SPEEDAF Carrier na uhuni wenu wa kitoto mnaotufanyia

Sure, mzigo unatoka China kwa spidi ya ajabu, siku 7 tu upo Dar, halafu sasa hao speedaf wa bongo ndio wanauchukua na kukaa nao zaidi ya siku 7 hauoni movement yoyote ya mzigo, siku wakikutaarifu kwenda kuchukua wanatuma text tu hawataki kupokea simu, wanaweka location za ajabu ajabu..yaani miyeyusho. Kama wameanza na hili la kusign mizigo ya wateja basi wanazidi kuharibu.
"Sajo sogea Hapa Kigogo Mwembe jando uchukue Parcel yako Chap" hapo unatumiwa huo ujumbe wakati tayari jamaa yupo eneo husika badala ya kukutumia ujumbe kabla kwamba muda f'lan atakuwa maeneo hayo ili upate kujiandaa.
Mbaya zaidi Ukipiga simu ili uulize Mwembe jando eneo gani hasa haipokelewi na sms hazijibiwi ndio mnakuwa mmeshapotezana hapo hawakutafuti wala hawakupi majibu ya kueleweka kuhusu Sehemu zilipo Delivery point zao
 
Ni kweli ila speedaf maisha yake bongo ni mafupi tu kama period ya mwananmke
Binafsi sijakumbana na dhahama zao pakubwa maana parcel zangu zote nilizoagiza black friday zimepewa tracking za Singapore post so nitakutana nazo kwa wazalendo wa Posta .
parcel pekee zilizopitia kwa Speedaf ni zile super economy shipping so hazina mbambamba kivile
 
KALYNDA wamekuja kivingine hawa ngoja wasepe na Kijiji tuanze kuomboleza.
Sijui kwanini Tz hatupo serious kama Kenya yaani Ishu za maana kama hizo wanawapa wauni wa boda boda?
hivi hawa speedaf si ndio wale KIKUKUU au nakosea
 
Mkuu hv ku confirm kama mzigo umeupokea Au bado si mpaka uingie kwenye account yako….sasa hao speed wanawezaje kufanya hvyo ili hali hawana access na account yko…

mi huwa nanunua bidhaa ndogondogo Mara nyingi napokeaga kupitia posta…mara chache sana napokea kupitia kikuku
 
Binafsi sijakumbana na dhahama zao pakubwa maana parcel zangu zote nilizoagiza black friday zimepewa tracking za Singapore post so nitakutana nazo kwa wazalendo wa Posta .
parcel pekee zilizopitia kwa Speedaf ni zile super economy shipping so hazina mbambamba kivile

Aisee parcel’s za Black Friday mpaka leo hujapokea mkuu??
 
Mkuu hv ku confirm kama mzigo umeupokea Au bado si mpaka uingie kwenye account yako….sasa hao speed wanawezaje kufanya hvyo ili hali hawana access na account yko…

mi huwa nanunua bidhaa ndogondogo Mara nyingi napokeaga kupitia posta…mara chache sana napokea kupitia kikuku
Mfumo wa posta ni tofauti na speedaf mkuu
 
Mkuu hv ku confirm kama mzigo umeupokea Au bado si mpaka uingie kwenye account yako….sasa hao speed wanawezaje kufanya hvyo ili hali hawana access na account yko…

mi huwa nanunua bidhaa ndogondogo Mara nyingi napokeaga kupitia posta…mara chache sana napokea kupitia kikuku
Kuna tofauti kati ya kusaini kwamba umepokea mzigo na kuconfirm kwamba umepokea. Kusaini hakuhitaji logins ila kuconfirm lazima account yako ihusike kupitia wewe.
 
Naheshimu sana mawazo yako siku zote , je hapa nini kifanyike kufanya tuwatue hawa speedaf
Mi hawajanidhulumu, ila jamaa wapo kienyeji sana, unaweza ukamtuma mtu bila kitambulisho wala kitu chochote cha uthibitisho wakampa mzigo.
 
Back
Top Bottom