Spika Ndugai adai tena kuwa Lissu alishalipwa pesa zake zote

SPIKA NDUGAI: HAKUNA ANAYELIDAI BUNGE, "KAMA MTU AMEISHIWA HUKO ULAYA SI ASEME"

Spika wa bunge Job Ndugai amewaonya wanaotoa taarifa za upotoshaji zenye lengo la kulichafua bunge kuacha kufanya hivyo kwa kuwa sasa hatua zitaanza kuchukuliwa ikiwemo kuitwa kwenye kamati ya maadili ya bunge

Spika Ndugai ameyasema hayo bungeni Dodoma leo Juni 25,2021 wakati akitolea ufafanuzi wa orodha inayozagaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha majina ya waliokuwa wabunge wa bunge la 11 likiwemo la Tundu Lissu kuwa wanalidai bunge hivyo walipwe

Spika amesema taarifa hiyo ni ya uongo kwa kuwa ilikuwa ya mwaka 2018 na kwamba hakuna mbunge wala aliyekuwa mbunge hata mmoja anayelidai bunge

"Na hata huyo mtu wao alilipwa kila kitu, ila zilipoingia benki walizichukua zote, na kama mtu kaishiwa huko ulaya alipo si aseme tu, bunge ni taasisi iliyopo makini na haimuonei mtu, hakuna hata mmoja anayeidai" amesema Spika Ndugai

==========

"Na hata huyo mtu wao alilipwa kila kitu, ila zilipoingia benki walizichukua zote, na kama mtu kaishiwa huko Ulaya alipo si aseme tu, Bunge ni taasisi iliyopo makini na haimuonei mtu, hakuna hata mmoja anayeidai"

Amesema Spika Ndugai

===========

Spika Ndugai akiwa Bungeni leo Ijumaa Juni 25, 2021 amekanusha Tangazo lilitoka na kuelezea madai ya wabunge wanaolidai Bunge.

Spika Ndugai: Jana kuna tangazo fulani lilitoka la majina mengi kwamba limetolewa na TRA, katika majina yale mengi ya wizara mbalimbali yapo na majina ya wabunge wa Bunge la 11 lililomaliza muda wake.

Kumbe lengo lao ni kumfatilia mtu mmoja tu wanayemtaka wao kuonyesha ana madai fulani bungeni lakini Orodha imetolewa ndefu na wakaanza kumshambulia Spika na kuchonganisha na kadhalika.

Tangazo hilo ni la uongo, ni tangazo lilikuwa la mwaka 2018 huko nyuma na malipo hayo yalisharekebishwa na niwaambie wabunge wa Bunge ambalo limemaliza muda wake maana wengine hali ni mbaya huko, sasa walipoona lile tangazo, simu ya spika imejaa bwana tuna madeni tunadai kwako.

Hakuna anaedai Bunge, hakuna. Katika chombo ambacho kinafanya kazi vizuri, kimojawapo ni bunge. Hakuna anaedai na kama mtu ameishiwa huko Ulaya au wapi si aseme tu kuliko kusingizia Bunge kila wakati kwamba kuna madai, hakuna anaedai, hayupo na hata huyo mtu wao alilipwa kila kitu.

Ukweli uthibitishwe na mamlaka huru tofauti na bunge kujitetea kupitia kiongozi wake maana siyo jambo rahisi kwa bunge linalotuhumiwa kwa kutowalipa wadai wake kukubali na kukiri mbele ya umma
 
Ndugai ishi vizuri na watu sponsor yu udongoni, kuna maisha baada ya u-spika!
 
Aisee kumbe hakuna mtu anadai Bunge,

Looh hawa chadema mbona hawaishi kuwa waongo waongo.
 
Malkia wa mipasho.
1624644800278.png
 
Chadema pia acheni tukunga uzushi mitandaoni.

Kama mlijua ile document ilikua ya 2018, mka crop majina tu ila hamkuweka full pdf document ili kuwapumbaza wafuasi wenu nyumbu spika amewaumbua.
Sio kila mtu ni CDM ila ndugai ana chuki Sana, hata u speaker umemzidi hakitendei haki kiti Cha u speaker wallah.
 
Leo nimefurahishwa Sana na michango ya Wadau wa JF.
Kuna mengi nimejifunza. Inaonekana kwamba baada ya Speaker Ndugai kutoa ufafanuzi kukanusha taarifa ile, taswira kadhaa zimejitokeza;
Kuna watu wameumia kwa nini ametolea maelezo!! Ni Bora angekaa kimya!!
Zaidi ya 80% ya michango imetoka nje ya mada badala ya kujadili ukweli wa taarifa iliyokanushwa watu wamejikita kumuandama Spika.
Kumbe wanaleta taarifa za uongo makusudi halafu wanaumia zikikanushwa. Yaani badala ya kumbana aliyeleta taarifa za uongo tunamsakama anayekanusha uongo.
Angalau basi hata angeitwa au angeombwa Lisu aje atoe maelezo binafsi ili kukiridhisha na kauli ya Ndugai
Kwa muktadha huu hatuna uhalali wa kudai JF tunawakilisha maoni ya Watanzania walio wengi manake siamini kwamba Watanzania ktk ujumla wetu Ni wanafiki na wenyechuki Kama sisi humu JF...!!

Halafu tunajiita eti sisi ni great thinkers

Great Thinker my foot!!
Lol
 
Pigo takatifu kwa huyu mtu linakuja tu
Kama kuna taasisi inayohitajika ipigwe chini ni hili bunge la mayatima chini ya yatima mkuu Ndugai ambaye kama si uvumilivu na ukondoo wa Watanzania hakutakiwa kuendelea kukinajisi kiti cha uspika hata kwa dakika moja zaidi.
 
SPIKA NDUGAI: HAKUNA ANAYELIDAI BUNGE, "KAMA MTU AMEISHIWA HUKO ULAYA SI ASEME"

Spika wa bunge Job Ndugai amewaonya wanaotoa taarifa za upotoshaji zenye lengo la kulichafua bunge kuacha kufanya hivyo kwa kuwa sasa hatua zitaanza kuchukuliwa ikiwemo kuitwa kwenye kamati ya maadili ya bunge

Spika Ndugai ameyasema hayo bungeni Dodoma leo Juni 25,2021 wakati akitolea ufafanuzi wa orodha inayozagaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha majina ya waliokuwa wabunge wa bunge la 11 likiwemo la Tundu Lissu kuwa wanalidai bunge hivyo walipwe

Spika amesema taarifa hiyo ni ya uongo kwa kuwa ilikuwa ya mwaka 2018 na kwamba hakuna mbunge wala aliyekuwa mbunge hata mmoja anayelidai bunge

"Na hata huyo mtu wao alilipwa kila kitu, ila zilipoingia benki walizichukua zote, na kama mtu kaishiwa huko ulaya alipo si aseme tu, bunge ni taasisi iliyopo makini na haimuonei mtu, hakuna hata mmoja anayeidai" amesema Spika Ndugai

==========

"Na hata huyo mtu wao alilipwa kila kitu, ila zilipoingia benki walizichukua zote, na kama mtu kaishiwa huko Ulaya alipo si aseme tu, Bunge ni taasisi iliyopo makini na haimuonei mtu, hakuna hata mmoja anayeidai"

Amesema Spika Ndugai

===========

Spika Ndugai akiwa Bungeni leo Ijumaa Juni 25, 2021 amekanusha Tangazo lilitoka na kuelezea madai ya wabunge wanaolidai Bunge.

Spika Ndugai: Jana kuna tangazo fulani lilitoka la majina mengi kwamba limetolewa na TRA, katika majina yale mengi ya wizara mbalimbali yapo na majina ya wabunge wa Bunge la 11 lililomaliza muda wake.

Kumbe lengo lao ni kumfatilia mtu mmoja tu wanayemtaka wao kuonyesha ana madai fulani bungeni lakini Orodha imetolewa ndefu na wakaanza kumshambulia Spika na kuchonganisha na kadhalika.

Tangazo hilo ni la uongo, ni tangazo lilikuwa la mwaka 2018 huko nyuma na malipo hayo yalisharekebishwa na niwaambie wabunge wa Bunge ambalo limemaliza muda wake maana wengine hali ni mbaya huko, sasa walipoona lile tangazo, simu ya spika imejaa bwana tuna madeni tunadai kwako.

Hakuna anaedai Bunge, hakuna. Katika chombo ambacho kinafanya kazi vizuri, kimojawapo ni bunge. Hakuna anaedai na kama mtu ameishiwa huko Ulaya au wapi si aseme tu kuliko kusingizia Bunge kila wakati kwamba kuna madai, hakuna anaedai, hayupo na hata huyo mtu wao alilipwa kila kitu.
Aonyeshe makaratasi kwani ugumu uko wapi
 
Back
Top Bottom