na Mwandishi Wetu
OFISI ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imesema Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ana maadui wanaoathirika na maamuzi ya Bunge pamoja na wafanyakazi wachache wa ofisi hiyo wenye nongwa na ambao wameshindwa kwenda na dhana ya viwango na kasi katika utendaji wao.
Kutokana na hali hiyo, ofisi hiyo imesema inazo taarifa za njia mbalimbali zinazotumika na mahasimu wake (Spika) kumchafua kutokana na msimamo wake wa kuliimarisha Bunge liwe chombo madhubuti zaidi cha uwakilishi wa wananchi.
Ofisi hiyo ya Bunge imelazimika kueleza hayo kufafanua tuhuma mbalimbali zinazotolewa dhidi ya Spika kwa njia ya mtandao wa inteneti.
Taarifa iliyotolewa jana na Kaimu Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, inaeleza kuwa tuhuma hizo zinazotolewa zinaelekea kuwa ni wa makusudi na usiostahili na unaenezwa na makundi hasimu dhidi ya Spika.
Ni vema vyombo vya habari vijihadhari na taarifa za kuokoteza ambazo zinaeneshwa kwa misingi ya chuki.
Tujiulize kwa nini haya yanatokea mara baada ya maamuzi ya Bunge kuhusu Richmond? Ofisi ya Bunge inatambua muhimu wa wananchi kupewa taarifa sahihi kuhusu Bunge na uendeshaji wake kwa vile ni chombo chao cha uwakilishi, ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa Ofisi ya Bunge inasikitishwa na tuhuma zinazoelekezwa kwa Spika na kusema ikiwa kuna yeyote ambaye anazo tuhuma halisi dhidi ya Spika, anapaswa kuziwasilisha kwa uwazi, ili zifikishwe kwenye mamlaka husika zifanyiwe kazi kwa utaratibu ulio bayana.
Vinginevyo minongono dhidi ya viongozi ndio zitakuwa habari za nchi yetu. Hapo sio tu tunawadhalilisha viongozi walengwa bali zaidi tunaidhalilisha nchi, ilieleza taarifa hiyo.
Taarifa hiyo inakanusha Ofisi ya Bunge kumlipia Spika sh milioni mbili kwa kila wiki kwa ajili ya dawa au matibabu na kwamba hajawahi kuhojiwa kuhusu matumizi ya gari la umma.
Inaelezwa kuwa Spika ana magari ya walinzi na ya huduma za nyumbani licha ya gari rasmi na kwamba magari yote yanatumika kuzingatia bajeti iliyopangwa, kwa ajili ya Ofisi ya Spika.
Aidha, inaelezwa kuwa Bunge linasimamia vema matumzi kwake na yangekuwepo matumizi ya hovyo ya fedha, yangedhihirishwa katika taarifa za kila mwaka za wakaguzi.
Source: TanzaniaDaima