya, ipo siku utafumba macho , tenda mema utalipwa mema aya ni Manisha yanapita ,please NDUGAI hacha,hacha,hacha,hacha
 
Back
Top Bottom