Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 21,213
- 36,195
Habari za usiku huu,
Rejea kichwa cha habari, leo hakuna mahaba. Lengo la uzi huu ni kuwapa faraja wanaume wote hasa wale ambao wanapitia kipindi kigumu kwenye maisha yao. Najua kuna wanaume ambao hawapitii au hawajapatwa na changamoto za maisha au ugumu wa maisha. Basi wewe mshukuru mola wako na endelea kutoa sadaka yasikupate yanayowapata wenzio.
Hii video hapa chini iwape faraja, angalia hilo gari ni Benz moja ya kampuni kongwe inayotengeneza magari ya kifahari duniani. Ukilitazama hilo gari linaonekana limechoka na kuchakaa. Lakini dereva na using wake hawajakata tamaa, angalia njia wanazopita ubovu wa barabara, lakini wako tuu. Wanabeba chepeo au spedi, mawe, mchanga vipande vya miti na vigogo ili kurekebisha njia safari yao iendelee.
Maana ya kuiweka hii video hapa ni kuwafikirisha maisha ni safari ukibahatika kupata mteremko well and good. Ukikutana na changamoto ndo upambane. Wewe kama mwanaume ndo kiongozi wa familia yako ya baba na mama na ndugu zako wakati huo huo ukija kuoa na kuwa na mke na watoto wote watakutegemea wewe. Sasa ikitokea ukikutana na changamoto za maisha halafu ukakata tamaa maana yake ndo mwisho wa familia yako ya wazazi na ya mkeo na wanao.
Kikubwa ujue kuwa wewe ni zaidi ya hilo Benz, unauwezo wa kuishi mazingira yeyote yale na ukapata ana na maisha na utasikia malango yako. Ila peke yako huwezi...... shirikiana na mkeo, wazazi wako, ndugu zako mliozaliwa tumbo moja, rafiki, wafanyakazi au wafanyabiashara wenzio kila mmoja kwa nafasi yake ili usilemewe na changamoto za maisha.
Chukulia mfano dereva wa hilo Benz angekuwa yuko mwenyewe asingekuwa mbali maana eneo la kuelekezwa wapi aelekeze tairi peke yake angeshaingia mtaroni. Kushuka kila saa kuweka mawe magogo na kuondoa vizingiti ili gari ipite angechoka na safari ingeishia njiani.
Mwanaume Pambana Gangamala Pambana wewe ni Zaidi ya Benz.
Kasie Matata.