Spika aahirisha safari ya Marekani

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,573
Naona spika ameamua kuahirisha safari ya marekani na kurejea bungeni kesho huenda hii ni kutokana na hali halisi ya bunge na mjadala wa jana na wabunge kushinikiza waletewe ripoti ya richmond.

Hapa kunaanza kukucha kidogo kidogo.
 
MK.Eleeke.

Great news...Can you gives us the source please?

Tunashangaa hat made him come to the concl. Kanini hakuona umuhimu huo mapema..!!
 
Source ni taarifa rasmi za bunge zilizotangazwa na naibu spika muda mfupi uliopita na atakuwa bungeni kesho,
 
Bungeni pamewaka moto sana kutokana na wabunge wengi kuona hali halisi kuwa spika amemdhalilisha naibu wa spika.

Wabunge ni wakali kwelikweli na wanataka kuzungumzia azimio leo mchana japo haijajulikana ni azimio gani hilo ambalo wanalizungumzia ,nitawapa news pindi zikiwepo.
 
Source ni taarifa rasmi za bunge zilizotangazwa na naibu spika muda mfupi uliopita na atakuwa bungeni kesho,

ok Thanx ... Kumbe unaweza kuacha safari ya USA ukawahi bungeni kesho akati umeshaaga nchiozima ka mbwembwe kibao..tutajua nini kilimfika na kuamsha akili yake toka usongizini!!! I though he is very sick and can not stop the appntment ya Dr!!! Kumbe ..nisemeje ..ulikuw amchezo? Utoto?/...???
 
Bungeni pamewaka moto sana kutokana na wabunge wengi kuona hali halisi kuwa spika amemdhalilisha naibu wa spika.

Wabunge ni wakali kwelikweli na wanataka kuzungumzia azimio leo mchana japo haijajulikana ni azimio gani hilo ambalo wanalizungumzia ,nitawapa news pindi zikiwepo.

Nafikiri ni AZIMIO JIPYA!!! ...Im jocking!!!!!.

Moto unawaka kwelikweli. OK.. Hata likiwa azimio la arusha ..au la zanzibar..au..La Kuwashughulikia mafisadi..ETC The thing is Ifike mahali Heshima ya Tiafa tukufu Tz irudi!!Tena maramoja!!!

Ni forces za kijamii zinazoamua nini kitokeee!!

Miakili ya kifisadi inaweza ikaamua kufuta vifungu muhimu vya maazimio muhimu ya kitaifa kama Azimio La Arusha. Kilevi tu mtu anaamka asubuhi anaondoa miiko ya uongozi! KISA?? MAFISADI Kama Mkapa, Yona, Richmond, Buzwagi, at al.. Wanataka kufanya Biashara za kifisadi. Mkapa ameponzwa..na azimio la zanzibar..Sasa Hivi anaonekana haifananii tz kila anapopita.

Leo hii Mtu akisema turudishe kipengele muhimu cha azimio la A nani atabisha.Kila manachi anajioneea nini viongozi anafanya ikulu, richmond, migodini..etc.. Nguvu za kijamii zinaongea na zina mikondo yake isiyopindishwa kipuuzi tu!! Hapo Mwanzo Hatukumuelewa JKNyerere...But time SPEAKS...UTU..UKWELI NA UBINADAMU VILIVYO NDANI YA AZIMIO LA ARUSHJA HAVIPITWI NA WAKATI...just wait and uc'..Mkapa na machungu yote yanayompata..hawezi kupinga Azimio la Arusha..anaWish asingeliamini azimio la zanzibar..aka_Behave . Leo asingecheka hata na Mtoto...Anamshangaa. Nafikiri abunge wameweza kusoma taarifa za ENZI NA NYAKTI ZILIZOPO...HAWACHEKI NA MTU!!!
 
Haya sasa ni maigizo!!!!!!!!!!

Nyambala nakuungana nawe uamuzi huo nafikiri ni maamuzi ya juu, maana mzee Six alifanya Bunge tukufu ni mkoba wake ambao anawaachia watoto wake wasiufungue mpaka awepo. Hii inanikumbusha hadithi za zamani wakati tu watoto mfalme alipoenda safari ya mbali aliwaamuru wafuasi wake wasifunue sanduku, alipoondoka wafuasi wake wakakaidi ile amri ya mfalme, wakalifungua lile sanduku kumbe mfalme alificha njiwa mle wakaruka wote waliokuwa wamefichwa na mfalme, labda mfalme Six anaogopa Buzwagi, BOT na Richmondi vitaruka .....
 
Hao wabunge wa CCM hapo hakutakuwa na jipya wala hawawezi kumfanya lolote spika wao. Ni huyo mama Malecela tu ndio Ngangari kweli kweli lakini wengine ni waoga na wanataka vyeo.

Bunge lingelikuwa na nguvu basi wangepiga kura ya kutokuwa na imani na spika.
 
Naona spika ameamua kuahirisha safari ya marekani na kurejea bungeni kesho huenda hii ni kutokana na hali halisi ya bunge na mjadala wa jana na wabunge kushinikiza waletewe ripoti ya richmond.

Hapa kunaanza kukucha kidogo kidogo.

Shenzi kabisa huyu! Yeye alifikiri nani mpaka aahirishe kikao cha bunge kwa sababu ya safari yake uchwara ya kwenda US! Hawa watu wana kiburi cha hali ya juu.
 
Ushirombo ulipotelea wapi wewe? Hii kali ndugu yangu. Unajua umefika wakati immature politicians like Six kuondoka bungeni. Inakuaje unapoondoka na ofisi nayo inaondoka? nini maana ya kuwepo naibu spika? au ndiyo njama za kuwepo yeye hili awabane akina Zitto na Slaa? Huyu mzee anamatatizo ya akili. Naona baada ya kelele nyingi za raia na magazeti ameona amekosea. Sitta ovyoooooooooooooooooooooo
 
Ushirombo ulipotelea wapi wewe? Hii kali ndugu yangu

Mshikaji mambo ya mabox mazee ila nipo sasa !!! Naanza pata hisia kuna wabunge hata walio kwenye sisiem wanauchungu na nchi na wako tayari kuitetea, wakati mwingine nawaza labda hata hao tunaodhani wako jasili wakipewa ulaji watabadilika....Kuna Jamaa alikuwa anaitwa Njelu Kasaka alikuwa vocal sana na G55 baada ya kupewa mrija hahahahahah akawa bubu...nafikiri tuanze upya tu kutofautisha itakuwa ngumu, ama zile sheria za China zitumike, umefisadi basi shaba mbele ya halaiki hahahahahah haki za binadamu zifuate baadaye
 
Hao wabunge wa CCM hapo hakutakuwa na jipya wala hawawezi kumfanya lolote spika wao. Ni huyo mama Malecela tu ndio Ngangari kweli kweli lakini wengine ni waoga na wanataka vyeo.

Bunge lingelikuwa na nguvu basi wangepiga kura ya kutokuwa na imani na spika.

Nakuunga mkono kwa hoja hiyo
Ingekuwa wanataka kuondokana na usanii wa Sitta lazima wangemkomalia ajiuzulu kwa kuliburuza bunge!
 
Kumbe safari yenyewe haikuwa muhimu hiiivyooooooooooooooooo!!!!!

Yaani huyu mzee longolongo kweli na ana roho mbaya vilevile, si angemtuma Naibu Spika Mama Makinda au Mwenyekiti Job Ndugai na wao wakatanue majuu huko.
 
Tamaa baba!
Anataka ashike kila kitu mwenyewe, bunge mwenyewe, safari yeye mwenyewe, mikataba yeye mwenyewe nk, naona hizi "per diem" zitawaua hawa wazee wetu sasa. Labda aliona mama Makinda ama katibu wa bunge watafaidi sana hizo dola.
Wazee wengine noma sana.
 
Kumbe safari yenyewe haikuwa muhimu hiiivyooooooooooooooooo!!!!!

Yaani huyu mzee longolongo kweli na ana roho mbaya vilevile, si angemtuma Naibu Spika Mama Makinda au Mwenyekiti Job Ndugai na wao wakatanue majuu huko.Yaani Masatu leo ndiyo unajua haya ? CCM yetu ina mambo ya ajabu . Spika kaambiwa na Mwenyekiti wa Chama kwamba unakiua Chama sasa wakato yeye akiwa Pemba anajaribisha .Uamuzi huu ni kutoka juu na ndiyo sasa wameanza kuona uchungu wa wananchi .
 
Yaani Masatu leo ndiyo unajua haya ? CCM yetu ina mambo ya ajabu . Spika kaambiwa na Mwenyekiti wa Chama kwamba unakiua Chama sasa wakato yeye akiwa Pemba anajaribisha .Uamuzi huu ni kutoka juu na ndiyo sasa wameanza kuona uchungu wa wananchi .

Welcome back to CHAMA CHAMA MAPINDUZI (CCM)
 
Back
Top Bottom