Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge

Pascal take strength from this indictment! Hii kwako ni recognition kwamba Paschal Mayallah a.k.a NJALA you are notable member of the fourth estate, a confident "pen pusher" of merit; nenda Dodoma with confidence, kwako hii ni fursa adhimu kusema unachokiamini na kuweka msimamo mzito kwanini uliandika ulichokiandika kwa makusudi mazima wala sio bahati mbaya, wape waheshimiwa wabunge darasa, usiogope, ni kweli utaadhibiwa na kukemewa kwa namna moja au nyingine kwani watu hao wana madaraka na hasira kwa ulichokiandika lakini katika adhabu wanazoweza kukupa sio kifungo wala kukuua bali kujaribu kukupunguza confidence! Kwa hiyo simama imara, pay them back in kind kwa kuwaambia ukweli kwa kadiri unavyoamini na jinsi dhamira yako ilivyokutuma kuandika, maana kusema ukweli kutakuweka huru, na pia kusema ukweli sio hodhi ya mtu mmoja peke yake "NJI" hii! wambie ukweli, ukweli mtupu ili nafsi na dhamira yako viwe huru, Paschal nasisitiza usiogope kwani There is no gain without pain! I wish you a good encounter@parliament.org
 
Tatizo wewe Ulitaka awe Ukawa?
Paschal Mayalla ni Mwanahabari huru...
Hafungamani na Upande wowote na Huwa analiweka wazi hilo....Tatizo Inategemea na Uelewa wa Kichwa chako...spoon Feeding!
Yeye kila Upande Kukosoa na Kusifia pale inapostahili....Tatizo wewe Umezoea 1+1=2
Kwani 1+1 inajibu jingine tofauti na 2 ???
 
Pascal yuko sahihi katika hili ndiyo ukweli wenyewe bunge linajikomba komba. Huyu spika kwa nini alimpigia simu Rais Magufuli eti kumuuliza ni wabunge gani awateue kwenye kamati ya uchunguzi wa madini? Sasa kama si kujipendekeza nini? Wakati yeye ana uwezo wa kikatiba kuteua wabunge wowote. Na sisi tusingeyajua kama bila rais mwenyewe kusema. Siku hiyo ndiyo nilijua Spika huyu hafai ni bendera kufata upepo tu.
 
Ushahidi wa 1+1=4 huu hapa.
Screenshot_2018-01-22-10-17-06-1.jpg
 
Spika Job Ndugai ametoa maagizo kwa Kamati ya Maadili ya Bunge, kumhoji Mwanahabari Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema kwa kuandika makala ikiwa na kichwa "Bunge linajipendekeza?"

View attachment 742128

Makala hiyo inayodaiwa kulidhalilisha Bunge ilitoka kwenye toleo la Jumatatu tarehe 9 Aprili 2018.

Taarifa zaidi zinafuata...

INGEFAA ZAIDI SPIKA AMWITE P.MAYALA AKATOE SEMINA JUU YA WAJIBU, HAKI NA MAANA YA BUNGE. NASHANGAA SANA KWA MR NDUGAI AMBAYE AMEZEEKEA BUNGENI HAJUI KUWA RIPOTI YA KAMATI TEULE YA BUNGE INAWASILISHWA BUNGENI. HIYO NI AIBU YA KARNE. SPIKA WAOMBE RADHI WATANZANIA KWA KUKOSEA HUKO KWA MAKUSUDI KWA LENGO LA KUJIKOMBA KWA RAISI. ANGALIA JINSI ULIVYOLIFANYA BUNGE KUWA JUMUIYA YA CCM.
 
Wanabodi,
Leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa habari, kila mwaka sisi waandishi huwa tunakutana mahali kwa siku 2 na kujadili mambo mbalimbali kuhusu uhuru wa habari, na katika mkusanyiko huo, serikali, vyama vya habari na Taasisi za habari hutoa matamko kede kede kuhusu uhuru wa habari, lakini kwa mwaka huu, kufuatia janga la Corona, hakuna maadhimisho yoyote rasmi ya kukutana, ila nilitegemea wizara ya habari, vyama vya habari na mashirika na Taasisi za habari zitoe matamko mbalimbali.

Bado sijabahatika kuona tamko lolote!, ila usikute zile speech huwa zinaandaliwa kwa ajili ya presentations kwenye kongamano hotelini, safari na per diem!, leo hakuna safari, no trip, no per diem, no hotel gathering, hivyo this time hata speech tuu hakuna?!.

Nawatakia waandishi wenzangu, maadhimisho haya ya kimya kimya, nawashauri wale wafadhili mbalimbali wa tukio hili, kwa vile hatukusafiri, wala kula na kulala hotelini, then naomba hao wafadhili watutumie tuu hizo per diem, tutahama majumbani mwetu na kuhamia hotelini 3 days kisha tutatoa matamko.

Paskali
 
Spika Job Ndugai ametoa maagizo kwa Kamati ya Maadili ya Bunge, kumhoji Mwanahabari Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema kwa kuandika makala ikiwa na kichwa "Bunge linajipendekeza?"

View attachment 742128

Makala hiyo inayodaiwa kulidhalilisha Bunge ilitoka kwenye toleo la Jumatatu tarehe 9 Aprili 2018.

Taarifa zaidi zinafuata...
Asalaam Tanzania! bilashaka mmejibu kazi iendelee.

binafsi nimehuzunishwa sana na kauli ya SPIKA akiwa bungeni siku ya alhamisi tarehe 8/4/2021 yakuwa

"MKUBWA akishasema wengine inabidi tukae kimya"

Aliyasema hayo akirejea maoni yake kuhusu ujenzi wa bandari ya bagamoyo ambapo alisema rais alishauriwa vibaya.

Kiukweli kauli hii inaonesha udhaifu MKUBWA katika taasisi ambayo ilipaswa kuheshimika na kusikilizwa sana! Taasisi ambayo ni mhimili mkuu, taasisi ambayo inapaswa kuisimamia serikali, kutunga sheria na kutupa bajeti bora kwa maendeleo ya kweli kwa taifa letu.

Kistaarabu kauli ile (YA AIBU) ilipaswa kufutwa kwenye Hansard kwani inawafundisha wabunge ambayo wengine niwageni sio tuu kutoshauri kitu mkubwa (rais) akishakiongea! Bali kuwa waoga! bubu! na kutowasilisha matakwa ya wananchi waliowachagua!

Endapo kiongozi wako ananyamazishwa wewe uliye chini yake utasema nini?

Na huu ni uthibitisho mwingine yakuwa serikali ililiweka bunge mkononi na kuliamulia vyakusema, kwa bunge la namna hii tusitarajie maendeleo hili ni 'rubber stamp' ya nini serikali inataka.

Si ajabu sasa kuona wooote waliokosoa serikali waziwazi wametupwa pembeni kwenye uchaguzi wa aibu wa 2020. Sio ajabu kusema wabunge wa upinzani kupitia viti maalumu kuingia bungeni litakuwa ni agizo toka kwa MKUBWA kwenda kwa MDOGO.

Mhimili umegeuka sio mhimili tena,haustahimili kulibeba taifa na hauwezi. Udhaifu huu ni lazima tuuongee bila kukubali kuogopa vitisho na mateso yanayoweza kutekelezwa juu yetu! Tupaze sauti tulikatae.

BUNGE LA AIBU, AIBU, AIBU TUPU!
Hii iishie humu humu jf, ikitoka tuu nje, ikachapishwa na gezeti lolote, jiandae kuitwa Dodoma!.
Usije kusema hukujua, niulize mimi mwenzio, yalinikuta yepi?.
P
 
Hii iishie humu humu jf, ikitoka tuu nje, ikachapishwa na gezeti lolote, jiandae kuitwa Dodoma!.
Usije kusema hukujua, niulize mimi mwenzio, yalinikuta yepi?.
P

Mayalla P,
Upo rafiki yangu? Ulikuwa kimya sana tangu homeboyz wako atutupe mkono....once again pole sana.
Nilidhani baada ya homeboyz wako JPM kuihama duniya hii pengine mama angeli kukumbuka kwenye umalkia wake lakini wapi...!!!
Nilitegemea angalau nikuone pale Whitehouse ukichukua nafasi ya Msigwa lakini timu ya Vetting hawajakuona......!! Itabdi upeleke maombi maalumu kwa mama aise!!!
Pole.

Kuhsu Bunge niseme hivi: Supukali Ndugai ni mnafiki mkubwa, kigeugeu na mfitini Bunge la Tanzania limewahi kuwa naye!!
Hatumwelewi Ndugai kudai ati Hayati Jiwe alishauriwa vibaya kuhusu BANDARI YA BAGAMOYO!!!
Bunge ni chombo/muhimili unaotakiwa KUISIMAMIA na KUISHAURI SERIKALI. Je, wakti Rais akishauriwa vibaya Ndugai na KAMATI zake zote walikuwa wapi?
Huyu mgogo hajitambui hebu aache ujinga!!!
Watz tunajua MADUDU MENGI tu aliyofanya kwa USHAURI WA MAREHEMU MAGUFULI kwa uchache tu ni haya:
1. Kuwadhibiti Wabunge wa Upinzani.
2. Kuzuia Bunge Live.
3. Kumfurusha CAG Prof. Assad baada ya kuhoji ufisadi wa 1.5 Trillion na matumizi ya hovyo Spika akiwa India kwa matibabu.
4. Utungaji wa Sheria kandamizi kwa media na mitandao ya kijamii.

Ni Bora Ndugai akae kimya itamsaidia vinginevo anataka kuwachokora Watz kwene Awamu hii ya Mama!!
 
Spika Job Ndugai ametoa maagizo kwa Kamati ya Maadili ya Bunge, kumhoji Mwanahabari Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema kwa kuandika makala ikiwa na kichwa "Bunge linajipendekeza?"

View attachment 742128

Makala hiyo inayodaiwa kulidhalilisha Bunge ilitoka kwenye toleo la Jumatatu tarehe 9 Aprili 2018.

Taarifa zaidi zinafuata...
1624273650218.png

nilitaka nijue tu kipindi cha miaka mitano iliyopita hakuna matukio yaliyotokea na haukuandika chochote
Mkuu NIJUE , kumbe licha ya kuitwa nijue, kumbe hujui na unataka kujua!. Na mimi naomba kujua hiyo miaka 5 iliyopita, ulikuwa unasomaga magazeti?.
Gezeti hili uliwahi kulisoma?. Angalia ni la mwaka gani!.
Pasco
 
Pascal take strength from this indictment! Hii kwako ni recognition kwamba Paschal Mayallah a.k.a NJALA you are notable member of the fourth estate, a confident "pen pusher" of merit; nenda Dodoma with confidence, kwako hii ni fursa adhimu kusema unachokiamini na kuweka msimamo mzito kwanini uliandika ulichokiandika kwa makusudi mazima wala sio bahati mbaya, wape waheshimiwa wabunge darasa, usiogope, ni kweli utaadhibiwa na kukemewa kwa namna moja au nyingine kwani watu hao wana madaraka na hasira kwa ulichokiandika lakini katika adhabu wanazoweza kukupa sio kifungo wala kukuua bali kujaribu kukupunguza confidence! Kwa hiyo simama imara, pay them back in kind kwa kuwaambia ukweli kwa kadiri unavyoamini na jinsi dhamira yako ilivyokutuma kuandika, maana kusema ukweli kutakuweka huru, na pia kusema ukweli sio hodhi ya mtu mmoja peke yake "NJI" hii! wambie ukweli, ukweli mtupu ili nafsi na dhamira yako viwe huru, Paschal nasisitiza usiogope kwani There is no gain without pain! I wish you a good encounter@parliament.org
Sijawahi kuwa na Mashaka na Pascal, ninamuelewa mara zote.
 
Back
Top Bottom